Tarura Tanzania

Directions Website

Tarura Tanzania Ukurasa rasmi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) "Barabara Bora kwa Maendeleo Ende

03/10/2026
TARURA NJOMBE YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ‎‎Njombe‎‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wi...
03/10/2026

TARURA NJOMBE YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
‎
‎Njombe
‎
‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Njombe inaendelea na utekelezaji wa miradi ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara inayolenga kuboresha usafiri, kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
‎
‎Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Meneja wa TARURA wilaya ya Njombe, Mhandisi Costantine Ibengwe amesema Wakala umejipanga kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inatekelezwa kwa ufanisi na kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia masharti ya mikataba.
‎
‎Amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa barabara ya Igeleke–Matalawe yenye urefu wa kilomita 1.16 kwa kiwango cha lami mradi unaolenga kuboresha kwa kiasi kikubwa usafiri na mawasiliano katika eneo hilo.
‎
‎"Mradi huu ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ambapo unajumuisha ujenzi wa boksi kalavati pamoja na uwekaji wa taa za barabarani", amesema.
‎
‎Katika hatua nyingine, Mhandisi Ibengwe amesema TARURA Wilaya ya Njombe imeendelea kuchukua hatua za maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha ikiwemo kuboresha na kusafisha mifereji ya maji katika maeneo mbalimbali.
‎
‎Amesema hatua hizo zinalenga kuhakikisha maji ya mvua yanaelekezwa katika njia sahihi na kupunguza uwezekano wa maji kuingia kwenye makazi ya wananchi huku miundombinu ya barabara ikiendelea kuwa katika hali nzuri.
‎
‎Kwa upande wake, Bw. Frank Mtewa mkazi wa Mji wa Njombe amesema ujenzi wa barabara ya Igeleke–Matalawe ni hatua muhimu kwa wananchi wanaotumia barabara hiyo katika shughuli zao za kila siku.
‎
‎"Barabara hii imekuwa changamoto kwetu lakini ikikamilika tutaweza kupita kwa urahisi zaidi hata wakati wa mvua", amesema.
‎
‎Utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea katika maeneo mbalimbali wilayani Njombe huku TARURA ikiendelea kuimarisha miundombinu ya barabara kwa lengo la kuwezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa kwa urahisi pamoja na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa usalama katika misimu yote.
‎

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA YA MAKANDANA-BUNGILA WILAYANI RUNGWE‎‎Rungwe, Mbeya‎‎Kiongozi wa Mbio za ...
02/10/2026

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA YA MAKANDANA-BUNGILA WILAYANI RUNGWE
‎
‎Rungwe, Mbeya
‎
‎Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Bw. Wazo Mwang’onda ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara ya Makandana–Bungila yenye urefu wa mita 500 kwa kiwango cha lami iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
‎
‎Mradi huo wenye thamani ya shilingi 457,404,300 unalenga kuboresha usafiri na mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii.
‎
‎Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi, Mwang’onda amewataka wakandarasi na wahusika wa mradi kuhakikisha ujenzi huo unakamilishwa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya ubora ili wananchi waanze kunufaika na barabara hiyo.
‎
‎Kwa upande wake, Meneja wa TARURA mkoa wa Mbeya, Mhandisi William Lameck amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea shughuli za maendeleo katika eneo hilo ikiwemo kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kufanyika kwa shughuli za biashara wakati wote.
‎
‎Mhandisi Lameck amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kutunza miundombinu hiyo akisema ujenzi na uboreshaji wa barabara unatumia fedha nyingi za serikali hivyo ni muhimu wananchi kuitunza ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa muda mrefu.
‎
‎Ameongeza kuwa utunzaji wa barabara utasaidia kupunguza gharama za matengenezo na kuwezesha fedha za serikali kuelekezwa katika miradi mingine ya maendeleo.

01/10/2026

‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE imefanikisha ukarabati wa barabara ya Igawilo–Nacheo yenye urefu wa kilomita 5.5 kwa kiwango cha changarawe mkoani Mbeya hatua iliyosaidia kuondoa changamoto ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo hususani wakati wa msimu wa mvua.
‎

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA LA MLOWO, MBARALI‎‎Mbarali, Mbeya‎‎Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe l...
01/10/2026

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA LA MLOWO, MBARALI
‎
‎Mbarali, Mbeya
‎
‎Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa daraja la Mlowo lenye urefu wa mita 13.40 lililopo kata ya Mahongole wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwa lengo la kuboresha mawasiliano na usafiri kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani.
‎
‎Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda amewataka wahandisi kusimamia kwa umakini ujenzi wa daraja hilo ili likamilike kwa wakati na kuanza kutumiwa na wananchi.
‎
‎Aidha, amewapongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa utekelezaji wa mradi huo.
‎
‎Kwa upande wake, Meneja wa TARURA mkoa wa Mbeya, Mhandisi Wiliam Lameck amesema ujenzi wa daraja la Mlowo umefikia asilimia 85 huku akieleza kuwa mradi huo unalenga kuondoa changamoto ya usafiri iliyokuwa ikiwakabili wananchi na wanafunzi hasa wakati wa msimu wa mvua.
‎
‎Mhandisi Lameck amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza daraja hilo pamoja na miundombinu inayozunguka eneo hilo ili iweze kudumu na kuwanufaisha kwa muda mrefu.

Address

Dodoma
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tarura Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share