Tarura Tanzania

Tarura Tanzania

Share

Ukurasa rasmi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) "Barabara Bora kwa Maendeleo Ende

30/05/2026


..
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativilla amepongeza kasi ya ujenzi wa miradi ya Tactic ikiwemo ujenzi wa stendi kuu ya mabasi ya manispaa ya Musoma na kuongeza kuwa ujenzi huo pia umezingatia ubora wa vifaa.

30/05/2026


..
Serikali imeingiza barabara ya Kampala University–Magole–Rada yenye kilomita 6.35 pamoja na barabara ya Njia Nne–Buyuni–Tuliani katika mpango wa DMDP II ambapo zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa awamu ili kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi wa Jimbo la Kivule.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange kwa Niaba ya Waziri wa Nchi, OWM-TAMISEMI, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kivule, Mhe. Douglas Didas Massaburi, Mei 29, 2026, Bungeni jijini Dodoma, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Madaraja na Barabara ya Kitunda - Nyangasa - Kibeberu hadi Magole kwa kiwango cha lami.

Dkt. Dugange amesema Serikali tayari imeanza taratibu za manunuzi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo huku ikiendelea kufanya matengenezo ya maeneo korofi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya usafiri hasa kipindi cha mvua.

“Kwa hiyo nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Kivule kwamba Serikali iko kazini na itahakikisha barabara hizi zinajengwa na zinapitika vizuri kwa manufaa ya wananchi,” amesema Dkt. Dugange.

Aidha, amesema Serikali imeendelea kutenga bajeti kuhakikisha barabara za Kitunda, Nyangasa, Kibeberu hadi Magohe zinapitika muda wote, huku ikijikita zaidi katika ujenzi wa barabara ya Kitunda–Mwangati kwa Mpalange ambapo kiasi cha shilingi milioni 950 kimetengwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

30/05/2026
Photos from Tarura Tanzania's post 29/05/2026

MRADI WA RISE WAONDOA KIKWAZO CHA MAWASILIANO KATA YA IYOGWE WILAYANI GAIRO

Gairo, Morogoro

Wakala ya Barabara za vijijini na mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE unaotekelezwa kwa mkopo nafuu toka Benki ya Dunia imekamilisha ujenzi wa barabara ya Iyogwe-Chogohali yenye urefu wa Km 21.5 wilayani Gairo mkoani Morogoro na kuondoa kikwazo cha mawasiliano kati ya kata ya Iyogwe na Chogohali pamoja na wilaya jirani ya Mvomero.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TARURA wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala wakati wa ziara maalum ya kutembelea miradi ya RISE inayotekelezwa chini ya programu ya kuondoa vikwazo barabarani (Bottleneck).

Amesema ujenzi wa barabara hiyo umehusisha ujenzi wa makalavati madogo madogo ya zege tisa na kubwa moja lenye midomo minne ambalo kabla ya ujenzi wake eneo hilo lilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa wananchi hao.

"Tulipata fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa RISE ambapo baada ya kupata fedha hizo tulizielekeza kwenye barabara hii kwa ajili ya kuondoa vikwazo ambavyo wananchi wetu kutoka upande wa Chogohali walikuwa wanashindwa kwenda kupata huduma katika wilaya yetu ya Gairo".

Amesema vijiji vya ng'ambo ya pili ya mto vinategemea huduma zote za kijamii k**a vile vituo vya afya na shule ya sekondari upande wa Iyogwe na makao makuu ya wilaya mjini Gairo kwa hiyo walikuwa wanapata shida hasa kipindi cha masika kwani walikuwa wanashindwa kuvuka hivyo kulazimika kusubiri mpaka maji yapungue.

Kwa upande wa kiuchumi, Mhandisi Masala amesema barabara hiyo inaunganisha wilaya ya Gairo na wilaya jirani ya Mvomero na kuongeza kuwa kabla ya ujenzi huo wananchi kutoka pande zote walikuwa hawawezi kuingia kwenye wilaya hizo kupitia barabara hiyo ambayo ni fupi na kulazimika kuzunguka kupitia njia nyingine ambayo ina urefu wa zaidi ya Km 60.

"Baada ya kuifungua barabara hii wilaya jirani ya Mvomero na kata zao za jirani wanakuja kupata huduma hapa wilaya ya Gairo kwa hiyo wananchi wanapata huduma kwa urahisi zaidi katika muunganiko wa kiuchumi kwa kuuza na kununua mazao yao na bidhaa nyingine", amefafanua.

29/05/2026


..
Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 97 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kilomita 36 kupitia mradi wa DMDP II wilayani Kinondoni ikiwa ni katika mkakati wa kutatua adha ya usafiri wilayani humo ambapo TARURA inaendelea kusimamia wakandarasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati na kwa viwango bora.

Akizungumza wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam alipotembelea ujenzi wa miradi ya barabara na madaraja Meneja wa TARURA wilaya ya Kinondoni Mhandisi Edwin Kabwoto amesema kupitia fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 97 zilizotengwa na serikali kwa ajili ya wilaya ya kinondoni amebainisha kuwa ujenzi wa barabara wilayani humo unaofanyika chini ya DMDP II umegawanywa kwenye "package" nne ili ufanyike kwa urahisi na tayari baadhi ya "package" zipo katika hatua za umaliziaji.

Akizungumzia ujenzi wa miradi ya barabara zilizoharibiwa na mvua yaani CERC Mhandisi Kabwoto amesema wilaya ya Kinondoni imetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 8 ambapo ndani ya mradi huo wanaendelea na ujenzi wa daraja la Nakalekwo, daraja la Mikoroshini ambao umefikia asilimia 95.

Aidha, amesema pia wana ujenzi wa barabara ya Maelaela makaburini eneo la chasimba inayojengwa kwa kiwango cha zege pamoja na barabara ya makaburini Chatembo pia barabara ya kilonga wima.

28/05/2026

Wananchi wa manispaa ya Tabora wameishukuru serikali kwa ujenzi wa daraja pamoja na maingilio ya barabara mita 290 kwenye barabara ya Ndovelwa yenye urefu wa Km 20.2.

28/05/2026

Repost
..
Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Temeke Mhandisi Paul Mhere anaeleza hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha

🇹🇿 kissfm2026kuwaleokablayakesho

28/05/2026

Wananchi wa kijiji cha Chiuve kata ya Nangomba wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara sasa wamepata suluhu ya kudumu ya mawasiliano baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja katika mto Masyalele.

Photos from Tarura Tanzania's post 28/05/2026

TARURA NANYUMBU YAKAMILISHA UJENZI DARAJA LA MAWE LA SOMOE ISSA

Nanyumbu, Mtwara

Wananchi wa kijiji cha Chiuve kata ya Nangomba wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara sasa wamepata suluhu ya kudumu ya mawasiliano baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja katika mto Masyalele.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TARURA wilaya ya Nanyumbu, Mhandisi Dickson Mkokota wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo.

Amesema ujenzi wa daraja hilo lililojengwa katika barabara ya Chiuve-Kalipinde umetekelezwa na Mkandarasi Central Highway kwa gharama ya shilingi 120,560,360 na umekamilika kwa asilimia 100.

Mhandisi Mkokota ameongeza kuwa kabla ya ujenzi wa daraja hilo wananchi wa vijiji vya Chiuve na Kalipinde walikuwa wanatumia kivuko aina ya "drift" ambacho wakati wa mvua walikuwa wanapata shida kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili kwa ajili ya kupata huduma za kijamii na kiuchumi k**a vile hospitali na masoko.

"Manufaa makubwa yaliyopatikana kwenye mradi huu ni watu wamerahishiwa kuvuka katika eneo hili la mto", amesema.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mkokota daraja hilo limepewa jina la Somoe Issa kwa sababu kabla ya ujenzi wa daraja alitokea mama mmoja mjamzito kutoka Kijiji cha Chiuve kwenda kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Mangaka na kwa bahati mbaya alipofika katika eneo hilo alikuta maji yamejaa na kushindwa kuvuka na kujifungua mtoto ambaye amepewa jina la Somoe Issa hivyo wananchi wa kijiji hicho walipendekeza daraja hilo kuitwa Somoe Issa.

Kwa upande wake, Bi. Ashura Hamis ambaye ni mama wa mtoto Somoe Issa mkazi wa kijiji cha Chiuve amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea changamoto hiyo ya muda mrefu.

"Namshukuru sana mama Samia na serikali yake kwa hili lililofanyika na kwa wamama wenzangu ambao tumejifungulia hapa.
Nashukuru kwa kupewa jina la mwanangu daraja hili Somoe Issa", ameeleza.

Naye, Bw. Rajabu Chakubanga mkazi wa Mangaka Kilimahewa ambaye ni mkulima amesema ukosefu wa kivuko katika eneo hilo ilikuwa ni changamoto kubwa kwao hasa wakati wa kusafirisha mazao yao kutoka mashambani lakini kwa sasa wanashukuru kwani hata gharama za usafirishaji zimepungua.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Dodoma
255