Takukuru.tz

Takukuru.tz

Share

Hii ni akaunti rasmi ya TAKUKURU TANZANIA.

27/05/2026
27/05/2026

TAKUKURU KATAVI YAOKOA SH. 34,851,040/= NA NG’OMBE SITA

TAKUKURU Mkoa wa Katavi katika robo ya *Januari - Machi 2026* iliokoa jumla ya Sh. 34,851,040/= pamoja na Ng’ombe sita.

Kati ya fedha hizo:
🖊️Sh. 28,258,040/= zilirejeshwa kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, ambazo baadhi ya watumishi walikusanya ushuru kupitia mashine za POS lakini hawakuwasilisha fedha benki.
🖊️Sh. 509,000/= zililipwa kwa mlalamikaji baada ya kucheleweshewa malipo ya kazi ya huduma za maji MUWASA.
🖊️Sh. 1,700,000/= pamoja na ng’ombe 6 zilirejeshwa kwa mwananchi aliyetozwa k**a faini ya kusingiziwa katika kesi ya mauaji, huku hatua za kinidhamu zikiendelea dhidi ya waliohusika.

🖊️Sh. 3,184,000/= zilirejeshwa kwenye akaunti ya kitongoji cha Mbogwe Wilaya ya Tanganyika baada ya viongozi wa kitongoji na sungusungu kugawana fedha hizo.

🖊️Sh. 1,200,000/= zilirejeshwa katika akaunti ya kijiji cha kalalamsenga baada ya Afisa Mtendaji wa kijiji hicho kutoa fedha katika akaunti ya kijiji na kuzitumia kwa manufaa yake binafsi.

23/05/2026

MAFUNZO YA WELEDI – UTATU ARUSHA

Watumishi wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha wameshiriki katika mafunzo ya weledi yaliyoandaliwa na taasisi zinazounda ushirikiano wa UTATU mkoani humo.

Taasisi nyingine zilizoshiriki katika mafunzo hayo ni Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha utendaji kazi katika uchunguzi na uendeshaji wa mashauri mahak**ani kupitia kubadilishana uzoefu wa kikazi.

TAKUKURU Arusha - Mei 22, 2026

23/05/2026

UELIMISHAJI KUHUSU ATHARI ZA RUSHWA YA NGONO - BUNGU SEKONDARI

Wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa na wanafunzi wasio wanachama wa klabu hiyo, wamependekeza kuwekewa sanduku la maoni shuleni hapo, ili waweze kutoa kero zao kwa usiri.

Pendekezo hilo limetolewa baada ya maafisa wa TAKUKURU kuwasilisha kwao mada iliyohusu athari za rushwa ya ngono katika jamii.

TAKUKURU Korogwe, Mei 18, 2026

21/05/2026

VYAMA VYA USHIRIKA VYASISITIZWA UMUHIMU WA USHIRIKIANO NA TAKUKURU KUIMARISHA UADILIFU.

“Vyama vya Ushirika mnapaswa kuzingatia uadilifu na kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwani makubaliano yaliyoingiwa kati ya TAKUKURU na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), yanalenga kuimarisha uadilifu ndani ya vyama vya ushirika.”

Hayo yamesemwa na Mhe. Nurdin Babu - Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro, lililofanyika katika ukumbi wa YMCA - Moshi Mjini.

TAKUKURU Kilimanjaro, Mei 14, 2026

21/05/2026

MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026 - RUVUMA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Ndg. WAZO MICHAEL MWANG'ONDA, ametembelea Klabu ya Wapinga Rushwa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Mbinga (FDC) iliyopo Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

Kiongozi huyo ameipongeza TAKUKURU kwa jitihada nzuri za kuwashirikisha vijana kwenye mapambano dhidi ya Rushwa.

TAKUKURU Mbinga - Ruvuma Mei 17, 2026

21/05/2026

TAMASHA LA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA KATAVI

“Ninawapongeza washiriki wote kwa kushiriki vizuri katika tamasha hili.
Rushwa ni Adui wa Haki; mmekua mashuhuda katika mapambano dhidi ya Rushwa kupitia kuandaa nyimbo, ngojera na maigizo.
Hivyo ni vizuri mkawe darasa linalotembea, mkatusaidie kwenye maeneo yenu ya shule pamoja na makazi mnayo ishi, ili elimu hii iweze kuwafikia jamii nzima”.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mgeni Rasmi (Mkuu wa Wilaya) Bw. Mbonimpaye Nkoronko, katika tamasha la wapinga rushwa Katavi.

TAKUKURU Katavi, MEI 15, 2026

15/05/2026

ESAMI NA TAKUKURU KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MAFUNZO

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, Mei 14, 2026 amepokea ugeni wa Mkuu wa Chuo cha ESAMI cha Jijini Arusha - Profesa Peter Kiuluku, aliyemtembelea katika ofisi za TAKUKURU Upanga Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, Mkurugenzi Mkuu wa The Eastern and Southern African Management Institute - ESAMI, alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa kuruhusu watumishi kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayoendeshwa na chuo hicho.

Profesa Kiukulu alieleza kuwa ESAMI ni chuo cha umma ambacho pamoja na mambo mengine, kina wajibu wa kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa umma wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama k**a TAKUKURU, kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Jamhuri Street
Dodoma
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00