Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mei 29, 2026 limeweka Azimio la kuipongeza Timu ya Taifa ya Vijana wa Umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kufuzu kucheza mchezo wa Fainali ya michuano ya AFCON 2026 inayoendelea nchini Morocco na kukata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar.
Gerson Msigwa
The Permanent Secretary of Information, Arts and Sports & Chief Government Spokesperson|Former DPC.
Maelezo kamili ya mwekezaji na tajiri wa Afrika Alhaji Aliko Dangote kuhusu uwekezaji wake Tanzania muda mfupi baada ya kukutana na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 16 Mei, 2026.
Dondoo, Alhaji Dangote anasema;
1. Tanzania ni nchi yenye mazingira bora na ya uhakika kwa uwekezaji ikichagizwa na nguvukazi kubwa ya vijana.
2. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi shupavu na mwenye dhamira ya dhati ya kutekeleza mipango iliyowekwa katika kukuza uwekezaji.
3. Kampuni yake ya Dangote inaridhishwa na imepata mafanikio makubwa katika uwekezaji wake wa kiwanda cha saruji Mkoani Mtwara na hivyo;
i) Itapanua kiwanda hicho kwa kuongeza uwekezaji na usambazaji ukiwemo kununua malori mapya 600 ya kusafirishia saruji
ii) Inafanyia kazi uwekezaji katika kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi (refinery) hapa nchini.
iii) Itajenga kiwanda cha mbolea ili kusaidia upatikanaji wa bidhaa hiyo.
iv) Inakusudia kuwekeza katika bandari ya Bagamoyo
Na ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa na kuanza safari ya kuwa matajiri wakubwa k**a alivyoanza yeye kwa mtaji mdogo lori nne za saruji na sasa anamiliki kampuni kubwa ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa 120 Duniani, na kwamba kampuni zake zinazalisha ajira kwa maelfu ya watu.
Mwambie jirani ya HAHAA HABARI NDO HIYO.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo katika kuiimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TaDB) kwa kuipatia mtaji wa shilingi Bilioni 452 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima ili kuongeza uzalishaji, tija na kuongeza kipato cha wananchi.
Dondoo;
1. TaDB imeweza kukopesha wakulima mikopo ya moja kwa moja ya kiasi cha shilingi trilioni 1.43
2. Wanufaika 2,600,000 wamefikiwa
3. TaDB imetoa mikopo ya dhamana kwa wakulima yenye thamani ya shilingi Bilioni 621.39 kwa wanufaika 639,543
4. Katika Nyanda za Juu Kusini, TaDB imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 173.11 kwa wakulima.
na alama zisizofutika Tanzania.
Ziara ya Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame nchini Tanzania leo tarehe 03 Mei, 2026.
Biashara ya Tanzania na Rwanda imekuwa na itakuwa zaidi siku zijazo.
Tulinde maadili ya Mtanzania.
Mhe. Paul Christian Makonda
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza katika uzinduzi wa Mkakati wa Utekelezaji wa Mwongozo wa Maadili ya Taifa katika ukumbi wa Wizara uliopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 29 Aprili, 2026.
Kujali,
Dhamira Njema,
Ujasiri,
Utu,
Matumaini.
NI UONGOZI.
Sikiliza simulizi hii iliyojaa matumaini, dhamira njema na uthubutu wa kulinda maisha ya Watanzania na hata wageni.
Ni uwekezaji wa zaidi ya shilingi Bilioni 50 katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam ulioleta mageuzi makubwa katika matibabu nchini Tanzania na kutegemewa na ukanda wote wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Asante Mheshimiwa Rais Dkt.
Serikali imekamilisha ujenzi wa Bandari ya Karema iliyopo Mpanda Mkoani Katavi katika Ziwa Tanganyika na kuwezesha uwekezaji kutoka sekta binafsi wa meli 4 za mizigo ambazo zipo katika hatua za mwisho za kukamilika.
Dondoo;
1. Kila meli moja ina uwezo wa kuchukua tani 2,000 za mzigo (Jumla tani 8,000 kwa mpigo)
2. Meli hizi zitafanya safari kati ya Bandari ya Karema Tanzania na Bandari ya Kalemii nchini DRC
3. Zitawezesha usafirishaji wa zaidi ya Tani Milioni 2 za mizigo kwa mwaka kwenda DRC (Hii itakuwa ni mara ya kwanza kufikia rekodi ya usafirishaji wa kiwango hicho kikubwa cha mzigo)
4. Wawekezaji wa meli hizi pia watajenga Bandari ya Kigoma na bandari ya Kalemii nchini DRC pamoja na kujenga kilometa 500 za barabara ya lami kati ya Kalemii na eneo la madini la Manono ambalo lina mgodi mkubwa zaidi Duniani wa madini aina ya Lithium yanayotumika kutengeneza betri za magari.
5. Uwekezaji huu unatajiwa kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
Uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Tunajitosheleza kwa chakula kwa asimilia 130.
Msikilize Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph. C. Ndunguru, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo na fursa kwa vijana, Machi 24, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
//
Dondoo;
ya miaka mitatu, mamlaka imepata mafanikio makubwa kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa na usalama na utoshelevu wa chakula kwa asilimia 130.
kipindi cha miaka mitatu iliyopita, TPHPA imefanikiwa kudhibiti uvamizi wa ndege waharibifu wa mazao aina ya kwelea kwelea wapatao milioni 231 katika halmashauri 23 zenye skimu kubwa za kilimo cha mpunga, uwele na mtama, na kuokoa jumla ya tani 1,600,000 za mazao hayo.
imepata mafanikio makubwa katika kudhibiti balaa la panya lililokuwa likiathiri uzalishaji wa mazao kwa wakulima katika mikoa 16, wilaya 68 na vijiji 1,669, na kuokoa tani 400,008 za mazao ya wakulima.
#*TPHPA katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 imewezesha usafirishaji wa jumla ya tani milioni 6.6 za mazao mbalimbali yakiwemo mbogamboga na nafaka, na mauzo yake kuiingizia nchi dola za Marekani bilioni 6.6 sawa na shilingi trilioni 15.6.*
imewezesha kufunguliwa kwa soko la zao la parachichi katika nchi za Afrika Kusini, India, China na Marekani.
Tumewezesha mazao 14 kupata masoko katika nchi 15, yakiwemo pilipili manga, nanasi, vanila, tumbaku, ndizi, makademia na ngano.
Tumeweza kusajili kampuni 16 za parachichi kusafirisha matunda kwenda nchini China, pamoja na kuwezesha kampuni nyingine 408 kufanya biashara katika soko hilo.
Mamlaka imenunua ndege nyuki (drones) za kisasa kwa ajili ya kuchunguza mashamba ya kilimo na kubaini mapema uwepo wa visumbufu vya mazao ili kuvidhibiti kabla havijasababisha madhara makubwa.
Mamlaka imenunua ndege ya kisasa kwa ajili ya kunyunyizia viuatilifu yenye uwezo wa kunyunyizia katika eneo la ekari 2,400 kwa wakati mmoja.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Kisasa
Dodoma
