Ofisi ya Rais-UTUMISHI

Ofisi ya Rais-UTUMISHI

Share

Jukumu kubwa la OR-MUUUB ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu

14/05/2026

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

14/05/2026

WAUGUZI WATAKIWA KUWA NA KAULI NZURI,HURUMA NA UPENDO KATIKA UTENDAJI WAO

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 13/05/2026

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

Na. Antonia Mbwambo-Arusha
Tarehe 12 Mei, 2026.

Watumishi wa Umma nchini wamehakikishiwa kuboreshewa mazingira ya kazi kadri uchumi utakavyoruhusu ili kuleta tija katika utendaji kazi kwa maslahi ya umma.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika leo tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Mhe. Qwaray amesema, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Watumishi wa Umma wote nchini wakiwemo Wauguzi, hivyo itazingatia changamoto wanazokutana nazo watumishi hao, pamoja na kushughulikia kwa uzito unaostahili ili kutengeneza mazingira mazuri ya utendaji kazi.

"Niwahakikishie Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi wa Umma kadri uchumi utakavyoruhusu kwani tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuwahudumia Watanzania, fanyeni kazi, Serikali ipo nanyi." Mhe. Qwaray alisema.

Aidha Mhe. Qwaray ameongeza kuwa, ili kuwa na ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi Serikali itaendelea kuisimamia sekta ya afya pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma bila kuathiri misingi ya Utumishi wa Umma, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ikiwemo uzingatiaji wa maadili.
Aidha amewataka kuwa na kauli nzuri, huruma na upendo utakaoongeza tija katika utendaji kazi ili kuleta mabadiliko chanya katika Sekta ya afya.

"Ninyi ndiyo watu wa kwanza kukutana na mgonjwa pindi anapofika hospitali na ni watu wa mwisho mgonjwa anapotoka hospitali baada ya matibabu, ikiwa mtakuwa na nyuso za ukatili na ulimi mkali au wa kebehi, mtawakwaza wagonjwa na hata kuwakatisha tamaa jambo ambalo litaonyesha mapungufu katika sekta ya afya.”Mhe. Qwaray alisema.

Vilevile, Mhe. Qwaray amewaahidi Wauguzi hao kuwa Ofisi imepokea masuala yote waliyoyaeleza katika risala yao na kuwaahidi kuyawasilisha kwa ajili ya kufanyiwa kazi ikiwemo masuala ya Muundo Mpya wa Utumishi wa Kada ya Uuguzi na Ukunga na Muundo wa Utawala katika Sekta ya Afya ili kuboresha huduma ya afya na maslahi ya watumishi wa afya nchini.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Qwaray, ametoa wito kwa wauguzi kuhahakisha wanabadili mienendo na tabia zisizopendeza wala kuendana na maadili ya kazi yao, lakini pia amewapongeza kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi na kuboresha afya zao.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wauguzi (TANNA), Dkt. Ezekiel Mbao amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kujumuika nao kwenye maadhimisho ya siku hiyo adhimu.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Wauguzi Duniani yamebeba kauli mbiu isemayo �Wauguzi Wetu, Mustakabali Wetu, Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha.�

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 04/05/2026

AFYA NI MTAJI – KATIBU MKUU MKOMI AWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUJILINDA

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 04 Mei, 2026

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amewasisitiza watumishi wa umma kulinda na kuimarisha afya zao wakati wote ili zitumike kuwajibika ipasavyo na kuwa mtaji katika kuleta matokeo chanya Serikalini.

Bw. Mkomi ameyasema hayo leo Mei 4, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba Jijini Dodoma wakati akihitimisha mafunzo kuhusu fursa za mimea tiba katika kutibu magonjwa mbalimbali.

“Ni vizuri kila mtumishi wa umma akawa na uelewa kuhusu faida za utunzaji wa afya aliyo nayo na kuchukua hatua mapema pindi anapopata changamoto ili kuitumia afya hiyo kuwa mtaji Serikalini na kuleta tija katika maslahi ya umma”. Bw. Mkomi alisema.

Amesisitiza kuwa changamoto ya watumishi wengi kuugua mara kwa mara inapunguza kasi ya utendaji, lakini watumishi wanapokuwa na afya bora, hupunguza kuomba likizo za ugonjwa, na hivyo kuongeza bidii ya kazi.

Aidha, Bw. Mkomi amemshukuru Prof. Joseph Ndunguru ambaye ni Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) kwa wasilisho lake ambalo limetoa uelewa kwa watumishi utakaojenga hamasa na kuwa nyenzo muhimu ya kuongeza ufanisi katika kazi.

Awali akiwasilisha mada kuhusu fursa za Mimea Tiba katika Kutibu Magonjwa mbalimbali, Prof. Ndunguru alisema Tanzania ina utajiri mkubwa wa mimea yenye uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali lakini bado inahitaji utafiti wa kisayansi ili kuthibitisha usalama na ufanisi wake.

Aliongeza kuwa matumizi ya tiba asili yaliyofanyiwa tafiti za kisayansi yanapunguza magonjwa, hivyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu na kuboresha afya ya watumishi.

Prof. Ndunguru ametoa wito kwa Serikali na Taasisi za Umma kuwekeza katika tafiti ili kuendeleza tiba asili na kuchangia maendeleo ya afya na uchumi wa Taifa.

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 01/05/2026

HERI YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI)

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 01/05/2026

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI)

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, leo tarehe 1 Mei, 2026 wameungana na watumishi wengine kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yenye kauli mbiu isemayo “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050” ambapo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 01/05/2026

HERI YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 30/04/2026

KIKAO KAZI CHA MAAFISA BAJETI KUTOKA OFISI YA RAIS, -UTUMISHI KWA KILICHOLENGA KUKAMILISHA MPANGO MKAKATI WA OFISI HIYO

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 28/04/2026

WATUMISHI WALIOZALIWA MWEZI APRILI WAPONGEZWA

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 27 Aprili, 2026

Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Ofisi hiyo Bi. Mwanaamani Mtoo niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI amewapongeza na kuwatakia kila la kheri watumishi wawote waliozaliwa mwezi Aprili ambapo kwa kumbukizi hiyo wamepata nafasi ya kukata keki k**a ishara ya kuendeleza umoja na mshik**ano ili kuimarisha utendaji kazi.

Matukio mbalilmbali ya picha za watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, waliokuwa wanaadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa ya mwezi Aprili, yaliyofanyika katika Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 28/04/2026

MKURUGENZI OFISI YA RAIS UTUMISHI AAGWA RASMI

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 27 Aprili, 2026

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Nolasco Kipanda kwa niaba ya Katibu Mkuu na Watumishi wote wa Ofisi hiyo amemuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu wa Ofisi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa ambaye amestaafu kwa kwa mujibu wa Sheria.

Bw. Kipanda ameyasema hayo Aprili 27, 2026 katika eneo maalum la mafunzo lililopo katika ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.

Amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi itamkumbuka Mkurugenzi huyo kwa upendo wake, umahiri, ujasiri, mchango na kazi nzuri aliyoifanya ya kuleta tija katika utumishi wa Umma.

Kwa upande wake, Bi. Mwanilwa amewaasa watumishi hao kufanya kazi kwa umoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kutoa huduma kwa haki na usawa.

Bi. Mwanilwa aliwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujituma huku wakizingatia maadili ya utendaji ili kuufikia mwisho mwema wa utumishi wao.

Photos from Ofisi ya Rais-UTUMISHI's post 28/04/2026

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI KWA WATUMISHI WA UMMA KUONGEZA UFANISI

Na. Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 27 Aprili, 2026

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Leila Mavika amesema mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watumishi wa umma ni muhimu kwa kuwa yanaongeza uelewa wa kutambua, kuchambua na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaj kazi wa shughuli za Serikali.

Bi. Mavika ameyasema hayo Aprili 27, 2026 wakati akimwakilisha Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi katika kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wa Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.

Bi. Mavika meongeza kuwa, kutokana na uelewa ambao umepatikana wakati wa mafunzo hayo ni imani yake kuwa kila mtumishi wa ofisi hiyo atakuwa na uwezo wa kuchambua na kutambua vihatarishi vilivyopo katika eneo lake la kazi na kuvidhibiti kabla ya madhara kutokea.

Awali, Afisa Ukaguzi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha Bi. Adolphina Lugando amesema, Serikali imeweka msisitizo kwa Wizara na Taasisi za umma kuimarisha mifumo ya udhibiti wa vihatarishi ili kuboresha uwajibikaji.

Vilevile Bi. Lugando alitoa wito kwa watumishi wa kila Idara na vitengo kuhakikishe wanatambua vihatarishi vinavyoweza kutokea katika Idara na vitengo vyao ili kuimarisha usalama.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


670
Dodoma