Ofisi ya Rais-UTUMISHI

Call Directions Website Contact the organization

Ofisi ya Rais-UTUMISHI Jukumu kubwa la OR-MUUUB ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu

DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 ITUMIKE KUBORESHA UTENDAJI NA KUHAKIKISHA MIPANGO YA SERIKALI INATEKELEZEKA KWA WANANCHI...
21/10/2026

DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 ITUMIKE KUBORESHA UTENDAJI NA KUHAKIKISHA MIPANGO YA SERIKALI INATEKELEZEKA KWA WANANCHI-Mhe. Qwaray

Na Veronica Mwafisi-Kilwa
Tarehe 21 Oktoba, 2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema Watumishi wa Umma ni miongoni mwa nguzo kuu ya kufanikisha malengo ya taifa hivyo, katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni vema kila mtumishi akaongeza tija, kuboresha utendaji na kuhakikisha mipango ya Serikali inatafsiriwa kwa huduma na matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi.

Mhe. Naibu Waziri Qwaray ameyasema hayo leo tarehe 21 Oktoba, 2026 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

Mhe. Qwaray amesema, lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi hao na kujadili namna bora ya kuimarisha utendaji kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Naibu Waziri Qwaray alitoa fursa kwa watumishi hao na kusikiliza changamoto na hoja mbalimbali zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yao ambapo baadhi alizifanyia kazi na nyingine alizielekeza kwa Maafisa Utumishi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa haraka.

Vilevile Naibu Waziri Qwaray amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa ili kufikia uchumi wa kipato cha kati cha juu ni wajibu wa Watumishi hao kuongeza kasi ya utendaji, kutumia teknolojia ipasavyo na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma stahiki kwa wakati, kwa haki na bila usumbufu.

Akihitimisha hotuba yake wakati akizungumza na Watumishi hao Mhe. Qwaray amesema, Utumishi wa Umma ni dhamana hivyo, kila mmoja awajibike katika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, taratibu, weledi na maslahi mapana ya Taifa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omari ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo ikiwemo majengo ya kutolea huduma mbalimbali za afya, shule, nyumba za watumishi, majengo ya utawala pamoja na miundombinu jambo ambalo linawapa ari ya utendaji kazi Watumishi wa Halmashauri hiyo

WARATIBU WA AFUA ZA VVU, UKIMWI NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA WAKUTANA MBEYAWaratibu wa Afua za Kudhibiti VVU, UKIMWI ...
21/10/2026

WARATIBU WA AFUA ZA VVU, UKIMWI NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA WAKUTANA MBEYA

Waratibu wa Afua za Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) ngazi ya Wizara wamekutana Oktoba 20, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kwa kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, kilicholenga kupitia na kutathmini utekelezaji wa afua hizo, kubaini hatua zilizofikiwa na changamoto zilizojitokeza, pamoja na kujadili mikakati ya kuimarisha uratibu na utekelezaji wake katika Wizara na Taasisi za Umma.

KAMATI YA KITAIFA YAJADILI UIMARISHAJI WA UDHIBITI WA VVU, UKIMWI NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA MAHALI PA KAZIKamati ya Kit...
21/10/2026

KAMATI YA KITAIFA YAJADILI UIMARISHAJI WA UDHIBITI WA VVU, UKIMWI NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA MAHALI PA KAZI

Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza wameshiriki majadiliano katika kikao cha k**ati hiyo kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Kikao hicho kilijadili utekelezaji wa Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma, pamoja na hatua za kuimarisha uratibu na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa afua hizo.

BW. MWINUKA ASISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA AFYA YA WATUMISHI WA UMMANa. Antonia Mbwambo – MbeyaTarehe 19 Oktoba, 2026Mw...
21/10/2026

BW. MWINUKA ASISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA AFYA YA WATUMISHI WA UMMA

Na. Antonia Mbwambo – Mbeya
Tarehe 19 Oktoba, 2026

Mwakilishi wa Katibu Mkuu -UTUMISHI, ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Ufuatiliaji wa Sera katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Olgatho Mwinuka, amezitaka Wizara na Taasisi za Umma kuimarisha afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY), pamoja na kuweka mikakati ya kulinda afya ya akili ya watumishi mahali pa kazi, kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bw. Mwinuka ameyasema hayo Oktoba 19, 2026, wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi, katika ufunguzi wa kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 cha Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Amesema kuwa hatua za kudhibiti magonjwa hayo zinapaswa kujumuishwa katika mipango, bajeti na shughuli za kawaida za Wizara na Taasisi za Umma ili kulinda afya za watumishi na kuongeza ufanisi kazini.

“Afya ya mtumishi ni sehemu muhimu ya mafanikio ya Taasisi. Hivyo, ni wajibu wa kila mwajiri kuhakikisha afua hizo zinatekelezwa kwa vitendo, pamoja na kuimarisha huduma za afya ya akili na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watumishi,” amesema Bw. Mwinuka.

Katika kuimarisha utekelezaji wa afua hizo, Bw. Mwinuka amewahimiza waajiri kutoa elimu na mafunzo kwa watumishi na kujenga uwezo wa k**ati, waratibu na waelimishaji rika wanaohusika na kazi hiyo.
Amebainisha kuwa Ofisi hiyo itaendelea kushirikiana na Wizara na Taasisi za Umma katika kufuatilia utekelezaji, kutathmini mafanikio na kubaini changamoto zinazohitaji ufumbuzi.

Kadhalika Bw. Mwinuka amezitaka Wizara kuhakikisha Taasisi za Umma zilizo chini yake zinatekeleza Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2014 na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa wakati. Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kutathmini maendeleo, kubaini changamoto na kupanga maboresho yanayohitajika.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Anuai za Jamii ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bi. Juliana Ntukey ametoa wito kwa wajumbe wa kikao hicho kushiriki kikamilifu ili kupata maazimio yatakayoimarisha utendajikazi katika maeneo yao ya kazi kwa ustawi wa Taifa.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI (TGFA) KWA KUTEKELEZA MAJU...
16/10/2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI (TGFA) KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA WELEDI NA UFANISI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MRADI WA UJENZI WA MAKAZI KWA WATUMISH...
15/10/2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MRADI WA UJENZI WA MAKAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 15 Oktoba, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia taasisi yake ya Watumishi Housing Investments (WHI) baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya makazi kwa Watumishi wa Umma nchini.

Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Kamati hiyo mara baada ya kuhitimisha ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi eneo la Njedengwa na Mlezi jijini Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Edwin Swalle amesema ujenzi wa nyumba hizo unaakisi maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupeleka tabasamu kwa Watumishi wa Umma kwa kuwa na uhakika wa makazi.

“Kwa niaba ya Kamati hii, nitoe pongezi kwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia WHI, nyumba 1500 zilizojengwa kwa ajili ya Watumishi wa Umma nchi nzima zitasaidia kupunguza changamoto ya makazi kwa Watumishi wa Umma katika maeneo mengi nchini, kwa hakika mnafanya kazi nzuri ya kumwakilisha Mhe. Rais kwa kupeleka tabasamu kwa Watumishi wa Umma ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.” Amesema Mhe. Swalle.

Aidha, Mhe. Swalle ameuelekeza uongozi wa WHI kuangalia namna ya kupata benki ya ardhi katika maeneo mengi ili wajenge nyumba nyingi zaidi kwani watumishi wengi wana changamoto ya makazi jambo ambalo hutishia watumishi hao kutaka kuhama.

“Watumishi wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki, nashauri Ofisi iweke kipaumbele kutafuta benki ya ardhi maeneo mbalimbali ili muwe na uhakika wa kufanya miradi maeneo mbalimbali kutokana na uhitaji mkubwa wa nyumba za watumishi.” Amesisitiza.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema lengo la mradi huo ni kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma.

Amesema, WHI imeweka utaratibu wa namna ya kulipa fedha kwa wanaonunua nyumba hizo ili kuwapunguzia mzigo wa kulipa fedha nyingi kwa mkupuo kwa kuzingatia uwezo wao wa kifedha.

Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani amesema, Taasisi hiyo ya WHI imeanzisha dirisha la e-wekeza kwenye mfumo wa Watumishi Portal ambalo linawawezesha Watumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida Fund) kupitia makato ya hiari ya mshahara kila mwezi.

Mhe. Kikwete amesema, hatua hiyo imelenga kuwawezesha Watumishi wa Umma kujenga tabia ya kuwekeza na kuongeza uwezo wao wa kununua nyumba kabla na baada ya kustaafu. “Hivyo, e-wekeza ni hatua ya nyongeza ya uwezeshaji wa kifedha, sambamba na njia za kumiliki nyumba zinazotolewa na WHI,” ameongeza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Waziri Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray aliwashukuru wajumbe wa k**ati hiyo kwa ushirikiano, miongozo na maelekezo ambayo wamekuwa wakitoa mara zote ambayo yamewezesha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo pamoja na taasisi zake kwa ufasaha

Kwa niaba ya Waziri wake, Mhe. Qwaray ameiahidi k**ati hiyo kuyafanyia kazi maoni, ushauri na maelekezo yote waliyoyatoa ili kuboresha utendaji kazi wa Ofisi hiyo pamoja na taasisi zake.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Bw. Sephania Solomon amesema fedha za ujenzi wa mradi wa Makazi kwa Watumishi wa Umma eneo la Njedengwa utakamilishwa kwa wakati k**a ilivyopangwa kwa awamu hiyo ya kwanza ambapo zinatarajiwa kukamilika mwezi February 2027.

MHE. RIDHIWANI AWAASA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA AWALI YA UCHUNGUZI KULITUMIKIA TAIFA KATIKA MISINGI YA UADILIFU NA UZALEND...
08/10/2026

MHE. RIDHIWANI AWAASA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA AWALI YA UCHUNGUZI KULITUMIKIA TAIFA KATIKA MISINGI YA UADILIFU NA UZALENDO
Veronica Mwafisi-Moshi
Tarehe 08 Oktoba, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wanaofanya mafunzo ya awali ya Uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa mstari wa mbele kulinda heshima ya chombo hicho nyeti na hatimaye watakapotoka hapo wawe tayari kulitumikia Taifa katika misingi ya maadili na uzalendo.

Mhe. Kikwete amesema hayo leo tarehe 8 Oktoba, 2026 wakati akifungua mafunzo ya awali ya Uchunguzi kwa vijana hao yanayofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania-Moshi.

“Tambueni kwamba, TAKUKURU ni chombo nyeti sana na cha kiuchunguzi kinachosimamia maadili, hivyo mna wajibu wa kuhakikisha mnakuwa mstari wa mbele kulinda heshima yake,” amesisitiza.

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa Mafunzo hayo ya awali ya Uchunguzi katika kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa Uadilifu na Ueledi Mkubwa. “Hivyo ni matarajio yangu na ya Serikali kwa ujumla kuwa, mtatilia maanani na kwa uzito unaotakiwa mafunzo haya, ili mkitoka hapa mkawe mabalozi wema wa TAKUKURU katika vituo mtakavyopangiwa kwenda kufanya kazi” ameongeza.

Amewasisitiza kufuata miongozo, maelekezo pamoja na taratibu zote zitakazotolewa wakati wote watakapokuwa katika mafunzo pamoja na kuzingatia kila wanachofundishwa kwa umakini mkubwa kwakuwa ndicho kitakachoamua hatma ya ajira ya kila mmoja wao ndani ya TAKUKURU.

Waziri Kikwete amewapongeza vijana hao kwa kufanikiwa kuitwa katika hatua hiyo ya mwisho ya Mchakato wa Ajira wa Taasisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa sana.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akiwasilisha taarifa ya utendaji wa TAKUKURU alisema mafunzo hayo ni sharti la kimuundo, hivyo kila anayeajiriwa TAKUKURU ni lazima ashiriki kwani yanawasaidia kupata ujuzi na utalaam wa kuzuia na kupambana na rushwa.

Amesema mafunzo hayo yalianza tarehe 19 Septemba 2026 na yatafanyika kwa muda wa miezi mitano ambapo yataendeshwa kwa njia ya vitendo na nadharia ikiwemo kufundishwa suala la maadili katika Utumishi wa Umma na ajira itatolewa baada ya kuhitimu na kufaulu mitihani itakayotolewa wakati wa mafunzo.

WAZIRI KIKWETE AWASILI SHULE YA POLISI TANZANIA MOSHI KUFUNGUA MAFUNZO YA AWALI YA UCHUNGUZI YA TAKUKURU
08/10/2026

WAZIRI KIKWETE AWASILI SHULE YA POLISI TANZANIA MOSHI KUFUNGUA MAFUNZO YA AWALI YA UCHUNGUZI YA TAKUKURU

WAZIRI KIKWETE AHITIMISHA MICHEZO YA SHIMIWI 2026, AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJAZA PEPMIS NA KUSIMAMIA MIFUMO YA UTENDA...
08/10/2026

WAZIRI KIKWETE AHITIMISHA MICHEZO YA SHIMIWI 2026, AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUJAZA PEPMIS NA KUSIMAMIA MIFUMO YA UTENDAJI KAZI

Na. Veronica Mwafisi-Moshi
07 Oktoba, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Watumishi wa Umma waliokuwa katika michezo ya SHIMIWI watakaporudi katika maeneo yao ya kazi, kufanya kazi kwa kusimamia mifumo ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali waliyokasimiwa ikiwemo ujazaji wa Mfumo wa Upimaji wa Utendaji kazi (PEPMIS).

Waziri Kikwete amezungumza hayo leo tarehe 07 Oktoba, 2026 wakati akihitimisha rasmi michezo ya SHIMIWI iliyofanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro.

“Nitoe wito kwenu watumishi wenzangu, leo tunapohitimisha rasmi michezo hii ya SHIMIWI, mtakaporudi katika maeneo yenu ya kazi hakikisheni mnasimamia Mifumo ya utekelezaji wa majukumu yenu ikiwemo ujazaji wa PEPMIS,” amesema Mhe. Kikwete

Waziri Kikwete amesema, taasisi zote za Serikali zina utaratibu mzuri wa kumpima kila mtumishi kiutendaji hivyo, mafanikio ya mtu mmoja mmoja, Idara na taasisi kwa ujumla yatasaidia kujua utendaji wa Serikali nzima.

Ameongeza kuwa, ni vema kujenga ushirikiano kwa washiriki wa michezo hiyo ya SHIMIWI ambao utawasaidia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika maeneo yao ya kazi.

“Mkusanyiko huu mkubwa wa Watumishi wa Umma unatusaidia kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali pamoja na kujenga ushirikiano utakaoleta mafanikio kwenye maeneo yenu ya kazi,” ameongeza Mhe. Kikwete

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesisitiza suala la usimamizi wa Rasilimalifedha kwa Viongozi wa Klabu mbalimbali na kutaka kila ofisi kutenga bajeti kwa ajili ya mipango ya mwaka unaofuata.
Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Ridhiwani amesema kutokana na Kaulimbiu ya SHIMIWI 2026, inayosema Watumishi Tupo Tayari kwa AFCON 2027, kila mtumishi katika sekta aliyopo ahakikishe anaunga mkono mashindano hayo kwa ustawi wa Taifa letu.

MADAI YA FIDIA NI USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU SI FADHILA : KATIBU MKUU MKOMINa. Antonia Mbwambo – DodomaTarehe 7 Oktoba,...
07/10/2026

MADAI YA FIDIA NI USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU SI FADHILA : KATIBU MKUU MKOMI

Na. Antonia Mbwambo – Dodoma
Tarehe 7 Oktoba, 2026

Uzembe na ucheleweshaji wa taarifa unaofanywa na baadhi ya Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini unaathiri mchakato wa kushughulikia madai ya fidia kwa mfanyakazi wakati anapopata ajali, ugonjwa au kifo anapokuwa katika utekelezaji wa makumu ya kikazi.

Maneno hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi Oktoba 7, 2026 wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Wahasibu wa Wizara, Taasisi za Umma zilizopo Dodoma na Wilaya zote za Mkoa Dodoma kuhusu taratibu za kuwasilisha na kushughulikia madai ya fidia kwa wafanyakazi yaliyofanyika katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Bw. Mkomi alisema kuwa hapendi kuona mfanyakazi kwa bahati mbaya anapata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi lakini kutokana na kutokuwepo kwa taarifa sahihi, nyaraka muhimu au uelewa wa taratibu, anashindwa kupata haki yake kwa wakati.

“Mafunzo haya ni muhimu kwenu Maafisa Rasilimaliwatu kwa kuwa ndio kiungo kati ya mwajiri, mfanyakazi na mifumo mbalimbali inayohusika na usimamizi wa rasilimaliwatu, ninaamini baada ya mafunzo haya mtakuwa na uelewa wa hatua za kuchukua pale mfanyakazi anapopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi au anapofariki kutokana na mazingira yanayohusiana na kazi na kuharakisha upatikanaji wa fidia” alisema Bw. Mkomi.

Aliongeza kuwa, kuwasilisha taarifa sahihi, zenye ukamilifu na kwa wakati ni jambo muhimu katika mchakato wa fidia. Hivyo, mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanagusa moja kwa moja ustawi wa watumishi, usimamizi wa rasilimaliwatu, uwajibikaji wa mwajiri na utekelezaji wa haki za wafanyakazi.

Bw. Mkomi alisisitiza kuwa Taasisi zote za Umma ambazo kwa mujibu wa taratibu ni waajiri, zina wajibu wa kuhakikisha zinatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazohusu fidia kwa wafanyakazi.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni chombo kinachohakikisha wafanyakazi wanaopata madhara mathalani ajali au ugonjwa uliosababishwa na kazi wanapata fidia na huduma stahiki kwa mujibu wa sheria. Vilevile mfuko unaweka ulinzi wa mfanyakazi na wategemezi wake, uzuiaji wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, pamoja na wajibu wa mwajiri katika kumlinda mfanyakazi

Address

670
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Rais-UTUMISHI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Rais-UTUMISHI:

Shortcuts

Share

Category