WCF Tanzania

Call Directions Website Contact the organization

WCF Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from WCF Tanzania, Government Organization, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Jengo la Kambarage, Ghorofa ya Tatu, 1 Barabara ya Kambarage, S. L. P 329, 41101 Dodoma, Dodoma.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263] kwa lengo la kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi.

TANZIAOfisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus
07/10/2026

TANZIA

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus

Maafisa Rasilimali Watu nchini wametakiwa kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyakazi wanaowasimamia na taasisi za hifad...
07/10/2026

Maafisa Rasilimali Watu nchini wametakiwa kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyakazi wanaowasimamia na taasisi za hifadhi ya jamii, ikiwemo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki na stahiki zao kwa wakati wanapopatwa na ajali, ugonjwa au kifo kutokana na kazi na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kupata pensheni zao kwa wakati pale wanapostaafu.

Wito huo umetolewa Oktoba 7, 2026, jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais–Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, wakati akifungua mafunzo kuhusu majukumu ya WCF na taratibu za madai ya fidia kwa Maafisa Rasilimali Watu na Wahasibu kutoka Taasisi za Umma za Mkoa wa Dodoma. Mafunzo hayo yaliratibiwa kwa ushirikiano kati ya WCF na PSSSF, ambapo washiriki walipata elimu kuhusu masuala ya pensheni na fidia kwa wafanyakazi.

Mkomi alisema falsafa ya Serikali ya awamu ya sita ya “Kazi na Utu” inapaswa kuonekana katika namna Maafisa Rasilimali Watu wanavyotekeleza majukumu yao, kwa kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao bila vikwazo visivyo vya lazima.

05/10/2026

Ushuhuda wa mnufaika wa WCF

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News




Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, Karibu Tukuhudumie Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura...
04/10/2026

Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, Karibu Tukuhudumie



Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus




02/10/2026

Sangu: DIRA 2050 inachangiwa na Uwekezaji wa Kimkakati.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amepongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana katika ujenzi wa miradi ya kimkakati ambayo imekuwa na tija katika kukuza uchumi kwa maendeleo ya Taifa.

Mhe. Sangu ameyasema hayo leo, Oktoba 2, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ajili ya kushirikiana katika uwekezaji wa ujenzi wa Ukumbi wa mikutano na hoteli katika eneo la Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete mjini Morogoro.

Waziri sangu amesema uwekezaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ambayo imekuwa ikizitaka taasisi za umma kuzingatia matumizi yenye tija ya rasilimali za umma na uwekezaji unaozalisha thamani kwa Taifa. “Kwa mantiki hiyo, ushirikiano kati ya WCF na TRC unaonesha namna Taasisi za Serikali zinavyoweza kutumia nguvu na uwezo wao kwa pamoja ili kuendeleza miradi yenye manufaa mapana kwa Taifa,” alisema Mhe. Waziri Sangu.

Aidha, Waziri Sangu aliipongeza WCF kwa uamuzi wa kubuni mradi huo k**a sehemu ya mikakati ya kuhakikisha Mfuko unakuwa na rasilimali za kuufanya kuwa himilivu. “Kwa upande wa WCF, uwekezaji wenye tija ni sehemu muhimu ya kuimarisha uendelevu wa kifedha wa Mfuko ili uweze kuendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kutoa fidia kwa wafanyakazi na wategemezi wao pale wanapopata madhara yatokanayo na ajali au magonjwa yanayohusiana na kazi. Kwa hiyo, uwekezaji huu unatakiwa kuangaliwa kwa mtazamo mpana wa kulinda thamani ya rasilimali za Mfuko na kuongeza uwezo wake wa kutekeleza wajibu wake kwa muda mrefu,” alisisitiza Mhe. Waziri Sangu.

Sangu: DIRA 2050 inachangiwa na Uwekezaji wa Kimkakati. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano,...
02/10/2026

Sangu: DIRA 2050 inachangiwa na Uwekezaji wa Kimkakati.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amepongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana katika ujenzi wa miradi ya kimkakati ambayo imekuwa na tija katika kukuza uchumi kwa maendeleo ya Taifa.

Mhe. Sangu ameyasema hayo leo, Oktoba 2, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ajili ya kushirikiana katika uwekezaji wa ujenzi wa Ukumbi wa mikutano na hoteli katika eneo la Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete mjini Morogoro.

Waziri sangu amesema uwekezaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ambayo imekuwa ikizitaka taasisi za umma kuzingatia matumizi yenye tija ya rasilimali za umma na uwekezaji unaozalisha thamani kwa Taifa. “Kwa mantiki hiyo, ushirikiano kati ya WCF na TRC unaonesha namna Taasisi za Serikali zinavyoweza kutumia nguvu na uwezo wao kwa pamoja ili kuendeleza miradi yenye manufaa mapana kwa Taifa,” alisema Mhe. Waziri Sangu.

Kwa taarifa tembelea tovuti
www.wcf.go.tz

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Maelezo News Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Railways Corporation


02/10/2026

Mafunzo ya Madaktari kutoka Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar, Pwani, Morogoro na Dodoma kuhusu kutambua na kufanya tathmini ya wagonjwa yatokanayo na kazi.

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Maelezo News


WCF YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA TUGHE TAIFA, YATOA ELIMU KUHUSU HUDUMA ZA FIDIA KWA WAFANYAKAZIMfuko wa Fidia kwa Wafanyak...
01/10/2026

WCF YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA TUGHE TAIFA, YATOA ELIMU KUHUSU HUDUMA ZA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Taifa, uliofanyika katika Ukumbi wa Mabeyo, Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Mfuko wa kuwafikia wadau na kuongeza uelewa kuhusu huduma za fidia kwa wafanyakazi.

Katika mkutano huo, mwakilishi wa WCF aliwasilisha mada iliyolenga kuwajengea washiriki uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko, mafao yanayopatikana, pamoja na taratibu za kuwasilisha madai ya fidia pale mfanyakazi anapopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi, au anapofariki kutokana na kazi.

Elimu hiyo ni sehemu ya jitihada za WCF kuhakikisha wafanyakazi na wadau wanafahamu haki zao, huduma zinazopatikana na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupata huduma za fidia kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa TUGHE Taifa anayemaliza muda wake, Cde. Joel Kaminyoge, aliwasihi viongozi watakaochaguliwa kuwa waadilifu, kuzingatia maslahi ya chama na kuhakikisha wanawaunganisha wanachama wote.

“Kwa viongozi watakaochaguliwa leo katika nafasi zote kitaifa, mtambue kuwa aliyeshinda ni chama chetu cha TUGHE na si mtu binafsi. Mkaunganishe wanachama wote, muepuke makundi yaliyoundwa wakati wa kampeni, na mkawe kitu kimoja kwa maslahi ya chama,” alisema Cde. Joel Kaminyoge.

Kupitia ushiriki katika mikutano k**a hii, WCF inaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma za fidia, ili kuhakikisha wafanyakazi wanafahamu stahiki zao na namna ya kuzifikia.

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Tughe Tanzania


WCF YASHIRIKI C-CEOs FORUM 2026, KUCHANGIA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ...
30/09/2026

WCF YASHIRIKI C-CEOs FORUM 2026, KUCHANGIA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeshiriki katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Arusha.

Sambamba na kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt John Mduma amezungumza na wadau waliotembelea banda la WCF, akiwahimiza waajiri kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na wale ambao tayari wamejiunga kuendelea kutoa michango.

Aidha, amesisitiza waajiri kutoa taarifa kwa WCF pindi wafanyakazi wao wanapopata ajali au ugonjwa unaotokana na kazi, akieleza kuwa kwa sasa utaratibu wa kutoa taarifa umerahisishwa, ambapo taarifa zinaweza kuwasilishwa kwa njia ya mtandao.

Kupitia ushiriki wa kikao hicho maalum , WCF inaendelea kuwafikia wadau na kutoa elimu kuhusu majukumu na huduma za Mfuko, pamoja na umuhimu wa waajiri kutekeleza wajibu wao katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao za fidia kwa wakati pale ambapo watapatwa na madhila ya ajali,kifo au ugonjwa unaotokana na kazi na pia unaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga nguvu kazi yenye ulinzi na ustawi, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News


Address

Mkurugenzi Mkuu, Mfuko Wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), Jengo La Kambarage, Ghorofa Ya Tatu, 1 Barabara Ya Kambarage, S. L. P 329, 41101 Dodoma
Dodoma

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222926107

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WCF Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to WCF Tanzania:

Shortcuts

Share