Ministry of Water

Ministry of  Water

Share

Karibu: Maji ni hitaji la msingi na haki kwa binadamu wote. Tafadhali yathamini, kuongeza matumizi y

The Ministry of Water is mandated to formulate and monitor implementation of policies on rural and urban water services; water resources development; water infrastructure development; water sources protection and conservation; sanitation improvement; water laboratories; river basins development and management; water quality and pollution control; drilling and dam construction and rain water harves

Photos from Ministry of  Water's post 03/06/2026

Wadau wa Sekta ya Maji Wajadili Maendeleo ya Sekta

Wadau wa Sekta ya Maji nchini wamakutana kujadiliana maendeleo ya Sekta ya Maji.

Kikao kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ya Maji Bi. Rose Zacharia Ambrose akifungua kikao amesema Sekta ya Maji ndiyo nguzo muhimu katika kuhakikisha mipango iliyopangwa inakuwa endelevu na kutimia.

Amesema ni muhimu kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji na maendeleo yaliyofikiwa.

Bi. Rose amesema Wizara ya Maji inatambua uwepo wa changamoto ya kifedha katika kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ya utafiti wa vyanzo vya maji nchini na inatumia vyanzo mmbadala kufanikisha hilo.

Amewataka wadau wa Sekta ya Maji nchini kuandaa mkakati kufanikisha miradi ya maji.

Katika kikao hicho imeelezwa kuwa mojawapo ya changamoto zinazoikabili Sekta ya Maji ni pamoja na ongezeko la mahitaji ya huduma ya maji, mabadiliko ya tabianchi.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji, Bw. Robert Sunday amesema lengo la serikali ni kuhakikisha huduma ya ni yenye ubora kwa matumizi, na maji kuwa chanzo kikubwa cha kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili changamoto, mafanikio ya Sekta ya Maji na mpango mkakati ya kutekeleza malengo ya sekta kwa miaka ijayo Ili kuboresha huduma za maji nchini.

Photos from Ministry of  Water's post 03/06/2026

Wakazi wa Dodoma na viunga vyake, pamoja na mikoa jirani wakitumia fursa ya maonesho kuelekea siku ya mazingira kutembelea Banda la Wizara ya Maji na Taasisi zake katika katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Wananchi wanajionea kazi zinazofanywa na Wizara ya Maji ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati kote nchini

Banda la Wizara ya Maji lipo geti kuu la kuingia viwanja hivyo ikijumuisha Taasisi za DAWASA,DUWASA, RUWASA, Mfuko wa Taifa wa Maji na Bodi ya maji ya bonde la Wami-Ruvu. Hakuna kiingilio katika maonesho haya wananchi wote wanakaribishwa kupata majibu ya jambo lolote kuhusu Sekta ya Maji.

03/06/2026
03/06/2026

Dodoma, taswira ya kikao kati ya Wizara ya Maji na UNICEF

Photos from Ministry of  Water's post 03/06/2026

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa katika kikao kazi pamoja na menejimenti ya Wizara ya Maji, mahsusi katika kuhakikisha mkakati wa kuimarisha huduma ya majisafi kwa wananchi wote.

Photos from Ministry of  Water's post 03/06/2026

Tembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Maji na Taasisi zake katika maonesho kuelekea siku ya mazingira Duniani tarehe 5 Juni yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Karibu ujionee kazi zinazotekelezwa katika Sekta ya Maji ikiwamo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea sehemu mbalimbali nchini na hatua za kuhifadhi na kuendeleza vyanzo vya maji

Banda la Wizara ya Maji lipo geti kuu, Banda la kwanza ambapo utakutana na taasisi ikiwamo DUWASA, DAWASA, RUWASA, Mfuko wa Taifa wa Maji na Bodi ya Maji ya bonde la Wami-Ruvu

Photos from Ministry of  Water's post 03/06/2026

UTEUZI

03/06/2026

UNICEF Hails Tanzania’s Remarkable Progress in Water and Sanitation

The United Nations Children's Fund (UNICEF) has commended Tanzania for achieving significant progress in the provision of water and sanitation services, attributing the success to sustained government investment and commitment to improving the wellbeing of its citizens.

The praise was delivered by UNICEF Representative in Tanzania, Ms Elke Wisch, during a meeting with the Minister for Water, Hon. Jumaa Aweso (MP) at the Ministry of Water offices in Mtumba, Dodoma.

The discussions focused on reviewing the achievements of the long-standing partnership between the Government and UNICEF, while also exploring new areas of cooperation aimed at advancing the country’s water sector.

During the meeting, the two sides agreed to strengthen collaboration in Water, Sanitation and Hygiene (WASH) programmes to enhance access to safe and clean water, improve sanitation services, and promote public health across the country. They also discussed strategies to increase the effectiveness of ongoing WASH projects and interventions.

Hon. Aweso described UNICEF as one of the Ministry’s most reliable and strategic development partners, highlighting the organisation’s contribution to improving water and sanitation services nationwide.

“Through the Water Sector Development Programme and other initiatives, UNICEF has contributed approximately $11.5 million over the past three years towards strengthening water services, sanitation and community health in Tanzania,” he said.

For her part, Ms Wisch applauded Tanzania’s achievements in the sector, noting that continued government investment had positioned the country among Africa’s top performers in water and sanitation development.

She said Tanzania’s progress serves as an example of how sustained investment and effective partnerships can transform essential public services and improve the quality of life for millions of people.
Ms Wisch reaffirmed UNICEF’s commitment to supporting the government in sustaining and expanding these gains to ensure that all Tanzanians have access to safe water and improved sanitation facilities.

Photos from Ministry of  Water's post 02/06/2026

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), akiwaaga Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Elke Wisch, pamoja na ujumbe wake mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja kilichofanyika Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma.

Kikao hicho kimejadili kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na UNICEF katika sekta ya maji, usafi wa mazingira na afya (WASH), pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuendeleza upatikanaji wa huduma bora za maji safi na salama kwa wananchi. Ushirikiano huo unaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya maji na ustawi wa jamii nchini.

Photos from Ministry of  Water's post 02/06/2026

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), akiongozana na Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Elke Wisch, pamoja na ujumbe wake, wakati wakiondoka eneo la kikao kilichofanyika Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma.

Katika mazungumzo, viongozi hao wamedilishana mawazo kuhusu hatua za kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na UNICEF katika kuboresha huduma za maji, usafi wa mazingira na afya (WASH), kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na huduma bora na endelevu nchini.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


456
Dodoma