02/06/2026
Unaweza kufuatilia matangazo mbashara kupitia channel ya youtube ya Ofisi ya Makamu wa Rais
Ukurasa rasmi wa Facebook wa Ofisi ya Makamu wa Rais
02/06/2026
Unaweza kufuatilia matangazo mbashara kupitia channel ya youtube ya Ofisi ya Makamu wa Rais
02/06/2026
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Bi. Tone Tinnes. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam Juni mosi, 2026.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Muyungi ameishukuru Serikali ya Norway kwa ushirikiano wa muda mrefu waliouonesha kwa Serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali na kwa nyakati zote.
Alisema kuwa Serikali chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa nchi hiyo katika usimamizi mwa mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Dkt. Muyungi alitaja moja ya alama ya mchango wa Norway ni kuanzishwa kwa Kituo cha Study za Mabadiliko ya Tabianchi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kunzishwa kwa Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
Kwa upande wake Balozi Mhe. Tonnes alisema kuwa Norway itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika masua mbalimbali yahusuyo sekta ya hifadhi ya mazingira.
Miongoni mwa maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ni pamoja na Programu ya kuijengea uwezo NCMC ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuwafikia wadau wengi zaidi.
Balozi Tinnes alisema pia Serikali ya nchi yake iko tayari kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya Mheshimiwa Rais ya Nishati Safi ya Kupikia ili kufikia lengo asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi yabkupikia ifikapo mwaka 2034.
Halikadhalika, katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na uzalishaji wa gesijoto, Norway itaendeleza ushirikiana na Tanzania katika teknolojia na matumizi ya magari ya umeme.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akilfungua maonesho ya mazingira katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026.
01/06/2026
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa ametoa wito kwa wadau kuendelea kuwekeza katika ubunifu wa teknolojia ili kuimarisha juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ametoa wito huo wakati akifungua maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani katika Viwanja vya Jakaya
Kikwete jijini Dodoma leo Juni mosi, 2026.
Mhe. Kwagilwa alisema pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi, Watanzania wameonesha utayari wa kushiriki katika mapambano changamoto hizo kwa kufanya ubunifu wa teknolojia, matumizi ya sayansi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira.
Alisema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha usimamizi wa mazingira kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazosaidia kuongeza ufanisi katika uhifadhi wa rasilimali za asili na kukabiliana na changamoto za tabianchi.
Aidha, Naibu Waziri huyo alieleza kuwa nguzo ya tatu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeweka msisitizo katika uhifadhi wa mazingira na kuongeza uwezo wa taifa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Halikadhalika, aliipongeza Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu muswada wa Sheria mpya ya Mazingira kuwasilishwa bungeni ambayo itawezesha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa Mamlaka kamili, hatua itakayoongeza chachu katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
Hivyo, Mhe. Kwagilwa aliwasihi wananchi, taasisi na wadau wa maendeleo kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira na kusisitiza kulinda na kuhifadhi mazingira.
Awali akizungumza, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda alisema maonesho hayo yatahusisha wadau mbalimbali wa mazingira watakaoonesha teknolojia, ubunifu na elimu.
Alisema maonesho hayo yatasaidia vilevile kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kutumia rasilimali za asili kwa njia endelevu.
Alisema wananchi watajifunza kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kukabiliana nazo.
Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu 'Dira 2050;Tuwajibike kukijanisha Tanzania' na kilele kinatarajiwa kufanyika Juni 05, 2026.
01/06/2026
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akikagua mabanda ya maonesho katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026.
01/06/2026
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa leo Juni mosi, 2026, akiwasili katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kukagua mabanda ya maonesho ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 05, 2026.
31/05/2026
29/05/2026
Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha usimamizi wa mazingira ikiwemo kuboresha sera na sheria za udhibiti wa mazingira nchi.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) uliofanyika katika Ukumbi wa Kiimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema katika kuhakikisha mazingira bora na salama kwa wananchi Serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi, na kuimarisha utendaji kazi wa NEMC kwa kuanzisha mchakato utakaoibadilisha kuwa Mamlaka kamili ya Mazingira.
Mhe. Hemed amefahamisha kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na athari za matumizi ya nishati isiyo safi kwa kuendeleza mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034, hatua itakayolinda afya, mazingira, na kuboresha maisha ya wananchi.
Aidha, Mhe. Hemed amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mipango ya Kitaifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo utekelezaji wa mpango wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza uwezo wa Taifa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za maji, kilimo, afya, nishati na miundombinu.
29/05/2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiweka mchanga na shada la maua katika kaburi la Bi. Suzana Ngolo Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, wakati wa mazishi yaliyofanyika Kilimani Wilayani Chato leo tarehe 29 Mei 2026.
29/05/2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli, ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yaliyofanyika Kilimani, Chato mkoani Geita.
Akitoa salamu za rambirambi mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya kumuombea Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli, Makamu wa Rais amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameguswa na msiba huo na anatoa salamu za pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
Makamu wa Rais amewasihi Watanzania kumtumia marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli k**a kielelezo cha malezi ya watoto, malezi ya maadili na uzalendo kwa kuwafanya watoto kutanguliza maslahi ya Taifa mbele na kuwa tayari kutumikia Taifa kwa nafasi yeyote wanayopewa. Ameongeza kwamba namna bora ya kumuenzi marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli ni kuiga mfano wa malezi bora na mema ya watoto.
Amesema msiba wa Bi. Suzana Ngolo Magufuli unafundisha kuwa alikuwa sehemu kuu ya malezi ya Hayati Rais Dkt. John Magufuli ambaye alitoa mchango mkubwa katika utumishi wa nchi yetu. Amesema kitendo cha wananchi wengi kutoa salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii ni ishara ya Watanzania kuguswa na Maisha ya Hayati Magufuli ambaye alitumikia nchi kwa uzalendo wa hali ya juu.
Halikadhilika, Makamu wa Rais amemuelezea hayati Dkt. John Pombe Magufuli, k**a kiongozi aliyejitoa kutetea nchi pamoja na kuwa na utashi wa kujua wajibu wa kulea watu wengine na kuwafanya kuwa Viongozi wa Taifa baadaye. Ameongeza kwamba kujitoa na kufanya matendo mema kwaajili ya wengine ni matunda ya baadaye kwa mtu na familia yake.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya familia Bw. Simon Nyahinga amesema familia hiyo inamshukuru kwa dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa, huruma, faraja na mchango wake mkubwa aliyouonesha wakati wa kuugua kwa Bi Suzana Magufuli. Amesema tangu kufariki kwa Hayati Dkt. John Magufuli, Rais Samia ameendelea kusimama pamoja na familia katika kipindi chote cha matibabu.
Aidha, amewashukuru Viongozi wakuu wa Kitaifa na Viongozi wakuu wastaafu kwa msaada waliyotoa na kuifariji familia wakati wa matibabu ya Bi Suzana Magufuli pamoja na wakati wa msiba. Pia ameishukuru Serikali kwa kubeba jukumu ya kugharamia shughuli zote za msiba huo.
Ibada ya kumuaga na kumuombea Marehemu Bi. Suzana Magufuli imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande na kuhudhuriwa na Maaskofu mbalimbali, Mapadre, Viongozi mbalimbali, Viongozi Wakuu wastaafu, pamoja na wananchi mbalimbali.
| Monday | 08:00 - 15:30 |
| Tuesday | 08:00 - 15:30 |
| Wednesday | 08:00 - 15:30 |
| Thursday | 08:00 - 15:30 |
| Friday | 08:00 - 15:30 |