Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu -CDA Dodoma

Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu -CDA Dodoma

Share

MJI MKUU DODOMA

01/02/2017

Nukuu za Hayati baba wa Taifa wakati wa kuhamisha Makao Makuu ya nchi.

"Makao Makuu ya Nchi ni kitu cha kudumu .K**a tukiamua kwamba Makao Makuu yakabaki Dar-es-salaam au yahamie Dodoma tutakuwa tunata uamuzi wa kudumu. Kwa hiyo sababu zitakazotufanya tukate shauri lazima ziwe zakudumu. Tusitumie njia ya mkato kutoa uamuzi wa kudumu.

Photos from Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu -CDA Dodoma's post 22/12/2016

Ziara ya Wataalamu wa kupitia mpango kabambe wa mji wa Dodoma Beijing-China

Photos 22/12/2016

Ziara ya k**ati ya wataalamu ya kupitia mpango kabambe wa mji wa Dodoma Beijing-China

05/10/2016

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea maeneo yaliyopendekezwa kujengwa mji wa Serikali na kujiridhisha kuwa yanatosha kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu.
Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatatu, Oktoba 3, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ukubwa wa maeneo hayo ambayo pia yanatosha kujenga miundombinu inayohitajika.

Katika ziara hiyo Waziri mkuu ameridhishwa na maeneo yaliyotengwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu(CDA) yanayofaa kuwekeza kwa ujenzi wa miundombinu ya biashara k**a masoko na hoteli na viwanda na tumejirishisha kuwepo kwa ardhi ya kutosha.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amekaribisha wawekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za watumishi ambao watajenga nyumba za makazi na kuziuza kwa watumishi wa umma na wananchi.
Aidha amebainisha kuwa muwekezaji atakayekuwa tayari awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye ndiye anayeratibu shughuli hiyo huku akikaribisha wawekezaji wa ujenzi wa hoteli za kitalii na kawaida kwa kuwa wanatarajia kupata wageni wengi.

“Tumekaribisha pia wawekezaji wa ujenzi wa viwanda tumeiona ardhi inatosha na uzalishaji ni mkubwa Kanda ya kati kwa mkoa wa Dodoma wenyewe, Manyara, Singida na mikoa ya jirani ya Iringa na Morogoro inaweza kunufaika na fursa hizo,” amesema.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Mhandisi Paskasi Muragili alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambayo Waziri Mkuu alimeyatembelea ni Chigongwe lenye hekta 11,297, Kikombo hekta 13,275 na Nyankali hekta 2,370.

05/10/2016

WAKAZI WA DODOMA WAONDOLEWA HOFU YA BEI YA VIWANJA

Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskasi Muragili, amewatoa hofu wakazi wa Dodoma kwa kusema kuwa ardhi mjini hapa itauzwa kwa bei ya kawaida ili watu wengi waweze kumiliki viwanja.
Ameyasema hayo alipokuwa akijibu hoja za waandishi wa habari kuhusu kauli za wananchi kudai kuwa bei ya viwanja Dodoma itapanda kutokana na ujio wa Makao Makuu na kusababisha wananchi maskini kutoweza kumiliki viwanja hivyo.
Muragili amesema kuwa viwanja hivyo havitapandishwa bei kwani kwa sasa Mamlaka inaua mita moja ya kiwanja cha makazi kwa Sh 5,500 hadi Sh 10,000 katika maeneo ambayo kitaalamu tunayaita ‘medium density’.“Viwanja kwa ajili ya uwekezaji mkubwa mita moja kwa Sh 13,300 na maeneo hayo kitaalamu tunayaita ‘low density’.
Amesema pamoja na uwepo wa mahitaji makubwa, nasema ardhi ipo ya kutosha, yaani hata k**a watakuja wananchi wote wa Dar es Salaam, watapata ardhi ya kutosha.“Narudia tena, ardhi ipo ya kutosha, hata k**a watu watakuja baada ya miaka 30, wataipata kwa sababu hata Mwalimu Nyerere alipoamua Dodoma iwe makao makuu, alijua kuna ardhi ya kutosha kwa idadi yoyote ya watu,”
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa CDA Bw. askasi Muragili ametoa angalizo kwa wanaohitaji kununua viwanja mjini Dodoma na kusema watatakiwa kupitia CDA kwa kuwa ndiko vinakopatikana.
“Viwanja tusinunue kienyeji, tufuate taratibu kwani najua watatokea wapigaji wa dili watakaowaumiza watu. Nawaombeni mje ofisini kwetu, k**a mnataka viwanja mtapata tu kwa kufuata utaratibu,’’ alisema
Amewaomba wananchi hasa wanaotoka nje ya Mkoa wa Dodoma kufuata sheria na taratibu za Mipango Miji taofauti na hapo Mamlaka haitasita kubomoa maeneo yamejengwa kiholela
Akizungumia kuhusu suala la uwekeaji Dodoma Bw. Muragili amesema tayari Mamlaka imetenga maeneo ya uwekezaji la Njedengwa kwa ajili ya kujenga mahoteli makubwa na nyumba mbalimbali za kupanga.
“Kuonyesha kwamba tulijipanga mapema katika eneo la uwekezaji, kule Ndejengwa miundombinu iliishafika mapema, kwani kuna maji, umeme pamoja na barabara za lami,” alisema Muragili.

Untitled album 05/10/2016
20/09/2016

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Bi. Christine Mademe amewaagiza Manispaa ya Dodoma na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu kushirikiana katika kutatua kero za wananchi hasa katika suala zima la ardhi.

Alitoa maagizo hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo juu ya uhusiano kati ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na Maadili ya uongozi kwa Madiwani yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Manispaa alisema migogoro ya ardhi haiwezi kwisha bila kujenga uhusiano imara kati ya Manispaa na CDA

Bi. Mademe alisema " Dodoma kuna migogoro mingi ya ardhi, migogoro hiyo inatakiwa kumalizwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na Manispaa ya Dodoma.

Alisema Madiwani wana wajibu mkubwa wa kutatua kero za wananchi hasa zinazohusu ardhi ili kujenga mahusiano mazuri kati ya Manispaa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu.

01/08/2016

WIZARA ZOTE MGUU SAWA DODOMA

Baada ya Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa kutamka kuwa atahamia Dodoma Septemba atahamia Dodoma mwaka huu , Wizara zote za serikali zimetuma maombi kwa ajili ya kuoneshwa maeneo watakapojenga ofisi zao.

Katika hatua nyingine , sekta binafsi mkoani Dodoma imejigamba kujipanga vizuri kuhakikisha inatumia fursa ya masoko kujiimarisha kibiashara kutokana na matarajio ya makao makuu kuingiza wabia wengi wa kibiasharakutoka ndani na nje ya nchi.

Akihojiwa hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA), Paskas Muragili alisema katika harakati za serikali kuhamia Dodoma Mamlaka hiyo imepokea barua za maombi ya wizara zote wakitaka kuoneshwa maeneo yao.

Alisema kuwa hayo yamefanyika ikiwa ni mwitikio wa kauli ya Rais John Magufuli ya serikali kuhamia Dodoma , sambamba na Waziri Mkuu Majaliwa kuitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha wanatenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu

Aliseama CDA imeshapokea barua za maombi kutoka Wizara zote za Serikali zikitaka kuoneshwa maeneo yao na kazi ambayo tunaifanya kwa sasa ni kushughulikia barua hizo na kuweza kujua jinsi gani tunajipanga kulingana na mahitaji ya Wizara hizo.

Aliseama kuwa Mamlaka hiyo inao mpango kabambe wa kuhakikisha Mji wa Dodoma unakuwa katika mpangilio mzuri na usiokuwa na msongamano. Alisema katika mpango huo zipo barabara za kutosha ambazo kwa kwa sasa haziwezekani kwa macho.

22/06/2016

NYARAKA ZINAZOHITAJIKA WAKATI WA KUBADILI UMILIKI WA VIWANJA

1. Nyaraka halisi za umiliki wa kiwanja
2. Nakala za nyaraka hizo
3. Mkataba wa kuhamisha miliki ( Deed of transfer - land form No.35) nakala halisi mbili na kivuli kimoja.
Ikiwa kiwanja kina hati iliyosajiliwa , hati itawasilishwa na kubaki ofisini.

09/06/2016

NYARAKA ZINAZOHITAJIKA KATIKA KUANDAA HATI.

1. Barua ya Toleo ( Letter of Offer)

2. Stakabadhi za malipo ya umilikishwaji

3. Stakabadhi ya malipo ya kodi ya ardhi ya sasa

4. Barua ya Kupewa Kiwanja

5. Fomu ya maombi ya Kiwanja.

Kabla ya kuanza ujenzi, unapaswa kutoa taarifa kwa wakaguzi wa Majengo wa Mamlaka (CDA), ili waweze kukagua upimaji ( setting out) wa jengo hilo.

Hakikisha unakaguliwa na wakaguzi wa majengo toka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu kwa kila hatua ya ujenzi unaofanyika.

HATUA ZA KUFUATA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI HADI

03/06/2016

Kwa nini Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imekuwa ikitwaa ardhi ambayo wananchi wamekuwa wakiimiliki hata kabla ya kuanzishwa kwake. Moja ya maswali ambayo wananchi wamekuwa wakihoji.

CDA ni Mamlaka inayotoa huduma zake kwa kafuata sheria , kanuni na matangazo ya Serikali (GN) yanayotolewa mara kwa mara. Sheria hizi ni sheria ya ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, sheria ya utwaaji ardhi 1967, sheria ya usajili ardhi sura 334,sheria ya usajili wa nyaraka Sura 117 sheria ya upimaji ardhi sura 324pamoja na marekebisho mbalimbali.

Zoezi la utwaaji wa ardhi hufanyika kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu zifuatazo: Kwanza kulitambua eneo la mpango kupitia wataalam wa Mipango Miji, ikifuatiwa na ushirikishwaji wa viongozi na wananchi wa eneo husika kuhusu mpango uliopo. Wananchi wakikubaliana na mpango utekelezaji hufuata kwa kutumia sheria ya ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 ambayo inatambua ardhi ni mali yenye dhamani na imetoa maelekezo mali zitakazostahili malipo ya fidia pamoja na posho kwa mwananchi ambaye ardhi yake inatwaliwa.

Kifungu Na. 3 (1g) cha sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inaelekeza fidia italipwa kwa mali zote zilizopo katika eneo husika , zitalipwa kwa dhamani linganifu kutegemea gharama ya soko katika muda wa utwaaji mali hizo ambazo ni nyumba, ardhi na mazao, Posho ya usumbufu, posho ya Usafiri kwa wamiliki wa nyumba pekee, Posho ya pango kwa wenye nyumba ya kuishi( inayoishi mtu) na posho ya hasara kwa wamiliki wa majengo ya biashara zinazoendelea wakati wa utwaaji wa eneo. Mifano hai ya maeneo yaliyotwaliwa ya utaratibu huu ni Iyumbu,Miganga Mkalama na Mkonze.

Kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi hasa wale waliotwaliwa ardhi miaka ya nyuma kuwa ardhi ilitwaliwa pasipo kulipwa fidia. Kabla sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 haijapitishwa utwaaji wa ardhi ulikuwa ni rahisi kwa ardhi ilitambulika kuwa haina dhamani kwa mujibu wa sheria iliyokuwepo ambayo ni Land Ordinance ya mwaka 1923.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


913
Dodoma

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:00
Tuesday 08:00 - 15:00
Wednesday 08:00 - 15:00
Thursday 08:00 - 15:00
Friday 08:00 - 15:00
Saturday 00:00 - 23:00