Tanzania Insurance Regulatory Authority

Directions Website Contact the organization

Tanzania Insurance Regulatory Authority Official page of Tanzania Insurance Regulatory Authority

Only 9 Days Left! Join us on October 16, 2026, at TIRA Bima House, Njedengwa, Dodoma, for the Annual Insurance Market Pe...
06/10/2026

Only 9 Days Left! Join us on October 16, 2026, at TIRA Bima House, Njedengwa, Dodoma, for the Annual Insurance Market Performance Report Launch.

Theme: “Transforming the Insurance Sector for Economic Growth Towards Implementation of DIRA 2050.”

Stay tuned!

GAVANA TUTUBA AITAKA SEKTA YA BIMA KUBUNI BIDHAA ZINAZOKIDHI MAHITAJI YA SEKTA YA MADINIGavana wa Benki Kuu ya Tanzania ...
03/10/2026

GAVANA TUTUBA AITAKA SEKTA YA BIMA KUBUNI BIDHAA ZINAZOKIDHI MAHITAJI YA SEKTA YA MADINI

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, ametaka sekta ya bima kuendelea kubuni bidhaa na huduma zinazokidhi mahitaji halisi ya wadau wa sekta ya madini, hususan katika kukabiliana na vihatarishi vinavyotokana na shughuli za uchimbaji.

Meneja wa TIRA Kanda ya Ziwa Bw. Oyuke Phostine, alieleza kuhusu fursa zilizopo kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika Kanda ya Ziwa, zikiwemo biashara za mipakani na shughuli zinazohusiana na sekta ya madini.

Aidha, Bw. Oyuke alieleza utayari wa TIRA kuhusu utekelezwaji wa bima ya afya katika sekta ya madini, akieleza kuwa katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, TIRA imeanza mazungumzo na kampuni za madini ili kutafuta namna bora ya utekelezaji wake kwa kuzingatia mazingira na mahitaji ya sekta hiyo.

Kwa upande wake, Gavana Tutuba alisisitiza umuhimu wa kuwa na bima za maisha kwa wachimbaji wanaofanya kazi katika mashimo ya migodi kutokana na vihatarishi vinavyoweza kujitokeza katika shughuli zao ambazo huathiri moja kwa moja familia na wategemezi wao.

Gavana Tutuba pia ameeleza umuhimu wa kuendelea na mchakato wa kuwa na kanuni zitakazoweka matakwa ya kuwa na bima katika baadhi ya maeneo ya umma, ikiwemo masoko na maeneo mengine yenye mikusanyiko mikubwa ya watu. Alitolea mfano wa matukio ya moto yaliyotokea katika masoko mbalimbali nchini na kusababisha hasara.

KIJIJI CHA BIMA CHAWAUNGANISHA WANANCHI NA WATOA HUDUMA ZA BIMA GEITAKatika harakati za kutafuta fursa na kujifunza kuhu...
03/10/2026

KIJIJI CHA BIMA CHAWAUNGANISHA WANANCHI NA WATOA HUDUMA ZA BIMA GEITA

Katika harakati za kutafuta fursa na kujifunza kuhusu sekta ya madini, wananchi wanaoshiriki Maonesho ya Madini Geita wamepata fursa ya kupata elimu kuhusu umuhimu wa bima na namna ya kutumia huduma za bima katika kulinda maisha, mali na shughuli zao za kiuchumi.

Kupitia Kijiji cha Bima, TIRA Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) pamoja na kampuni za bima zinazofanya shughuli zake katika kanda hiyo, imeendelea kutoa elimu na uhamasishaji kwa wananchi kuhusu huduma za bima, haki za watumiaji wa bima na namna ya kupata msaada pale wanapokutana na changamoto zinazohusu huduma za bima.

Ushiriki huo umeifanya Kijiji cha Bima kuwa sehemu ya maonesho inayowakutanisha wananchi na wadau wa sekta ya bima kwa mazungumzo ya moja kwa moja, ambapo wananchi wamepata fursa ya kuuliza maswali, kufahamu aina mbalimbali za bima na kupata ufafanuzi kuhusu hatua za kuchukua katika kupata huduma na kushughulikia migogoro ya bima.

Maonesho hayo yameanza tarehe 22 Septemba 2026 na kumalizika tarehe 2 Oktoba 2026 katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.

TIRA YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI GEITAMamlaka ya Bima Tanzania imeeleza dhamira yake ya kuendelea ...
03/10/2026

TIRA YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI GEITA

Mamlaka ya Bima Tanzania imeeleza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Geita katika kutoa elimu ya bima kwa wananchi, hususan makundi yanayotumia vyombo vya usafiri barabarani.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Jerry Mwantuke, Afisa Takwimu Bima Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania alitambulisha wadau wa sekta ya bima Kanda ya Ziwa na kueleza uwepo wao mkoani humo umelenga kutoa elimu kwa wadau wa shughuli za madini na sekta ya usafirishaji kuhusu umuhimu wa bima.

Bw. Mwantuke alieleza kuwa TIRA ililenga kutoa elimu ya bima katika Stendi mabasi ya Geita ili kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuwawezesha kuelewa umuhimu wa bima, haki na wajibu wao pamoja na namna ya kunufaika na huduma za bima.

Kwa upande wake, Makanda wa Polisi Mkoa wa Geita SACP. Jongo aliwakaribisha wawakilishi wa TIRA na wadau wa Bima na kukubali ombi la kutoa elimu ya bima katika Stendi ya Geita. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika utoaji wa elimu hiyo, hususan kwa waendesha bodaboda na bajaji ambao ni miongoni mwa makundi yanayokabiliwa zaidi na changamoto za ajali za barabarani.

Kamanda SACP. Jongo pia alieleza kuhusu operesheni inayoratibiwa na ofisi yake kwa kushirikisha taasisi mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na taasisi nyingine, ikiwa na lengo la kuimarisha usalama barabarani na kuhakikisha sheria na taratibu zinazohusiana na usalama wa watumiaji wa barabara zinafuatwa. Hivyo, hii ni sehemu muhimu kwa TIRA kushiriki.

Kamanda SACP. Jongo aliishukuru TIRA kwa ushirikiano unaoendelea na ofisi yake. Alibainisha kuwa ushirikiano kati ya taasisi za serikali na wadau wa sekta ya bima ni muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu bima na kuchangia katika kuimarisha usalama wa barabarani mkoani Geita.

ELIMU YA BIMA YATOLEWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA NYANKUMBUMamalaka ya Usimamizi wa Bima TIRA kwa kushirikiana na w...
01/10/2026

ELIMU YA BIMA YATOLEWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA NYANKUMBU

Mamalaka ya Usimamizi wa Bima TIRA kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Bima wametoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu mjini Geita.

Akizungumza katika zoezi hilo, Bw. Jerry Mwantuke, Afisa Takwimu Bima Mwandamizi kutoka (TIRA), alieleza umuhimu wa bima katika kulinda watu, mali na shughuli mbalimbali dhidi ya vihatarishi vinavyoweza kutokea.

Pia alieleza nafasi ya TIRA katika kusimamia na kuendeleza sekta ya bima nchini, pamoja na nafasi ya Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima katika utatuzi wa migogoro ya kibima. Wanafunzi walijifunza namna mifumo ya usimamizi na utatuzi wa migogoro inavyofanya kazi.

Baada ya kupokea elimu hiyo, Bi. Khadija Kayanda, Mkuu wa Shule aliwahimiza wanafunzi kuendelea kujifunza kuhusu bima na kuwa mabalozi wa elimu hiyo katika familia na jamii inayowazunguka. Aliwataka wanafunzi kufikisha ujumbe walioupata kwa wazazi, ndugu na marafiki, huku wakieleza umuhimu wa kuwa na uelewa wa bidhaa mbalimbali za bima zinazopatikana nchini.

Aidha, wakiwakilisha kampuni mbalimbali za bima, walitoa elimu kuhusu bidhaa za bima zinazopatikana nchini ikiwa ni bima ya afya, bima za maisha, pamoja na bima za kawaida zinazolenga kulinda mali na shughuli mbalimbali, ikiwemo bima dhidi ya majanga ya moto.

30/09/2026
TIRA YANG’ARA; YATUNUKIWA TUZO YA MSHINDI WA PILI KWA MATUMIZI BORA YA FEDHA - TAASISI ZA UMMAMamlaka ya Usimamizi wa Bi...
28/09/2026

TIRA YANG’ARA; YATUNUKIWA TUZO YA MSHINDI WA PILI KWA MATUMIZI BORA YA FEDHA - TAASISI ZA UMMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) leo Septemba 28, 2026, imetunukiwa tuzo ya mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Umma zisizo za Kibiashara zinazofanya vizuri katika usimamizi na matumizi bora ya fedha (Best Financial Management Performance – Non-Commercial Entities).

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo A. Saqware, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum) kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), jijini Arusha.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo la kutambua Taasisi za Umma zinazofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya usimamizi na matumizi ya rasilimali za umma. Akieleza kuhusu kundi la Matumizi Bora ya Fedha, Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amesema tathmini hiyo imezingatia ufanisi katika matumizi na ukusanyaji wa mapato, pamoja na hatua za kupunguza utegemezi kwa Taasisi za Umma zisizo za Kibiashara.

Ameeleza zaidi kuwa Taasisi zilizofanya vizuri katika kundi hilo zimeonesha kuimarika kwa mapato, udhibiti wa matumizi, kupungua kwa utegemezi, pamoja na kuboreka kwa upatikanaji wa ziada na ukwasi, kwa kuzingatia taarifa za hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

WADAU WA SEKTA YA MADINI WAFIKIWA NA TIRAMamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeendelea kutoa elimu kwa wadau w...
28/09/2026

WADAU WA SEKTA YA MADINI WAFIKIWA NA TIRA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini kuhusu umuhimu wa kuwa na bima katika shughuli zao katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Septemba 27, 2026 Mgeni Rasmi na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, amesisitiza umuhimu wa wadau wa sekta ya madini kutumia fursa zinazopatikana kupitia maonesho hayo kujifunza teknolojia, huduma na mifumo mbalimbali inayoweza kuongeza usalama, tija na ufanisi katika shughuli za uchimbaji madini.

Kwa upande wa Meneja wa TIRA Kanda ya Ziwa, Bw. Oyuke Phostine, amesema bima ni suluhisho katika kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kukabiliana na madhara ya hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa shughuli zao, badala ya kubeba hasara hizo wenyewe pindi zinapotokea.

Bw. Oyuke ameeleza kuwa shughuli za madini zinakabiliwa na hatari mbalimbali zinazoweza kuathiri maisha ya watu, mali na mitaji, zikiwemo ajali za kazini, moto, mafuriko, wizi, uharibifu wa mitambo, majanga ya asili pamoja na madai ya dhima.

Kwa msingi huo, amesema wadau wanapaswa kupata uelewa sahihi kuhusu bidhaa za bima zinazopatikana, masharti yake, aina na maeneo yanayokingwa sambamba na taratibu za kuwasilisha madai, ili waweze kuchagua kinga inayolingana na mahitaji ya shughuli zao.

Ushiriki wa TIRA na wadau wake wote katika maonesho haya unaendelea kuwa sehemu ya jitihada za kuongeza uelewa wa matumizi ya bima miongoni mwa wadau wa madini, kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa shughuli zao na kuongeza ustahimilivu wa sekta dhidi ya vihatarishi vinavyoweza kusababisha hasara.

TIRA YASHIRIKI CEO’s FORUM 2026 ARUSHAMamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki Kikao Kazi cha Wenyeviti w...
28/09/2026

TIRA YASHIRIKI CEO’s FORUM 2026 ARUSHA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (CEO’s Forum 2026), kinachofanyika leo Septemba 28, 2026 katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) jijini humo.

Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo A. Saqware, anashiriki katika kikao hicho kinachowakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji, usimamizi na maendeleo ya taasisi za umma na ujumuishwaji wa wananchi katika maendeleo katika Utekelezaji wa Dira 2050.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, anatarajiwa kufungua rasmi kikao hicho kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.ikao hicho kinatarajiwa kuwakutanisha wawakilishi kutoka takribani Mashirika ya Umma 300 pamoja na washiriki zaidi ya 700.

Address

Dodoma
11104

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Insurance Regulatory Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Insurance Regulatory Authority:

Shortcuts

Share