Chama Cha Mapinduzi

Chama Cha Mapinduzi

Share

Ukurasa rasmi wa Chama Cha Mapinduzi. Chama Tawala Tanzania

15/05/2026

MUSOMA IMEITIKA โœ…

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 15/05/2026

MICHANGO MASHULENI IKOMESHWE- KIHONGOSI
MUSOMA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi ameelekeza suala la michango mashuleni likome, na kuhakikisha wananchi wanatendewa haki kwa kupata huduma kwa mujibu na maelekezo ya serikali ili kuepuka kutengeneza mazingira ya kuonekana wanaweka vikwazo kwa wananchi wao.

Kihongosi ameeleza hayo leo Aprili 14,2026 alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi katika viwanja vya Mkendo Musoma Mjini mkoani Mara, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika mkoa huo.

Kihongosi ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea changamoto ya mama mmoja ambaye hakujitambulisha kwa majina yake alidai kuwa na changamoto ya uwezo na kushindwa kusomesha watoto wake akieleza kuwa moja ya watoto hao yupo kidato cha nne lakini ameshindwa kwenda shule kwa sababu hana uwezo wa kumlipia fedha ya kambi ambayo ni zaidi ya Sh 600,000.

Baada ya kusikia Changamoto hiyo Kihongosi alimuita Afisa Elimu Sekondari wa Mkoa wa Mara, Aviti Malya ili kutoa ufafanuzi wa suala hilo alidai kuwa ni kweli kuna utaratibu huo lakini ni kwa wazazi wenye uwezo na kiasi kinachotakiwa kulipwa ni Sh 680,000 kwa ajili ya kulipia umeme, maji na mahitaji mengine muhimu wawapo kambini hapo.

Baada ya kusikiliza hilo Kihongosi alisema suala hilo bado ni changamoto na linaleta ukakasi kwa sababu k**a ni watoto wa darasa moja na ni masomo sawa, hakukuwa na ulazima wa kufanya hivyo na badala yake wangewaambia wazazi wachangie chakula ili kuwasaidia watoto hao kuliko kutoa kiasi hicho cha fedha.

โ€œKwanini hamkwenda na utaratibu wa kuchangia chakula na sio fedha labda
Mpeleke mahindi au maharage au mchele, wa sababu la Sh 600,000 haina tofauti na shuke binafsi na k**a serikali tunahubiri kwamba tunatoa elimu bila malipo sasa hoja k**a hii sioni uhalali wake mimi binafsi,โ€ amesema Kihongosi.

15/05/2026

๐—–๐—–๐—  ๐—›๐—”๐—œ๐—๐—”๐—ช๐—”๐—›๐—œ ๐—ž๐—จ๐—ž๐—ข๐—ฆ๐—˜๐—” ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐—”๐— ๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—”๐—ž๐—˜ ๐—Ÿ๐—”๐—ญ๐—œ๐— ๐—” ๐—ฌ๐—”๐—›๐—˜๐—ฆ๐—›๐—œ๐— ๐—œ๐—ช๐—˜ - ๐—ž๐—˜๐—ก๐—”๐—ก๐—œ

๐˜ผ๐™จ๐™š๐™ข๐™– ๐™ข๐™–๐™–๐™ข๐™ช๐™ฏ๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐˜พ๐˜พ๐™ˆ ๐™๐™ช๐™š๐™ฃ๐™™๐™–๐™ฃ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™ฉ๐™–๐™ง๐™–๐™Ÿ๐™ž๐™ค ๐™ฎ๐™– ๐™’๐™–๐™ฉ๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™–๐™ฃ๐™ž๐™–.

๐˜ผ๐™จ๐™ž๐™จ๐™ž๐™ฉ๐™ž๐™ฏ๐™– ๐™๐™–๐™ ๐™ช๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™ ๐™ช๐™—๐™ฌ๐™– ๐™ฏ๐™–๐™ž๐™™๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐˜พ๐™๐™–๐™ข๐™–.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndug. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐—ถ amesema ๐—–๐—–๐—  itaendelea kuzingatia ubora wa wagombea wenye uzoefu wa kujenga hoja na kutoa majawabu kwa wananchi kulingana na matakwa na matarajio yao.

Mwenezi Kenani amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakijawahi kukosea katika maamuzi yake na nyakati zote kimekuwa kikifanya maamuzi yenye kuzingatia mahitaji ya Watanzania kwa ujumla pasipo kujali itikadi za vyama vyao.

Aidha, Mwenezi Kenani amesema maamuzi ya chama yanapaswa kuheshimiwa na kila mwanachama huku akieleza kuwa hakuna aliye mkubwa kuliko chama.

Mwenezi Kenani ameeleza hayo leo tarehe 14 Mei 2026 wakati alipotembelea Tawi la veta lililopo shina No.5 kata ya Veta Mjini Musoma Mkoani Mara.

15/05/2026

๐—–๐—–๐—  ๐—ฌ๐—”๐—ช๐—”๐—ง๐—”๐—ž๐—” ๐—ช๐—”๐—ญ๐—”๐—ช๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฆ๐—œ๐— ๐—”๐— ๐—œ๐—” ๐— ๐—œ๐—ฅ๐—”๐——๐—œ ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ช๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐——๐—œ

๐™ˆ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™š๐™ฏ๐™ž ๐™†๐™š๐™ฃ๐™–๐™ฃ๐™ž ๐™–๐™๐™ž๐™ข๐™ž๐™ฏ๐™– ๐™‘๐™ž๐™Ÿ๐™–๐™ฃ๐™– ๐™ ๐™ช๐™จ๐™๐™ž๐™ง๐™ž๐™ ๐™ž๐™จ๐™๐™ฌ๐™– ๐™ž๐™ก๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ฃ๐™ช๐™›๐™–๐™ž๐™ ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™›๐™ช๐™ง๐™จ๐™– ๐™ฎ๐™– ๐™–๐™Ÿ๐™ž๐™ง๐™– ๐™ ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ช๐™ฉ๐™š๐™ ๐™š๐™ก๐™š๐™ฏ๐™–๐™Ÿ๐™ž ๐™ฌ๐™– ๐™ข๐™ž๐™ง๐™–๐™™๐™ž.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐˜‚ ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa barabara zenye urefu wa kilometa 3.364, Kituo cha Mabasi cha Bweri na soko la kisasa Nyasho, leo tarehe 14 Mei 2026.

Katika ukaguzi huo Mwenezi Kenani amewataka wafanyakazi wazawa wanaosimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kuwa wazalendo na kuhakikisha wanailinda kuepuka hujuma na kuhakikisha kazi zinafanyika kwa weledi ili wananchi waliokusudiwa kunufaika na miradi hiyo.

โ€œTunawatakia kila la heri kikubwa tu ninyi wazawa muwe wazalendo katika kusimamia hii miradi msije mkaungana na wakandarasi, mkahujumu miradi,โ€ Alisema Kenani.

Akisomewa taarifa ya mradi huo na Mkandarasi Aloyce Kadokado, alisema mradi huo wa uboreshaji wa barabara unahusisha barabara ya Shabani, Mukendo , Musoma Bus hadi Saa Nane zenye jumla ya kilometa 3.364 na ujenzi wa Stendi ya Bweri na Soko la Nyasho ambao unatarajiwa kufharimu zaidi ya Sh bilioni 21.537.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hadi kufikia sasa mradi umekamilika kwa 21.90% na muda wa mradi uliopita ni 32.33% ambapo Mwenezi Kenani alibaini ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi huo.

Kutokana na hilo, Mwenezi Kenani alihoji ili kufahamu ni changamoto gani iliyosababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi huo na katika majibu ilielezwa kuwa changamoto cha mvua ni moja ya sababu zilizopelekea kuchelewa kukamilika kw amradi huo.

Pamoja na changamoto hizo zilizoelezwa, Mwenezi Kenani alimtaka mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huku akisisitiza kuwa kuna vijana wanaohitaji ajira na ni

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 14/05/2026

BILIONI 16 ZAIDHINISHWA KUTEKELEZA AWAMU NYINGINE YA UJENZI WA HOSPITALI YA MWL NYERERE MARA

MUSOMA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema zaidi ya Sh bilioni 16 zimeidhinishwa bungeni kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Amesema hatua hiyo ni dhamira ya serikali ya kuhakikisha hospitali hiyo inakamilika kwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Mara pamoja na maeneo jirani yanayonufaika na huduma zake.

Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 14,2026 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa hospitali hiyo iliyopo katika Kata ya Kwangwa, Wilaya ya Musoma ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku 5 Mkoani Mara.

Akizungumza hayo Kihongosi amesema ujenzi wa hospitali hiyo ulianza miaka mingi iliyopita lakini ulipata nguvu mpya baada ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wakati huo kufuatilia utekelezaji wake na baadaye kuendelea kutoa fedha zaidi alipokuwa Rais wa Tanzania.

โ€œKatika bajeti iliyopitishwa hivi karibuni, Bunge limeidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa mradi huo huku kazi zikitarajiwa kuanza rasmi mwezi Julai,โ€ amesema Kihongosi.
Kihongosi amewapongeza watumishi wa afya wa hospitali hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya licha ya mazingira yenye changamoto, akisema huduma za afya zinahitaji moyo wa kujitoa na uaminifu mkubwa.

โ€œTumezungumza na wagonjwa na watumishi, wengi wao ni vijana, kazi mnayoifanya si rahisi lakini Mungu awaongoze na awalinde,โ€amesema Kihongosi.

Pia akijibu kuhusu suala la upungufu wa watumishi katika hospitali hiyo alisema taarifa zinaonyesha kuna upungufu wa watumishi kwani waliopo hawaendani na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa, jambo ambalo amesema atalifikisha kwa Waziri mwenye dhamana ili lipewe kipaumbele.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo,Dk Osimund Dyegura amesema tangu mwaka 2021 zaidi ya Sh bilioni 32 zimetumika katika ujenzi wa majengo, ununuzi wa vifaa tiba na magari ya wagonjwa.

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 14/05/2026

KIHONGOSI: โ€œUMUHIMU WA AMANI UWE NI AJENDA NA KIPAUMBELE CHETU.โ€

MUSOMA: Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema madhara ya kupoteza amani ni makubwa kuliko kuilinda amani yenyewe, hivyo amewaasa wananchi kuutambua umuhimu wa amani na kwamba iwe ni ajenda na kipaumbele chao.

Kenani ameeleza hayo leo Mei 14,2026 alipotembelea na kushiriki kikao cha Shina namba Tano Tawi la Veta Kata ya Mwisengwe Veta Musoma Mjini mkoani Mara ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika mkoa huo.

Akizungumza baada ya kusikiliza taarifa fupi ya shina hilo, Kihongosi amesema wamekusanyika na kuhudhuria katika kikao hicho kutokana na amani na utulivu uliopo katika Wilaya ya Musoma na mkoa mzima wa Mara kwa ujumla.

โ€œAmani ndiyo msingi wa maendeleo, amani ndiyo inayoleta kila kitu ndani ya Mkoa wenu wa Mara niwaombe mlinde amani, ikitoweka hakuna atakayelima..watoto hawa hawataenda shule, biashara hamtafungua, umuhimu wa amani iwe ni ajenda na kipaumbele chetu watu wa Musoma,โ€ amesisitiza Kihongosi.

Ameongezaโ€Madhara ya kupoteza amani ni makubwa kuliko kulinda amani yenyewe na hapa ni waibie siri ndogo Wazee wetu, waasisi wa nchi hii, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume wangekuwa wabinafsi, tusingekuta Jamhuri hii ya Muungano wa Tanzania k**a viongozi wetu wasingelinda amani na utulivu wa taifa hili.โ€
Kihongosi aliwataka wananchi wawakatae baadhi ya watu ambao kwa makusudi, kwa tabia mbaya, kwa ajenda zao na kujiangalia wao,wapo tayari nchi iharibike ili wao wafanye mambo yasiyofaa ndani ya taifa hili,

Alisisitiza Mungu amewapa ardhi hivyo hawana nchi nyingine hapa Musoma ndiyo kwao pakiharibika hawana pakukimbilia, hata wakienda nchi jirani atakuwa mkimbizi si kwao, hivyo aliwataka wazazi kuwaelimisha watoto wao na kila kijana aipende nchi yake .

Awali, Katibu wa Shina Namba Tano, Emiliana Kuboja alisoma ajenda ya kikao hicho akieleza kuwa lina wanachama 50 wanaume wakiwa 21 na wanawake 29 na waliolipa ada hadi sasa ni wanachama 35 lakini wameendelea kufanya vikao vya chama pamoja kwa lengo la kuimarisha shughuli za CCM eneo hilo.

14/05/2026

๐— ๐—ง๐—จ๐— ๐—œ๐—ฆ๐—›๐—œ ๐—ช๐—” ๐—ช๐—ข๐—ง๐—˜ ๐—”๐—ฃ๐—ข๐—ž๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐—ช๐—” ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ฆ๐—›๐—”๐—ก๐—š๐—ช๐—˜ ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ž๐—” ๐—”๐—ฅ๐——๐—›๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—จ๐—ฆ๐—ข๐— ๐—”

Maelefu ya Wanachi wa Mkoa wa Mara Wilayani Musoma wamejitokeza katika kumlaki Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐—ถ, Ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa Ziara yake ya kikazi leo tarehe 14 Mei 2026 Mkoani Mara itakayifanyika kwa siku tatu (3).

Wananchi hao wakiwemo wana CCM, wadau mbalimbali wa maendeleo na hata wasio na vyama wameonesha kufurahia ujio wa Mwenezi Kenani huku wakiamini kero na changamoto zao zinakwenda kupata matibabu.

Katika mapokezi hayo, Mwenezi Kenani amepokea salamu za upendo kutoka kwa wananchi hao walizomuomba azifikishe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya huku wakiahidi kulinda na kuitunza ๐—”๐—บ๐—ฎ๐—ป๐—ถ ya nchi yetu.

Huu ni muendelezo wa Ziara ya Mwenezi Kenani ya kutembelea Mikoa yote nchi nzima yenye lengo la kujionea uhai wa chama na jumuiya zake, ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni katika usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi (2025/26) pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi.

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 14/05/2026

MUSOMA: Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amewasili leo Mei 14, 2026 mkoani Mara Region kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nne.

Kihongosi amepokewa na viongozi pamoja na wanachama wa CCM ngazi ya Mkoa na Wilaya, ambapo mara baada ya kuwasili alipata nafasi ya kufanya kikao cha ndani na kuzungumza na viongozi wa chama kuhusu masuala mbalimbali ya uhai na uimarishaji wa CCM katika mkoa huo.

Ziara hiyo inalenga kukagua uhai wa chama kupitia mashina, kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM kupitia miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Aidha, katika ziara hiyo, Kihongosi anatarajiwa kutembelea wilaya za Musoma, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Butiama na Bunda kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na viongozi wa chama kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo na uimarishaji wa chama.

Katika ratiba ya leo, Kihongosi anatarajiwa kutembelea mashina mbalimbali ya CCM katika Musoma, akianza na uzinduzi wa Shina namba tano Tawi la Veta Kata ya Mwisenge, pia atakagua miradi ya maendeleo, na baadaye kufanya mkutano wa hadhara Musoma Mjini.

14/05/2026

Kazi na Utu, Tunasonga Mbele โœ…

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 13/05/2026

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha-Rose Migiro, ameshiriki dhifa ya jioni iliyoandaliwa na Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Chama cha National Resistance Movement (NRM), ikiwa ni sehemu ya shughuli za uapisho wa Rais wa Uganda.

Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Vyama vya Ukombozi na Vyama-rafiki vilivyoshiriki katika hafla hiyo, Katibu Mkuu Migiro alitoa salamu za pongezi kwa Rais Museveni na Chama cha NRM kufuatia kuaminiwa tena na wananchi wa Uganda kuendelea kuiongoza nchi hiyo.

Katika salaam zake, Ndugu Asha-Rose Migiro alisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshik**ano, ushirikiano na urafiki wa kihistoria kati ya vyama vya ukombozi barani Afrika katika kuimarisha maendeleo, amani na ustawi wa wananchi wake.

10/05/2026

๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐—ก๐—–๐—›๐—œ ๐—ช๐—” ๐— ๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ž๐—”๐—˜๐—ก๐—œ ๐— ๐—ž๐—”๐—ข ๐—ช๐—” ๐— ๐—”๐—ฃ๐—ข๐—ž๐—˜๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—ง๐—จ๐— ๐—œ๐—ฆ๐—›๐—œ ๐—ช๐—” ๐—ช๐—ข๐—ง๐—˜ ๐— ๐—ช๐—˜๐—ก๐—˜๐—ญ๐—œ ๐—ž๐—˜๐—ก๐—”๐—ก๐—œ ๐—ž๐—œ๐—›๐—ข๐—ก๐—š๐—ข๐—ฆ๐—œ

๐™‰๐™ž ๐™ข๐™ช๐™š๐™ฃ๐™™๐™š๐™ก๐™š๐™ฏ๐™ค ๐™ฌ๐™– ๐™ฏ๐™ž๐™–๐™ง๐™– ๐™ฎ๐™–๐™ ๐™š ๐™ฎ๐™– ๐™ ๐™ž๐™ ๐™–๐™ฏ๐™ž ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐™จ๐™ž๐™ ๐™ช ๐™ฉ๐™–๐™ฉ๐™ช (3)

Baada ya kumaliza ZIARA ya kikazi Mkoani Geita, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐—ถ (๐™ˆ๐™ฉ๐™ช๐™ข๐™ž๐™จ๐™๐™ž ๐™ฌ๐™– ๐™ฌ๐™ค๐™ฉ๐™š) anabisha hodi Mkoani ๐— ๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ kwa kishindo chenye kuleta matokeo chanya katika kuhakikisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2025/26) inaendelea kutekelezwa ipasavyo kwa maslahi mapana ya wana Mara na Taifa kwa ujumla.

Ziara kuanza tarehe 14 - 16 Mei, 2026.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Dodoma
0000