Ewura Tanzania

Ewura Tanzania

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ewura Tanzania, Government Organization, Ewura House, 3 EWURA Street, Tambukareli, Plot no. 3, P. O. Box 2857, Dodoma.

Ukurasa rasmi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), EWURA imeundwa kwa Sheria ya EWURA Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2019.

02/06/2026

BEI YA PETROLI YASHUKA, SERIKALI YAWEKA RUZUKU KWENYE DIZELI

Watumiaji wa petroli wamepata afueni mwezi Juni 2026 baada ya bei ya mafuta hayo kushuka ikilinganishwa na mwezi uliopita. Kwa Dar es Salaam, petroli sasa itauzwa kwa bei kikomo ya shilingi 4,086 kwa lita, hatua inayotarajiwa kupunguza gharama kwa watumiaji wa kawaida na baadhi ya shughuli za usafiri.

Kwa upande wa dizeli, watumiaji wanakabiliwa na ongezeko dogo la bei, ambapo kwa Dar es Salaam bei kikomo imefikia Shilingi 4,333 kwa lita. Ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia pamoja na kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa bidhaa hiyo.

Licha ya changamoto hizo za kimataifa, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kulinda uchumi na wananchi kwa kuweka ruzuku ya Shilingi 534.91 kwa kila lita ya dizeli. Hatua hiyo imelenga kupunguza athari za ongezeko la bei kwa sekta muhimu k**a usafirishaji, viwanda na huduma za kijamii.

Mabadiliko haya yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati, vinavyohusisha Marekani, Israeli na Irani. Mgogoro huo umeathiri uzalishaji, uhifadhi na usafirishaji wa mafuta duniani, huku kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz kukiongeza gharama za usafirishaji na bima za meli za mafuta.

Photos from Ewura Tanzania's post 02/06/2026

EWURA YAENDESHA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI NJOMBE

Waandishi wa habari wa Mkoa wa Njombe wamepatiwa elimu kuhusu masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji, katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uelewa na kuongeza ushirikiano katika kuelimisha umma kuhusu sekta zinazodhibitiwa.

Akifungua semina hiyo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Wilfred Mwakalosi, alisema, waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi na kuchangia maendeleo ya jamii kupitia elimu wanayoitoa.

“Natumaini elimu mtakayoipata leo itawafikia wananchi na wadau mbalimbali hivyo kuongeza uelewa kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji pamoja na haki na wajibu wa watumiaji wa huduma hizo” alisema.

Katika semina hiyo, Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mha. Walter Christopher, aliwasilisha mada kuhusu majukumu ya EWURA Kanda ya Nyanda za Juu.

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano na Uhusiano, Bw. Mwakalosi, aliwasilisha mada kuhusu umuhimu wa uvunaji wa maji ya mvua, akisisitiza kuwa hiyo ni njia ya kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa maji na mabadiliko ya tabia nchi, hususan maeneo yanayokumbwa na upungufu wa rasilimali hiyo muhimu.

Aidha, Ofisa Huduma kwa Wateja wa EWURA Bw. Francis Mhina, aliwasilisha mada kuhusu EWURA inavyoshughulikia malalamiko kati ya watoa huduma na wateja wa sekta zinazodhibitiwa. Alisema mbalimbali zinazofuatwa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa pande zote.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki, Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe Bw. Binasi Lugono alisema, semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa wanachama, na imewapa uelewa kuhusu masuala ya udhibiti. Aliahidi kuwa elimu waliyoipata wataifikisha kwa wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.

29/05/2026

Mtu yeyote mwenye maoni au pingamizi dhidi ya mabadiliko ya umiliki na majina ya leseni tajwa hapo juu, afanye hivyo kwa maandishi na kuwasilisha EWURA kwa anwani iliyotajwa hapa chini ndani ya siku kumi na nne(14) tokea tarehe ya tangazo hili.

29/05/2026

Mtu yeyote mwenye maoni au pingamizi dhidi ya ombi tajwa hapo juu, afanye hivyo kwa maandishi na kuwasilisha EWURA kwa anwani iliyotajwa hapa chini ndani ya siku kumi na nne (14) toka tarehe ya tangazo hili.

Photos from Ewura Tanzania's post 28/05/2026

Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote aliyetajwa hapo juu kwamba asipewe leseni au Kibali cha ujenzi, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili kupitia anwani tajwa.

27/05/2026

Eid Mubarak

Photos from Ewura Tanzania's post 19/05/2026

EWURA , PAU, ZATEMBELEA VISIMA VYA MAFUTA UGANDA

Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA na wenzao wa Mamlaka ya Udhibiti wa Petroli Uganda (PAU) leo wametembelea eneo la visima vya mafuta Tilenga, Kaskazini mwa jiji la Hoima, kujionea hatua hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya kuanza kuchimba mafuta.

Mafuta hayo yatasafirishwa kwa njia ya bomba la East African Crude Oil Pipeline (EACOP), kutoka Hoima, nchini Uganda, mpaka Chongoleani, Tanga kwa ajili ya kusafirishwa kwa soko la nje. Wataalam wamesema kazi ya ujenzi wa mitambo ya kuchimba, kutenganisha maji na mafuta imefikia asilimia 72.

Bomba la EACOP linamilikiwa kwa pamoja kati ya Shirika la Mafuta la Uganda (asilimia 15), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (15). Kampuni ya Total East Africa Midstream BV ( 62) na China National Offshore Oil Corporation (8).

Wataalam wa ujenzi wamezieleza bodi hizo mbili kwamba bomba la EACOP litaanza kusafirisha mafuta ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, na kwamba katika maeneo mengi ya mradi, ujenzi umekamilika kwa asimia zaidi ya 90.

Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA Prof. Mark amesema Wajumbe wa Bodi hizo mbili wameridhishwa na hatua kubwa zilizopigwa katika ujenzi wa bomba hilo, ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa uunganishaji wa bomba hilo, kulifukia bomba na kusawazisha maeneo yaliyochimbwa. Jana, wajumbe wa bodi hizo mbili walitembelea visima vingine vya mafuta Ziwa Albert, kusini mwa jiji la Hoima, ambako walijionea hatua zilizofikiwa katika shughuli za maandalizi ya uchimbaji mafuta.

Nchini Tanzania, Bodi ya EWURA ilijionea namna ambavyo bomba hilo linavushwa Mto Kagera kwa kupitia handaki lililochimbwa mita 55 kutoka usawa wa ardhi ili kulinda mazingira. EWURA ina wajibu wa kutoa kibali cha ujenzi na leseni ya uendeshaji wa bomba hilo linalotarajiwa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda, hadi Chingoleani, Tanga, Tanzania.

Photos from Ewura Tanzania's post 19/05/2026

Mtu yeyote au kikundi cha watu wenye pingamizi kwa mwombaji yeyote aliyetajwa hapo juu kwamba asipewe leseni au Kibali cha ujenzi, anatakiwa kuwasilisha pingamizi hilo kwa EWURA ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

Photos from Ewura Tanzania's post 19/05/2026
Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Ewura House, 3 EWURA Street, Tambukareli, Plot No. 3, P. O. Box 2857
Dodoma
41104

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 04:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00