29/08/2025
Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania
Tume ya Utumishi wa Walimu ni Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari
29/08/2025
13/02/2024
SERIKALI KUENDELEA KUONGEZA NGUVU KATIKA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA WALIMUI
Serikali imesisitiza kuendelea kuweka nguvu kwenye matumizi ya teknolojia katika kutoa elimu shuleni ikiwa ni moja ya njia za kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu nchini.
Hayo yamesemwa Februari 12, 2024 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde wakati alipotembelewa na ujumbe wa wataalamu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Serikali ya Mapindinduzi ya Zanzibar ambao wamefanya ziara Tume ya Utumishi wa Walimu kwa lengo la kujifunza namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Dkt. Msonde alisema Serikali chini ya Utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada mbalimbali za kuboresha elimu ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu k**a inavyohitajika.
“Kwa sasa tumeanza majaribio ya matumizi ya teknolojia ya ufundishaji inayowezesha Mwalimu kutoka kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa katika maeneo mbalimbali. Tumeanza majaribio haya katika Mikoa miwili ya Pwani na Dodoma na kwa kweli matokeo yake ni mazuri na wanafunzi wanafurahia,” alisema Dkt, Msonde.
Aliongeza kuwa, “kupitia teknolojia hiyo mwalimu anaona wanafunzi wake wote katika maeneo mbalimbali, anaweza kuuliza swali na mwanafunzi akanyoosha mkono na kujibu, yaani ni k**a vile mwalimu yupo hapo hapo.”
Naibu Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa mbali na mfumo huo kurahisisha utendaji kazi kwa walimu, ni moja ya njia za kukabiliana na upungufu wa walimu hususan wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Ameongeza kuwa katika kuendeleza jitihada hizo, Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) tayari ameagiza kutengwa kwa bajeti ili kuwezesha upatikanaji wa angalau darasa moja kwa kila Mkoa na kila Halmashauri katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Pamoja na hayo, Dkt. Msonde alieleza kuwa TSC imeendelea kusimamia masuala ya utumishi wa walimu kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kusimamia ajira, maadili na maendeleo ya walimu ambapo hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ili kumaliza malalamiko ya walimu.
@mohamed_mchengerwa
13/02/2024
WATAALAM WA ELIMU KUTOKA ZANZIBAR WATEMBELEA TSC KUJIFUNZA NAMNA INAVYOFANYA KAZI
Wataalam kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Februari 12, 2024 wametembelea Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kwa lengo la kupata uzoefu wa namna TSC inavyotekeleza majukumu yake katika kuhudumia walimu.
Ujumbe huo ulipokelewa na Katibu wa TSC, Mwl. Paulina Nkwama na kisha kufanya kikao na Menejimenti ya TSC ambapo pamoja na mambo mengine Mwl. Nkwama aliwaeleza wataalam hao kuwa Tume hiyo imeanzishwa kwa Sheria Sura 448 kwa lengo la kusimamia walimu wa Shule za Msingi na Sekondari walio kwenye Utumishi wa Umma Tanzania Bara.
“Tume yetu inasimamia masuala ya Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu. Tume hii inahusika na mwalimu tangu anapoingia kazini hadi anapostaafu kwa maana tunashughulika na ajira yake, tunamthibitisha kazini, tunampandisha cheo, tunambadilishia cheo pale anapojiendeleza kielimu na kutimiza vigezo, tunatoa kibali cha kustaafu lakini pia tunasimamia nidhamu na maadili yake,” alisema Katibu huyo.
Nkwama aliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria hiyo, TSC ina ofisi katika wilaya zote 139 za Tanzania Bara ambapo ofisi hizo ndizo zinazomhudumia mwalimu moja kwa moja jambo ambalo limesaidia kurahisisha mwalimu kupata huduma.
Aliongeza kuwa TSC kwa kushirikiana na Mamlaka zingine imesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa njia mbalimbali ikiwemo kuanzisha Mfumo wa Teachers’ Service Commission Management Information System (TSCMIS) ambao unamfanya mwalimu kuwasilisha changamoto zake kwa kutumia simu yake ya mkononi bila kutoka kwenye kituo cha kazi.
Kwa upande wake, kiongozi wa ujumbe huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bi. Mtumwa Iddi Hamad alimshukuru Katibu wa TSC pamoja na Menejimenti ya Tume kwa kukubali kuwapokea na kuwapa uzoefu wa namna kazi zinavyofanyika katika chombo hicho cha kuhudumia walimu.
Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuanzisha chambo cha kusimamia walimu tofauti na sasa ambapo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ndiyo inayosimamia walimu moja kwa moja.
07/02/2024
Maafisa Rasilimali Watu kutoka Halmashauri zote 184 nchini wakishirikiana na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais - Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na TAMISEMI wakiendelea na kazi maalum ya kuhuisha taarifa na kupakia taarifa sahihi za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Umma ili kukabiliana na changamoto ya malalamiko ya upandaji vyeo na kubadilisha kazi/ vyeo ili Serikali iweze kuchukua maamuzi na hatua stahiki ya kumaliza kabisa changamoto hiyo. Kazi hiyo inaendelea kwa siku 14 kuanzia Jumatano ya tarehe 31.01.2024 Jijini Dodoma.
07/02/2024
MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA UFUNDISHAJI MUBASHARA (SMART CLASSES)
SERIKALI imeanza majaribio ya mfumo wa ufundishaji mbashara ambao mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wa nchi nzima kwa wakati mmoja.
Mfumo huo ambao kwa sasa unafanyiwa majaribio kwa baadhi ya shule za mikoa miwili ya Pwani na Dodoma, unamwezesha mwalimu kutoka kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa mikoa tofauti.
Utaratibu huo unaleta tafsiri ya kwamba mbali na kurahisisha utendaji kazi, pia ni njia mojawapo ya kukabiliana na uhaba wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi shuleni.
Wakati Serikali inaendelea na majaribio ya mfumo huo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodom wamesema mfumo huo utawasaidia kupata uelewa kwa wepesi na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.
28/01/2024
Hongera sana kwa walimu wote nchini.
28/01/2024
Kheri ya kuzaliwa Rais wetu mpendwa.
28/01/2024
Pongezi nyingi kwa walimu nchini.
05/01/2024
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi amepokea msaada wa kiasi cha shilingi milioni tatu kutoka kwa Katibu wa Tume ya Utumishu wa Walimu Tanzania (TSC), Mwl. Paulina Mbena Nkwama kwa ajili ya waathirika wa maafa ya mafuriko katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Dkt. Yonazi amepokea msaada huo ofisini kwake Jijini Dodoma Ijumaa tarehe 05 Januari, 2024.
25/12/2023
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mtendeni
Dodoma
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 15:30 |
| Tuesday | 07:30 - 15:30 |
| Wednesday | 07:30 - 15:30 |
| Thursday | 07:30 - 15:30 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |

26/08/2025