ONWM Tanzania

ONWM Tanzania

Share

Ukurasa Rasmi wa Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati

13/11/2025

Hongera Mhe. Dkt

13/11/2025

Barua ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Spika wa Bunge M***a Azzan Zungu ya kumteua Mhe. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

13/11/2025

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kura 369 baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

29/10/2025

MWITIKIO WAPIGAKURA BUKOMBE WAMFURAHISHA DKT. BITEKO

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko ameeleza kufurahishwa kwake na idadi kubwa ya wananchi wa Jimbo la Bukombe waliojitokeza katika vituo mbalimbali kwa ajili ya kupiga kura.

Akizungumza leo Oktoba 29, 2025 mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bulangwa, Kata ya Bulangwa, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita, Dkt. Biteko amesema kuwa pamoja na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura zoezi hilo limefanyika kwa haraka na wepesi kutokana na utaratibu, maandalizi na usimamizi mzuri uliowekwa katika vituo mbalimbali.

“ Wananchi wamekuja kwa wingi nashukuru kwamba zoezi linafanyika kwa haraka na ni imani yangu hadi kufika saa kumi jioni watu wengi zaidi watakuwa wamepata nafasi ya kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka,” amesema Dkt. Biteko.

Ametoa wito kwa ambao bado hawajafika vituoni kwenda mapema ili waweze kutumia haki yao hiyo ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka ndani ya muda uliopangwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Aidha, amesema mchakato wa maadalizi ya kampeni hadi hatua ya upigaji kura umedhihirisha dhana ya uchaguzi huru na haki kutokana na wananchi kupata fursa ya kuchagua viongozi wao kikatiba.

“ Kila jambo limekwenda kwa utaratibu na ni kitu cha kujifunza, k**a kuna uchaguzi tumefanya kwa utulivu kwa kweli ni huu tumefanya katika mazingira ya utulivu sana na watu kwenye vituo ni wengi na kazi yao ni moja tu kwenda kupiga kura,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Oktoba 29, 2025 ni siku ya Uchaguzi Mkuu ambapo Watanzania katika maeneo mbalimbali nchini wametimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwachagua viongozi wanaowapenda katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mwisho.

17/10/2025

VIONGOZI CWT TUKUBALI KUBADILIKA - DKT. DOTO BITEKO

“ Tumetoka mbali, zamani familia iliyokuwa maarufu na kuheshimika kijijini ni ile iliyokuwa na taa ya chemli na watu walijipanga kuangalia namna inavyofaidi mwanga, Dunia imebadilika kwa kiwango ambacho leo hii kila nyumba ina umeme na watu wanaona umeme k**a hitaji la lazima kwenye maisha yao, Nataka niwaombe walimu wote nchini endeleeni kuishi kwa dunia inayobadilika, fikirini upya kila siku. Viongozi mnatakiwa kuwafikia walimu wote, kuwasikiliza na kuwahudumia ili wapate sababu ya kuwapenda ”. amesema Dkt. Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema hayo Oktoba 16, 2025 katika Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara wakati akifungua Semina ya Viongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kanda ya Ziwa na kanda ya Magharibi iliyoshirikisha viongozi kutoka mikoa minane.

Photos from ONWM Tanzania's post 16/10/2025

WALIMU TUJIENDELEZE KUENDANA NA MABADILIKO DUNIANI-DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza walimu nchini wasichoke kujiendeleza kitaaluma ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea kutokea Duniani.

Dkt. Biteko amesema hayo Oktoba 16, 2025 katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara wakati akifungua Semina ya Viongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kanda ya Ziwa na Ziwa Magharibi iliyoshirikisha viongozi kutoka mikoa minane.

Amesema Serikali imekuwa ikiboresha maisha ya watumishi wake wakiwemo walimu na tayari na walimu wenyewe wanaelewa maboresho yaliyofanyika ili kuwawezesha kuishi maisha ya staha.

“Rais wa CWT amesema hapa kwamba viongozi wote ni wapya, wanafanya kazi wakiwa wapya na muhimu kufanya kazi mkiwa wapya kwa kuzingatia kuwa Dunia imebadilika,” amesema na kuongeza kuwa “Mimi ni zao la mwalimu na nimetumikia taaluma hii, tulikuwa tunadai mambo haya haya tangu kipindi hicho na hata sasa mnaendelea kudai mambo k**a vile mishahara, posho za kufundishia pamoja na nauli”.

Kusema kweli Serikali imefanya mambo mengi kuboresha hali ya walimu na inaendelea kufanya kila jitihada kuhakikisha maisha yao yao yanakuwa bora, Wakati tukiendelea kudai maslahi tukumbuke kwamba dunia imebadilika sana. Pia tuseme ukweli na pengine kutoa shukrani kwa yale mazuri yaliyotokea ama kufanyika.

Amesema Serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuboresha miundombinu ya shule na rasilimali mbalimbali ili kutekeleza miradi mbalimbali.

Aidha, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa ajira zaidi ya 7000 kwa walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi ndani ya kipindi cha siku 100 atakapokuwa amechaguliwa kuwa Rais kwa kipindi kingine cha miaka miaka 5.

Vilevile amewataka walimu kutumia haki yao kikatibu kijitokeza kupiga kura, kuwachagua viongozi wao ifikapo tarehe 29 Oktoba, 2025 ili kutimiza wajibu wa kidemokrasia.

“Hakuna nchi inaweza kuwapata viongozi wa kidemokrasia bila kuwachagua kwa kuwapigia kura. Nawakumbusha ikifika siku ya uchaguzi mkawachague viongozi ambao pamoja na kutimiza jukumu la kikatiba, itakuwa inawapa uhalali wa kudai maendeleo

15/10/2025

TANZANIA YAZINDUA MRADI WA DUNIA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO NA DHARURA ZA KIAFYA

“Wizara zote, Tawala za mikoa na Taasisi , tekelezeni shughuli zote za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa haya ya mlipuko na dharura nyingine za afya kulingana na maeneo yenu na hakikisha kwamba hakuna hata shilingi moja inayopotea au kuchepushwa kando ya malengo yaliyokusudiwa,” amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Oktoba 15, 2025 jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 38.7 unalenga kuboresha huduma za afya kwa watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi.

Photos from ONWM Tanzania's post 15/10/2025

TANZANIA YAZINDUA MRADI WA DUNIA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO NA DHARURA ZA KIAFYA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua Mradi wa Dunia wa kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko nchini na kuzitaka wizara zote tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na taasisi kutekeleza shughuli za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura za kiafya.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Oktoba 15, 2025 jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 38.7 unalenga kuboresha huduma za afya kwa watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi.

Amesisitiza kuwa wizara,taasisi na washirika wa maendeleo wanatakiwa kusimamia utekelezaji katika uwekezaji huo na kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya k**a ilivyokusudiwa.

“Wizara zote, Tawala za mikoa na Taasisi , tekelezeni shughuli zote za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa haya ya mlipuko na dharura nyingine za afya kulingana na maeneo yenu na hakikisha kwamba hakuna hata shilingi moja inayopotea au kuchepushwa kando ya malengo yaliyokusudiwa” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kushirikiana na wadau wote wa ndani na nje ya nchi kuimairsha mradi huo ili uweze kuleta matokeo chanya katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa tishio kwa maisha ya watu na kurudisha nyuma maendeleo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga amesema uzinduzi wa mradi huo, ni muhimu katika jitihaza za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Amesema mradi huo unatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia sehemu ya Afya moja pamoja na wadau wa maendeleo likiwemo Shirika la Afya Duniani(WHO), Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto(UNICEF),Shirika la Chakula na Kilimo
(FAO) na Pandemic Fund.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambaye ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema mradi huo utaboresha mwitikio wa mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa k**a Ebola,MPOX,Marburg,ZIKA na magonjwa mengine yanayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi

04/10/2025

SIKU YA MWALIMU 2025 BUKOMBE





Photos from ONWM Tanzania's post 04/10/2025

SIKU YA MWALIMU DUNIANI 2025 BUKOMBE

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema Mwalimu ndiye anayetoa mwelekeo wa maisha ya kila mtu na ukiona jamii yoyote yenye ustaarabu na kustaarabika huhitaji kupiga ramli kujua nani chanzo chake bali mwalimu ndio sababu yake.

Photos from ONWM Tanzania's post 03/10/2025

WALIMU NI NGUZO YA MAENDELEO - WAZIRI MKUU MAJALIWA

📌Dkt. Biteko asema ualimu ndio taaluma inayomtengeneza mtu awe bora kuliko hata ualimu wenyewe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa walimu ni nguzo kuu ya maendeleo ya taifa lolote hapa duniani kwani ndio wanaotoa rasilimali watu yenye elimu ambayo ni muhimu zaidi kwa Taifa.

Amesema kuwa mafanikio ya kielimu, kijamii na kiuchumi yanatokana na juhudi za walimu kwani walimu ni fahari ya familia, jamii na nchi na kupitia mikono yao vijana wa kitanzania wanajengewa maarifa, stadi na maadili ya uzalendo.

Amesema hayo Oktoba 03, 2025 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani ambayo kiwilaya imeadhimishwa Bukombe mkoani Geita katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Ushirombo.

"Kila hatua ya ustawi wa kijamii na kiuchumi inaanzia darasani kupitia juhudi na maarifa ya walimu. bila walimu, hakuna taaluma, hakuna viongozi wa kesho na hakuna Taifa linaloweza kusimama imara, walimu ndio chimbuko la uvumbuzi na ubunifu wa kizazi kipya.".

Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kada ya ualimu hapa nchini, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya kada hiyo ikiwemo kwa kupandisha madaraja na kuimarisha mafunzo kwa walimu.

Ameongeza kuwa ili kukabiliana na upungufu wa walimu nchini Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuthamini na kuwekeza katika kada ya ualimu kwa kuajiri walimu wapya kila mwaka.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Ofisi ya Rais - UTUMISHI kufanya msawazo wa walimu ndani ya mikoa husika kwa kuhakikisha kila shule inapata walimu ili watoto wa Kitanzania wapate elimu bora.

"Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Vyuo vya Ualimu na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imarisheni mafunzo ya kitaaluma na endelevu kwa walimu ili waendane na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya dunia ya leo". Amesema Mhe. Majaliwa.

Naye, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa taaluma ya ualimu ndio taaluma pakee inayomtengeneza mtu awe bora kuliko hata ualimu wenyewe na wakati wowote hujinyima muda wake na nguvu zake zote kumtengeneza mtu kuwa mume au mke bora

Photos from ONWM Tanzania's post 03/10/2025

WAALIMU WA BUKOMBE WANASEMA NA KUTENDA

“Utamaduni wa waalimu katika wilaya ya Bukombe tumekubaliana hatutakuwa na maneno matupu ila tunasema na tunatenda” - Mgombea Ubunge jimbo la Bukombe Dkt. Doto Mashaka Biteko akiteta na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kuingia ndani ya viwanja vya Shule ya Sekondari Ushirombo




Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Mji Wa Serikali, Mtumba
Dodoma
P.O.BOX2494,MTUMBA