02/06/2026
PONGEZI KWA UTEUZI WA NDG. UMMY MWALIMU KUWA MSHAURI WA RAIS MASUALA YA AFYA YA UZAZI, MAMA NA MTOTO
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) ikiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) unampongeza Ndg. Ummy Mwalimu kufuatia kuaminiwa na kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.
Uteuzi huu ni uthibitisho wa uzoefu wake mkubwa, weledi, uzalendo na mchango wake uliotukuka katika sekta ya afya nchini. Katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kuzitumikia, ameonesha uwezo wa kipekee katika kusimamia na kuimarisha huduma za afya, hususani zinazohusu afya ya uzazi, mama na mtoto.
Tunaamini kuwa kupitia nafasi hii mpya, ataendelea kutoa ushauri wenye tija utakaosaidia kuimarisha sera, mipango na huduma za afya kwa manufaa ya wananchi, hususani wanawake, watoto na familia kwa ujumla.
Hongera sana Ndg. Ummy Mwalimu kwa uteuzi huu muhimu na wa heshima. Mungu akubariki na akuongoze katika utumishi wako.
02/06/2026
HONGERA SANA Mhe.Emmanuela Mtatifikolo kwa kushinda kwa kishindo na kuwa mbunge wa Jimbo la Isimani.
01/06/2026
VIONGOZI WA UWT TAIFA WASHUHUDIA UWASILISHWAJI WA BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII BUNGENI DODOMA
Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa UWT, Mhe. Zainab Khamis Shomari (MNEC), leo tarehe 1 Juni, 2026 wamehudhuria na kushuhudia uwasilishwaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jijini Dodoma.
Bajeti hiyo imewasilishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ikiwa na lengo la kuendelea kuimarisha ustawi wa jamii, kuwawezesha wanawake kiuchumi, kulinda haki za makundi maalum na kuendeleza mipango ya maendeleo ya kijamii nchini.
Viongozi wengine wa UWT waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa UWT, Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC), Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara, Ndg. Riziki Kingwande (MNEC), pamoja na watumishi wa Jumuiya ya UWT.
Ushiriki wa viongozi hao unaonesha dhamira ya UWT katika kufuatilia na kuunga mkono sera, mipango na bajeti zinazolenga kuimarisha maendeleo ya wanawake, watoto na makundi maalum nchini.
31/05/2026
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), ameshiriki ufungaji wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Migori jana, tarehe 31 Mei 2026, kuelekea Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Ismani unaofanyika leo, tarehe 1 Juni 2026.
Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara, Chatanda amebainisha mambo mbalimbali aliyowahasa wanawake katika kipindi chote cha kampeni. Amesisitiza kuwa CCM imeonyesha imani kubwa kwa kuweka mgombea mwanamke, Ndg. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, na kwamba sasa ni jukumu la wanawake wote kuungana na kushirikiana ili kuhakikisha ushindi unapatikana.
Pia, ametoa wito kwa wanawake wote kujitokeza kwa wingi na kuwahimiza wenza wao kwenda kupiga kura mapema asubuhi.
Mgeni rasmi katika ufungaji huo wa kampeni alikuwa Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Ndg. Issa Haji Ussi (Gavu).
31/05/2026
SHAMRASHAMRA NA MAFURIKO YA WATU ZATAWALA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM ISMANI
Hivi ndivyo hali ilivyo kwenye Mkutano wa Hadhara wa kufunga Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Migori, Jimbo la Ismani, Mkoa wa Iringa leo tarehe 31 Mei, 2026.
Shukrani za pekee kwa wana-Migori wote waliojitokeza kwa wingi kuunga mkono maendeleo.
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Ismani lililopo Wilaya ya Iringa Vijijini unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 1 Juni, 2026.
*Tukutane kwenye sanduku la kura!*