National Health Insurance Fund

National Health Insurance Fund

Share

The Management of the Fund is vested in the Board of Directors.

The Official Account of the National Health Insurance Fund (NHIF) of Tanzania I Ukurasa Rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 🇹🇿

Customer Service Toll Free - 199
Fraud Reporting Toll Free - 0800111163

www.nhif.or.tz The National Health Insurance Fund is a statutory health insurance scheme which was established by Parliamentary Act No.8 of 1999,in order to facilitate access to health services b

Photos from National Health Insurance Fund's post 06/05/2026

USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NHIF/TSN KWENYE UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Dodoma 06/05/2026

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) Bi. Asha Dachi jijini Dodoma ambapo masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano yalizungumzwa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TSN Bi. Dachi, alianza kwa kutoa shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kwa ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, aliendekea kusema kuwa anatambua kuwa NHIF imebeba agenda kubwa ya kitaifa, agenda ya Bima ya Afya kwa Wote, suala hili ni kubwa hivyo kuhitaji jitihada za pamoja ili kufanikiwa kuwafikia watanzania wote. Aidha Bi. Dachi alimhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kuwa TSN iko tayari kuibeba agenda hiyo kupitia majukwaa mbalimbali waliyonayo ikiwemo magazeti na mitandao ya kijamii (digital platforms). Kuna maboresho makubwa yamefanyika TSN ambapo kwa sasa magazeti yanasomwa kupitia mtandao (online) sio lazima kusoma nakala ngumu, alisema Bi. Dachi, pia habari zote zinapatikana katika mitandai ya kijamii ya TSN jambo linalofanikisha kufikia watu wengi kwa wakati sahihi.

Bi. Dachi aliendelea kusema kuwa TSN ingetamani kuwepo na mashirikiano ta kimkakati na NHIF katika kujenga uelewa wa Bima ta Afya kwa Wote (UHI) na hatimaye ndoto kubwa ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Isaka alikaribisha kwa mikono miwili mawazo yaliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa TSN, na kuekezea kuwa mawazo hayo yamekuja wakati sahihi ambapo Mfuko unafanya jitihada khbwa nchi nzima kutoa elimu na kusajili wanachama chini ya Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Ujio wenu utasaidia sana kujenga uelewa na hivyo kurahisisha zoezi la usajili wa wanachama, alisema Dkt. Isaka.

Wakihitimisha mazungumzo, watendaji Wakuu wa taasisi hizo, walikubaliana kuingia makubaliano rasmi yenye kuonesha maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya taasisi hizi kwa lengo la kufikia malengo ya kitaasisi na hatimaye kufanikisha agenda ya kitaifa ya Bima ya Afya kwa Wote.


01/05/2026

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!


Photos from National Health Insurance Fund's post 30/04/2026

WANANCHI WANUFAIKA NA HUDUMA ZA NHIF KATIKA MAONESHO YA OSHA NJOMBE

Wananchi wameendelea kupata huduma mbalimbali za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika banda la NHIF lililopo kwenye maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mwema, mkoani Njombe.

Kupitia banda hilo, wananchi wamepata huduma muhimu za uanachama ikiwemo kujisajili kujiunga na NHIF, kuhuisha taarifa zao, kuongeza wategemezi pamoja na kupatiwa elimu kuhusu vifurushi mbalimbali vya bima ya afya vinavyotolewa na Mfuko. Huduma hizo zimetolewa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa bima ya afya na kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwa na kinga ya matibabu.

Maafisa wa NHIF kutoka Ofisi ya Mkoa wa Njombe wamekuwepo kutoa huduma hizo kwa ufanisi, wakisaidiana na wanamichezo wa NHIF walioungana nao katika kuwahudumia wananchi pamoja na kutoa elimu ya afya. Ushirikiano huo umeongeza hamasa na kuvutia wananchi wengi zaidi kufika katika banda hilo.

Wananchi waliotembelea banda hilo wamepongeza juhudi za NHIF kwa kusogeza huduma karibu nao, huku wakieleza kuwa elimu waliyoipata imewasaidia kuelewa zaidi faida za bima ya afya katika kukabiliana na gharama za matibabu.

Ushiriki wa NHIF katika maonesho ya OSHA unaendelea kuwa muhimu kwa lengo la kufikisha huduma na elimu kwa jamii, sambamba na kuhamasisha umuhimu wa afya na usalama katika maisha ya kila siku.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!



Photos from National Health Insurance Fund's post 29/04/2026

NHIF YAFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA ROBO YA TATU YA MWAKA WA FEDHA 2025/26

Dodoma 29/04/2026

Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), chini ya Mwenyekiti wake Bw. Eliud Sanga, imekutana jijini Dodoma kwa lengo la kupokea taarifa ya maendeleo ya Mfuko kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/26.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 29 Aprili, 2026 kikitanguliwa na vikao vya kamati za Bodi vilivyofanyika tarehe 27 - 28 April, 2026. Kamati hizo ni Kamati ya Fedha na Uendeshaji (Finance & Operations Committee) chini ya Mwenyekiti Prof. George Ruhago, Kamati ya Ukaguzi na Hadhari ya Vihatarishi (Audit & Risk Commitee) chini ya Mwenyekiti CPA. Veronica Kishala na Kamati ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala Bora ( Human Resources and Governance Committee) chini ya Kaimu Mwenyekiti Wakili. Shaaban Kabunga.

Wajumbe wengine wa Bodi waliohudhuria kikao hicho ni Prof. Ramaiya Kaushik na Bi. Zubeda Chande.

Wenyeviti wa Kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa zao mbele ya Bodi, Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wajumbe wengine kwa pamoja waliipongeza Menejimenti ya Mfuko kwa mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha robo ya tatu.

Bodi ilipongeza mafanikio ya usajili wa wanachama yaliyofikia asilimia 58, aidha kuendelea kupungua kwa siku za ulipaji madai kwa watoa huduma (aging), kadhalika Bodi ilipongeza ( investment performance, vilevile Bodi iliendelea kupongeza matokeo mazuri kwenye ukuaji wa rasilimali za Mfuko pamoja na ziada (surplus) inayoendelea kukua zaidi.

Vilevile walipongeza mazoezi kwa watumishi na ushiriki wao kwenye michezo ya Mei Mosi pamoja na marathon ambazo zaidi ya watumishi 168 wamekuwa wakishiriki

Pamoja na pongezi hizo Bodi ilitoa maelekezo kadhaa ili kuboresha za kulinda mafanikio yaliyopatikana;

i. Mfuko uendelee kufanya uwekezaji makini ili kuongeza ukwasi kwa ajili ya kujenga uwezo zaidi wa kifedha na kutengeneza ziada kubwa zaidi;

ii. Kuendelea kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kupambana zaidi na vitendo vya udanganyifu,

iii. Bodi ilielekeza kuendelea kutoa elimu kwa watoa huduma kuhusu fursa ya mikopo ya NHIF ili wafunge vifaa vya utambuzi wa wanachama kupitia alama za vidole (biometric verification).

iv. NHIF tuendelee kuwa mfano wa kuigwa katika jitihada za kupambana na magongwa nyemelezi (NCDs) ili jamii na hatimaye kuepukana na gharama kubwa za kutibia magonjwa hayo;

v. Kuendelea kutekeleza ESG kwa kupanda miti na kupunguza matumizi ya karatasi

vi. Mfuko uendelee na hatua mbalimbali za kutatua changamoto za watumishi kupitia njia mbalimbali ikiwemo HR Clinics.

vii. kwa upande mwingine Bodi ilielekeza watumishi nao kutimiza wajibu wao pamoja na kufuata Sheria, miongozo na taratibu katika kutekeleza majukumu yao;

viii. Menejimenti iendelee kufanyia kazi hoja wa wakaguzi wa ndani na ukaguzi wa nje. Vilevile kutekeleza kwa wakati mapendekezo ya Wadhibiti pamoja na Actuarial recommendations.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Irene Isaka aliishukuru Bodi kwa kuendesha kikao vizuri pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa na Bodi, kwani miongozo hiyo imekuwa chachu kubwa ya kuteleleza majukumu ya Mfuko kwa mafanikio. Aidha aliihakikishia Bodi kuwa Menejimenti inafanyia kazi maelekezo yote ya Bodi ili kuboresha zaidi ustawi wa Mfuko.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa

29/04/2026

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!




28/04/2026

NHIF NA JIBU LA SWALI LAKO
Swali: Je nawazaje kujisajili na Vifurushi vya NHIF kupitia mfumo wa Self-Service?

Bima ya Afya kwa Wote, jiunge Sasa!



28/04/2026

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa !


27/04/2026

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!


Photos from National Health Insurance Fund's post 27/04/2026

NHIF Yatwaa Ubingwa wa Netiboli Mashindano ya OSHA Njombe

Timu ya wanawake ya mpira wa pete (netiboli) ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanikiwa kutwaa kombe la mshindi wa kwanza katika mashindano ya OSHA yaliyofanyika mkoani Njombe, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya OSHA. Ushindi huo umeonyesha kiwango cha juu cha ushindani dhidi ya timu zilizoshiriki mashindano hayo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi, Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Suzan Mkangwa, alisema kuwa bonanza hilo lina faida kubwa kwa watumishi, ikiwemo kuongeza ufanisi kazini, kuleta wafanyakazi pamoja na kuimarisha mshikamano. Alibainisha kuwa michezo huchochea motisha kazini, huboresha mawasiliano, na kuwajengea watumishi uwezo wa kusikilizana pamoja na kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali kwa ubunifu.

Aidha, aliongeza kuwa taasisi zinazothamini michezo huwa na wafanyakazi wenye ari na morali ya juu ya kazi, hali inayochangia kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila sikuna pia kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCD’s).

Naye kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Bi. Jacqueline Sikozi akizungumza kwa niaba ya wachezaji wote wa timu ya netiboli alitoa shukurani kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Irene Isaka kwa kuwezesha ushiriki wa watumishi katika michezo ya Mei Mosi ambayo imekuwa ni sehemu ya kujiimarisha kiafya na kiakili.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!

26/04/2026

TANZIA.

26/04/2026

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa !


24/04/2026

NHIF YAIBOMOA UJENZI 2 KWA 0

Timu ya mpira wa miguu ya NHIF imeshinda magoli 2 kwa 0 dhidi ya timu ya Ujenzi katika mechi iliyoendelea leo Aprili 24, 2026 huko Mkoani Njombe katika mwendelezo wa kuhamasisha utunzaji wa afya kwa watumishi na wanamichezo kwa ujumla kuelekea sikukuu ya MeiMosi 2026.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa


Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


NATIONAL HEALTH INSURANCE FUND
Dodoma
P.OBOX1437

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:00
Tuesday 07:30 - 16:00
Wednesday 07:30 - 16:00
Thursday 07:30 - 16:00
Friday 07:30 - 16:00