06/05/2026
USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NHIF/TSN KWENYE UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE
Dodoma 06/05/2026
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) Bi. Asha Dachi jijini Dodoma ambapo masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano yalizungumzwa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TSN Bi. Dachi, alianza kwa kutoa shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kwa ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, aliendekea kusema kuwa anatambua kuwa NHIF imebeba agenda kubwa ya kitaifa, agenda ya Bima ya Afya kwa Wote, suala hili ni kubwa hivyo kuhitaji jitihada za pamoja ili kufanikiwa kuwafikia watanzania wote. Aidha Bi. Dachi alimhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kuwa TSN iko tayari kuibeba agenda hiyo kupitia majukwaa mbalimbali waliyonayo ikiwemo magazeti na mitandao ya kijamii (digital platforms). Kuna maboresho makubwa yamefanyika TSN ambapo kwa sasa magazeti yanasomwa kupitia mtandao (online) sio lazima kusoma nakala ngumu, alisema Bi. Dachi, pia habari zote zinapatikana katika mitandai ya kijamii ya TSN jambo linalofanikisha kufikia watu wengi kwa wakati sahihi.
Bi. Dachi aliendelea kusema kuwa TSN ingetamani kuwepo na mashirikiano ta kimkakati na NHIF katika kujenga uelewa wa Bima ta Afya kwa Wote (UHI) na hatimaye ndoto kubwa ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Isaka alikaribisha kwa mikono miwili mawazo yaliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa TSN, na kuekezea kuwa mawazo hayo yamekuja wakati sahihi ambapo Mfuko unafanya jitihada khbwa nchi nzima kutoa elimu na kusajili wanachama chini ya Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Ujio wenu utasaidia sana kujenga uelewa na hivyo kurahisisha zoezi la usajili wa wanachama, alisema Dkt. Isaka.
Wakihitimisha mazungumzo, watendaji Wakuu wa taasisi hizo, walikubaliana kuingia makubaliano rasmi yenye kuonesha maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya taasisi hizi kwa lengo la kufikia malengo ya kitaasisi na hatimaye kufanikisha agenda ya kitaifa ya Bima ya Afya kwa Wote.

01/05/2026
30/04/2026
29/04/2026
28/04/2026
27/04/2026
27/04/2026
26/04/2026
26/04/2026
24/04/2026