*KWA NINI TPRB IMEANDAA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAKURUGENZI WA KAMPUNI ZA MIPANGOMIJI ZILIZOSAJILIWA TANZANIA BARA*
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB), TP. Martha Mkupasi akibainisha sababu ya Bodi hiyo kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakurugenzi wa kampuni za mipangomiji zilizosajiliwa Tanzania Bara yaliyofanyika Aprili 14, 2026 jijini Dar es Salaam.
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji -TPRB
Bodi ipo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji Sura 426 ya Mwaka 2007.
Bodi ina mamlaka ya kusimamia viwango vya utendaji, tabia na maadili ya wataalam wa pamoja na kampuni za mipamgomiji.
*TPRB YAWAPA MAFUNZO WAKURUGENZI KAMPUNI ZA MIPANGOMIJI, WATAKIWA KUONGOZA MAGEUZI YA SEKTA YA MIPANGOMIJI*
Wakurugenzi wa kampuni za mipangomiji zilizosajiliwa Tanzania Bara wametakiwa kuongoza mageuzi makubwa yatakayochochea ukuaji wa sekta hiyo na kuhakikisha miji inapangwa kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TP. Deogratius Kalimenze, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakurugenzi wa kampuni za mipangomiji yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB) jijini Dar es Salaam.
TP. Kalimenze amesisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya taaluma, akiwataka wataalamu hao kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kubaini na kudhibiti vitendo vya watu wanaofanya kazi za mipangomiji bila kufuata taratibu, ikiwemo kutosajiliwa na TPRB.
Kwa upande wake, Kaimu Msajili wa TPRB, TP. Martha Mkupasi, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wakurugenzi hao kwa kuwapatia jukwaa la kujadili changamoto wanazokutana nazo, kubaini mbinu za kuzitatua pamoja na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma.
Ameeleza kuwa jukwaa hilo ni muhimu katika kuimarisha taaluma ya mipangomiji, huku likichochea utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu ili kufanikisha ujenzi wa miji endelevu, jumuishi na inayokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
Wakizungumza baada ya mafunzo hayo, baadhi ya wakurugenzi wa kampuni za mipangomiji wameishukuru TPRB kwa kuandaa mafunzo hayo, wakieleza kuwa yamekuwa chachu ya mabadiliko chanya katika uendeshaji na utoaji wa huduma ndani ya kampuni zao.
13/04/2026
Karibuni Wakurugenzi wa Makampuni ya Upangajimiji
02/04/2026
KARIBUNI KAMPUNI ZA MIPANGOMIJI
05/02/2026
*TPRB YAKUTANA NA WATAALAMU WA MIPANGOMIJI MKOA WA IRINGA, YAWAHIMIZA KUZINGATIA MAADILI NA VIWANGO VYA TAALUMA*
Uongozi wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) umefanya kikao kazi na Maafisa na Wataalam wa Mipangomiji wa Mkoa wa Iringa kikiwa na lengo la kukumbushana masuala muhimu yanayohusu taaluma ya Mipangomiji.
Kikao hicho ambacho kimefanyika leo Alhamisi Februari 05, 2026 mkoani Iringa kimeongozwa na Kaimu Msajili wa TPRB, TP. Martha Mkupasi.
Akizungumza katika kikao hicho, TP. Mkupasi ambaye aliambatana na wataalamu wa kutoka TPRB, amewahimiza wataalam hao kuzingatia maadili ya taaluma, sheria, kanuni na miongozo inayosimamia taaluma ya mipangomiji, amesisitiza kuwa utekelezaji wa majukumu yao una mchango mkubwa katika uendelevu na ustawi wa jamii.
Kikao hicho ni mwendelezo wa utakelezaji wa mikakati ya TPRB ya kuhakikisha wataalamu na kampuni za mipangomiji zinazingatia sheria, kanuni na miongozo katika utoaji wa huduma.
29/01/2026
TAARIFA KWA UMMA
27/01/2026
WATUMISHI WA TPRB WASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI KUMTAKIA 'HAPPY BIRTHDAY' RAIS SAMIA
Watumishi wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) wameungana na Watanzania wengine katika zoezi la upandaji miti, ikiwa ni sehemu ya kumtakia heri ya Siku ya Kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuendeleza ajenda ya ulinzi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Zoezi hilo limefanyika leo Jumanne, Januari 27, 2026, katika Ofisi za TPRB zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ambapo watumishi walipanda miti mbalimbali ikiwa ni mkakati wa kuhifadhi na kulinda mazingira ikiwa ni kutekeleza kauli mbiu ya ‘ Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Shiriki Kupanda Miti'
Kampeni hiyo ya upandaji miti ni sehemu ya kuunga mkono maono ya Rais Samia ya kulinda na kuhifadhi mazingira ikiwa inaakisi upangaji miji endelevu unaoendana na uhifadhi wa mazingira na rasilimali asilia, ambapo kabla ya watumishi wa TPRB kushiriki zoezi hilo lilizinduliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo na Naibu wake Mhe. Kaspar Mmuya kwenye Ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
_
_
_
WIZARA YA ARDHI YAINGILIA KATI SAKATA LA ENEO LENYE MGOGORO GEITA
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeingilia kati mgogoro wa matumizi ya ardhi unaomhusisha mwekezaji Rashid Kwanzibwa, aliyedaiwa kubomoa baadhi ya majengo yaliyokuwa kwenye maeneo ya serikali na kuanzisha miradi bila utaratibu katika eneo la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro, Geita.
Akitolea ufafanuzi kuhusu suala hilo leo, tarehe 26 Januari, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amesema wizara yake inaungana na Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha mgogoro unafanyiwa kazi na kukamilika.
Mhe. Dkt Akwilapo amewakumbusha wamiliki wa maeneo yote nchini kuzingatia matumizi yaliyokusudiwa katika hati miliki zao, na endapo mmiliki ana mpango wa kuendeleza eneo lake kwa matumizi tofauti na yaliyotolewa katika hati, ni lazima apate kibali cha mabadiliko ya matumizi k**a sheria inavyoelekeza.
17/12/2025
TPRB YATOA TUZO KWA WANAFUNZI WATATU VINARA CHUO KIKUU ARDHI
Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imetoa tuzo kwa wanafunzi watatu waliofanya vizuri zaidi katika somo la Taaluma ya Mipangomiji (Professional Practice) katika Chuo Kikuu Ardhi (Ardhi University), ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kutambua na kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri zaidi na kuwa na wataalamu wenye weledi wa hali ya juu katika taaluma ya Mipangomiji.
Tuzo hizo zimetolewa tarehe 16/12/2025 katika hafla ya utoaji tuzo za kitaaluma iliyofanyika katika Jengo la Arch Plaza, Chuo kikuu Ardhi. Mgeni Rasmi katika utoaji wa tuzo hizo alikuwa Prof. Evaristo Joseph Liwa, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi.
Tuzo hizo zimetolewa kwa wahitimu wa mwaka 2025 wa shahada ya kwanza, katika fani tatu tofauti za mipangomiji k**a mwendelezo wa dhamira ya Bodi hiyo ya kuhamasisha ubora, nidhamu, uadilifu na weledi miongoni mwa wanafunzi wanaoingia soko la ajira na kufanya kazi za taaluma ya mipangomiji nchini.
Wahitimu hao walitunukiwa tuzo maalum ijulikanayo k**a “TPRB Final Year Best Student in Professional Practice Subject Award 2025”, baada ya kuonyesha kiwango cha juu cha ufaulu katika mwaka 2025. Kupitia tuzo hizo, TPRB inalenga kuwatia moyo wanafunzi kujenga misingi imara katika taaluma ya mipangomiji.
Tuzo hizo zilikabidhiwa na Afisa Mipangomiji Mwandamizi, TP. Mdoe Mjema kwa niaba ya Msajili wa Bodi ya Usajili wa wataalamu wa Mipangomiji.
Wahitimu waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Mary Jonas aliyekuwa akifanya kozi ya BSc. Housing and Infrastructure Planning; Doreen Litayunga kozi ya BSc. Regional Development Planning; pamoja na Leonel P Mollel aliyefanya kozi ya BSc. Urban and Regional Planning.
11/12/2025
UMEHUISHA LESENI?
14/10/2025
KAMATI YA ELIMU, MAFUNZO NA WELEDI YA TPRB YAFANYA KIKAO CHA USAJILI WA WATAALAMU WAPYA WA MIPANGOMIJI
Kamati ya Elimu, Mafunzo na Weledi ya Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imefanya kikao chake cha 37 kujadili maombi ya usajili wa wataalamu wapya wa mipangomiji kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kikao hicho cha siku mbili kimeanza Jumatatu Oktoba 13, 2025 katika Ofisi za Bodi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma na kuhitimishwa leo Jumanne.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, TP. Dkt. Regina John na Katibu ambaye ni Kaimu Msajili wa TPRB, TP. Martha Mkupasi, ambapo wajumbe walipokea na kujadili maombi 21 ya usajili wa wataamu wapya wa mipangomiji.
Pia, kikao hicho kilipokea na kilijadili mwenendo wa utekelezaji wa majukumu ya kusimamia taaluma na maendeleo ya taaluma, changamoto zilizojitokeza pamoja na mikakati ya kuboresha weledi na ufanisi katika taaluma ya mipangomiji.
Miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni mapendekezo ya utatuzi wa changamoto za uendelezaji wa viwanda katika Mkoa wa Pwani.
Aidha, kikao hicho kilipokea taarifa ya uchambuzi wa kina wa namna ya kuwapatia mafunzo wataalamu wa mipangomiji ambao hawakupata fursa ya kupitia module za mafunzo kwa vitendo ili kuinua uwezo wao katika kutekeleza majukumu ya mipangomiji na kuwapatia sifa za kuweza kusajiliwa kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira.
Mwenyekiti wa Kamati, TP. Dkt. Regina John, aliwapongeza wajumbe kwa uchambuzi makini wa hoja mbalimbali na kuhimiza kuendelea kuweka mkazo katika kuinua ubora wa elimu, mafunzo na weledi katika fani ya mipangomiji, akisisitiza kuwa taaluma hiyo ni nguzo muhimu katika maendeleo endelevu ya miji na vijiji nchini.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Contact the business
Website
Address
Barabara Ya Maktaba S. L. P. 1150, 41102 DODOMA
Dodoma
026
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 15:30 |
| Tuesday | 07:30 - 15:30 |
| Wednesday | 07:30 - 15:30 |
| Thursday | 07:30 - 15:30 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |
