Jukwaa la Biashara na Uwekezaji la Tanzania na Urusi linafanyika leo Mei 15, 2026 Ukumbi wa AICC,Mkoani Arusha. Jukwaa hilo la siku moja, litahusisha majadiliano ya kibiashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Urusi.
Msemaji Mkuu wa Serikali
Ukurasa Rasmi wa Msemaji wa Serikali ya Tanzania | Official account of the Chief Spokesperson of the Government of Tanzania.
SIKU YA 02: KIKAO KAZI CHA 21 CHA MAAFISA HABARI,MAWASILIANO, ITIFAKI NA UHUSIANO SERIKALINI
26/04/2026
https://podcasts.apple.com/tz/podcast/maelezo-podcasts/id1506559068?i=1000763588398
Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando Podcast Episode · MAELEZO PODCASTS · 25 April · 39min
26/04/2026
https://open.spotify.com/episode/7IAR6Sfa7k4kDGMm31QWeE?si=yNgRsmVCQd2xpEtAY27_Rw
Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando MAELEZO PODCASTS · Episode
RAIS SAMIA KUZINDUA MELI YA UVUVI WA BAHARI KUU APRILI 25, 2026 - DKT BASHIRU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuzindua Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu , ambapo uzinduzi wake utafanyika Makao Makuu ya
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO ) Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea na kukagua ujenzi wa bahari ya uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lind na kuieleza kamati hiyo kuwa bandari ya uvuvi Kilwa masoko iliyogharimu shilingi bilioni 280 baada ya kukamilika itafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa kwa serikali.
30/01/2026
FURSA MPYA KWA VIJANA: BILIONI 2 KWA WATENGENEZAJI WA MAUDHUI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.
Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.
Amebainisha kuwa, zoezi la uandikishaji wa walengwa linaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.
17/09/2025
Matukio katika picha
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa leo Septemba 17, 2025, amezungumza kwenye kipindi cha Kumepambazuka cha Redio One, kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuwaasa wananchi kutumia haki yao ya kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025 pamoja na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa vijana wa Kitanzania.
15/09/2025
Taarifa muhimu 📌
15/09/2025
📌
14/09/2025
Taarifa kwa Umma📌
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Dodoma

30/01/2026