Ofisi ya Waziri Mkuu

Ofisi ya Waziri Mkuu

Share

Huu ni ukurasa rasmi wa Facebook wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Tufuatilie ili kupata habari za uhakika, vipaumbele vya Serikali, na maendeleo ya taifa.

Tunatoa taarifa sahihi, matukio, na shughuli za Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na taarifa rasmi za Serikali.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu's post 02/06/2026

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Wabunge mbalimbali wakati wa vikao vya bunge vinavyoendelea.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu's post 02/06/2026

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Bungeli leo jijini Dodoma 2 Juni 2026 wakati wa Uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha.

01/06/2026

“Agnes alikuwa kiongozi aliyekuwa tayari kusimamia jambo aliloamini ni sahihi kwa manufaa ya wananchi. Alikuwa na ujasiri wa kusema ukweli na kusimamia maendeleo ya watu wake bila kuyumbishwa-Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba

📍Shelui-Singida
🗓️Juni 1, 2026

——————————

Amesema hayo aliposhiriki ibada ya mazishi ya Diwani wa Kata ya Shelui, Mhe. Agnes Nasania, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Shelui, wilayani Iramba mkoani Singida.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu's post 01/06/2026

DKT. MWIGULU ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA DIWANI AGNES NASANIA WILAYANI IRAMBA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu Juni 1, 2026 ameshiriki ibada ya mazishi ya Diwani wa Kata ya Shelui, Mhe. Agnes Nasania, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Shelui, wilayani Iramba mkoani Singida.

Akizungumza katika ibada hiyo, Dkt. Mwigulu amesema marehemu Agnes Nasania alikuwa kiongozi jasiri, mkweli na mwenye msimamo katika kusimamia maslahi ya wananchi wa Kata ya Shelui.

“Agnes alikuwa kiongozi aliyekuwa tayari kusimamia jambo aliloamini ni sahihi kwa manufaa ya wananchi. Alikuwa na ujasiri wa kusema ukweli na kusimamia maendeleo ya watu wake bila kuyumbishwa,” amesema Dkt. Mwigulu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu ameahidi kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu na kusaidia ustawi wa watoto wake ili kuhakikisha wanaendelea na masomo na kutimiza ndoto zao.

Aidha, amewataka wananchi wa Shelui kuendelea kudumisha umoja na mshikamano wakati huu wa maombolezo na kuepuka migawanyiko inayoweza kuathiri maendeleo ya eneo hilo.

Awali, akiongoza ibada hiyo, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati (Singida), Dkt. Syprian Hilinti amesema marehemu Agnes Nasania alikuwa kiongozi mwenye moyo wa huduma, aliyewapenda watu na aliyejitolea kwa dhati kulitumikia Kanisa, jamii na taifa.

“Agnes ametuonyesha kuwa inawezekana kuwa mwanasiasa na ukaendelea kuwa mtumishi wa watu, mcha Mungu na mwenye moyo wa kuwahudumia wengine. Alikuwa mtu wa amani, mnyenyekevu na aliyeishi maisha ya kuwatumikia watu,” amesema Askofu Dkt. Hilinti.

Aidha, Askofu Dkt. Hilinti amewahimiza Watanzania kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na kuheshimiana bila kujali tofauti za dini, makabila au itikadi, akisisitiza kuwa kipimo cha uongozi ni uwezo wa kutumikia watu na si utambulisho wa mtu.

Marehemu Agnes Nasania alifariki dunia Mei 30, 2026 akiwa Diwani wa Kata ya Shelui katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu's post 31/05/2026

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Madukani, wilayani Ikungi mkoani Singida.

Akiwa katika eneo hilo, Dkt. Mwigulu ameagiza kukamatwa kwa mtumishi mwingine wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni anayedaiwa kuhusika katika mtandao wa kulinda na kutetea watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwafuatilia wote waliohusika na wizi wa fedha za umma.

31/05/2026

DKT. MWIGULU AENDELEA KUUFYEKA MTANDAO WA WIZI WA MILIONI 500 MANYONI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kukamatwa kwa mtumishi mwingine wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni anayedaiwa kuhusika katika mtandao wa kulinda na kutetea watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwafuatilia wote waliohusika na wizi wa fedha za umma.

“Mkuu wa mkoa, mtume RPC, huyu naye akamatwe, aunganishwe. Nataka mtandao huu wa mchwa nitimue wote. Sina urafiki wala uungwana na wezi, walaghai, wazembe na wanyang’anyi,” amesema Dkt. Mwigulu.

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo Jumapili Mei 31, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Madukani, wilayani Ikungi mkoani Singida.

31/05/2026

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 31, 2026 anazungumza na wakazi wa Ikungi, Mkoani Singida.

31/05/2026

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 31, 2026 anazungumza na wakazi wa Itigi, Mkoani Singida.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu's post 31/05/2026

DKT. MWIGULU AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA BILIONI 29.6 ITIGI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumapili Mei 31, 2026 amekagua ujenzi wa Barabara ya Noranga (Doroto)–Itigi (Mlongojii) yenye urefu wa kilomita 25 inayojengwa katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kwa gharama ya shilingi bilioni 29.6.

Akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Miradi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Japherson Nnko, Dkt. Mwigulu alielezwa kuwa hadi Mei 30, 2026 mradi huo umefikia asilimia 83.25 ya utekelezaji ambapo kilomita 20.2 zimekamilika kwa kiwango cha lami huku kilomita 4.8 zilizobaki zikiwa zimejengwa hadi tabaka la juu la msingi na zinatarajiwa kukamilika Juni 30, 2026.

Mhandisi Nnko alisema kipande hicho ni sehemu ya Barabara ya Mbeya–Chunya–Makongolosi–Rungwa–Itigi–Mkiwa yenye urefu wa kilomita 524 inayounganisha mikoa ya Mbeya, Singida na Tabora na ambayo inatarajiwa kuimarisha usafirishaji wa watu, bidhaa na mazao katika ukanda huo.

Alisema mradi huo unagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unatekelezwa na Kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) kutoka China kwa gharama ya shilingi 29.6 bila VAT.

Aidha, alisema kazi za ujenzi zilianza Septemba 16, 2022 na zinatarajiwa kukamilika Agosti 7, 2026 baada ya mkandarasi kuongezewa muda wa utekelezaji kwa mujibu wa mkataba.

Katika utekelezaji wake, mradi huo umezalisha ajira 305 ambapo ajira 278 sawa na asilimia 91 zimetolewa kwa wazawa na ajira 27 sawa na asilimia 9 zimetolewa kwa wageni.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Https://www. Pmo. Go. Tz/
Dodoma