Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu

Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu, Public & Government Service, Dodoma.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 07/08/2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi akimfariji Dkt. Fatma Mganga, mjane wa Marehemu Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai, leo tarehe 7 Agosti, 2025 alipowasili nyumbani kwao jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa pole na kushiriki katika maombolezo.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 07/08/2025

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 03/08/2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu ametembelea Banda hilo leo tarehe 03 Agosti 2025.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 29/07/2025

"Watumishi tuongeze bidii, ubunifu na mshik**ano—Kazi zetu zagusa maisha ya mamilioni." — Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu OWM

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 25/05/2025

.
WAZIRI LUKUVI AMUWAKILISHA RAIS SAMIA TABORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Mhashamu Josephat Jackson Bududu.

Ibada hiyo imefanyika leo Mei 25, 2025 katika Kanisa Kuu la Mt. Theresia, Tabora.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 23/05/2025

.
Kikao cha 30 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Bajeti linaloendelea leo tarehe 23 Mei, 2025 jijini Dodoma.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 21/05/2025

.

UZINDUZI WA MWONGOZO WA KITAIFA KWA WATOA HUDUMA ZA MAENDELEO YA BIASHARA

JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 21 MEI, 2025

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 21/05/2025

.
MATUKIO KATIKA PICHA

Kikao cha 29 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Bajeti linaloendelea leo tarehe 21 Mei, 2025 jijini Dodoma.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 20/05/2025

.
MATUKIO KATIKA PICHA

Kikao cha 28 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Bajeti linaloendelea leo tarehe 20 Mei, 2025 jijini Dodoma.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 15/05/2025

.
WAELIMISHA RIKA WATAKIWA KUTUMIA MBINU ZA KISASA KATIKA KUELIMISHA MASUALA YA AFYA KAZINI

Waelimisha rika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watakiwa kutumia mbinu mbadala na zinazokwenda na mazingira ya sasa katika kufikisha elimu ya afya kwa watumishi wenzao kazini huku wakijitolea kwa uzalendo na weledi ili kuendelea kuwa na mazingira mazuri ya utendaji wa kazi kwa kuzingatia afya zao.

Hayo yamebainishwa Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Eleuter Kihwele kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim James Yonazi hii leo Mei 15, 2025, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa waelimisha rika mahala pa kazi, yanayofanyika mjini Morogoro.

Kihwele amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo waelimisha rika katika utoaji wa elimu, hasa katika kipindi hiki ambapo jamii inakumbwa na ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa pamoja na changamoto nyingine za kiafya.

“Mafunzo haya yatakuwa na mada muhimu. Zingatieni ili kuwawezesha watumishi wenzenu kupata uelewa wa kina kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa,” alisema Bw. Kihwele.

Aidha, amepongeza maandalizi ya mafunzo hayo, akisisitiza kuwa yatatoa mwanga na mwelekeo mpya wa kuhakikisha Ofisi ya Waziri Mkuu inakuwa mfano wa kuigwa katika kueneza elimu ya afya kwa watumishi wake.

Kwa mujibu wa Kihwele, mafunzo kwa waelimisha rika hufanyika kila mwaka ili kutathmini utekelezaji wa mwongozo uliopo, kubaini changamoto na kuja na mikakati bora ya kudhibiti magonjwa katika Idara na Vitengo husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Menejimenti ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;Bi. Mwanaamani Mtoo, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendeleza utekelezaji wa mwongozo wa waelimisha rika kwa mafanikio makubwa.

“Sisi k**a wasimamizi wa rasilimali watu, tunawapongeza kwa hatua mliyoifikia. Kuendeleza juhudi hizi ni hatua muhimu ya kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa kazini,” alisema Bi. Mtoo.

Photos from Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Na Uratibu 's post 14/05/2025

MATUKIO KATIKA PICHA

Kikao cha 24 cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Bajeti linaloendelea leo tarehe 14 Mei, 2025 jijini Dodoma.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dodoma