MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KIVUTIO SABASABA
Wadau mbalimbali wamejitokeza kupata elimu kuhusu ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Wizara ya Nishati inaendelea kueleza Mafanikio na Mipango ya kuiendeleza Sekta ya Nishati kupitia Maonesho hayo.
Wizara Ya Nishati
Huu ni Ukurasa rasmi wa Wizara ya Nishati unaolenga kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu Sekta ya Nishati
30/06/2025
DKT. BITEKO ASEMA NISHATI ITAKAYOZALISHWA NA NYUKLIA KUJUMUISHWA KWENYE GRIDI YA TAIFA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Doto amesema kuwa Tanzania inatarajia kuzalisha umeme unaotokana na nyuklia utakaojumuishwa katika Gridi ya Taifa ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme yanayotokana na ongezeko la viwanda.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Juni 30, 2025 Kigali nchini Rwanda wakati akihutubia katika Mkutano kuhusu masuala ya Nyuklia Afrika.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiagiza Wizara ya Nishati chini ya uongozi wangu kuhakikisha kwamba hivi karibuni umeme utakayozalishwa unajumuishwa katika Gridi ya Taifa,” amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa kupitia agizo hilo Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandaa mikakati ya pamoja ya taasisi za Serikali ili kufikia azma ya kuzalisha umeme wa nyuklia kwa kuwa ni nishati yenye unafuu wa gharama kulinganisha na vyanzo vingine vya nishati, pia isiyochafuzi kwa mazingira.
Ametaja baadhi ya jitihada kuwa Juni 2025 Tanzania iliandaa warsha ili kutoa uelewa kwa wadau wa masuala ya nyuklia ikiwa ni pamoja na kuanzisha taasisi itakayoratibu na kusimamia shughuli za nyuklia.
“Serikali yangu itahakikisha inaendeleza mazingira mazuri kwa ajili ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia nyuklia kwa kutunga sera thabiti na kuanzisha mifumo ya sheria na udhibiti kwa ajili ya usimamizi wa raslimali ya nyuklia na uzalishaji wa umeme unaotokana na nyuklia, amesisitiza Dkt. Biteko.
Vilevile amesema Serikali itaongeza raslimali watu wenye ujuzi katika teknolojia za nyuklia ili kutumia kikamilifu raslimali hiyo hususan katika maeneo mengine ikiwemo afya na kilimo.
Amesema tayari Tanzania ina nyaraka mbalimbali zinazoiangazia nyuklia k**a raslimali ya msingi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nishati ya baadae k**a vile Sera ya Taifa ya Nishati, Mkakati wa Nishati Jadidifu na Sera ya Maendeleo ya Madini.
Hata hivyo amesema Serikali ina lengo la kuimarisha Sera ya Teknolojia ya Nyuklia ya mwaka 2013 ili kiakisi maendeleo ya hivi karibuni sambamba na kufuata viwango vya kimataifa.
Akifungua Mkutano huo Waziri Mkuu wa Rwanda Mhe. Dkt. Edward Ngirente amesema kuwa ili kufikia Mpango wa Maendeleo wa Rwanda wa mwaka 2050 wa kuwa nchi ya kipato cha juu wanahitaji kuwa na uzalishaji wa umeme kwa kiasi kikubwa.
“ Hivyo, Rwanda tumeamua kuzalisha umeme wa nyuklia kwa kuwa ni salama na wa uhakika na hauhitaji mvua ili kurahisisha maendeleo kwa kutumia teknolojia,” amesema Mhe. Ngirente.
Aidha, amesema Mkutano huo wa nyuklia utakuwa na manufaa kwa Afrika katika kusaidia maendeleo. Pia nchi za Afrika kwa pamoja lazima ziwe kinara katika matumizi ya nishati safi na kuwa muda wa utekelezaji ni sasa ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira na ongezeko la idadi ya watu.
Waziri Mkuu wa Niger, Mhe. Ali Mahamane Lamine Zeine amesema kuwa nchi yake ina vyanzo vingi vya nishati ikiwemo maji na sasa imezindua mpango wake wa nyuklia hivyo nyuklia ni nishati safi na ina manufaa makubwa katika uzalishaji wa umeme barani Afrika.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Mionzi ya Atomiki Rwanda, Dkt. Lassina Zerbo amesema kuwa Rwanda ipo katika hatua za mwishoni za kuanzisha vinu vya nyuklia vya kuzalisha umeme.
Ameongeza kuwa katika kufikia hatua hiyo ilihitaji dhamira ya viongozi na imani kwa wananchi juu ya umuhimu wa uzalishaji wa umeme wa nyuklia.
Mkutano huo unaofanyika kuanza Juni 30 hadi Julai 1, 2025 nchini humo unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la kuharakisha matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.
30/06/2025
19/06/2025
AFRIKA IPEWE UHURU WA KUZALISHA NISHATI KWA KUTUMIA RASLIMALI ZAKE: DKT. BITEKO
📌Ahimiza Tanzania na Urusi kuendeleza uhusiano wake wa kuheshimiana
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa nchi za Afrika kupewa uhuru wa kuzalisha nishati kwa kutumia raslimali zilizopo barani humo.
Dkt. Biteko ametoa wito huo leo Juni 19, 2025 wakati akizungumza katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg linalofanyika nchini Urusi.
Amesema Afrika inahitaji programu itakayosaidia kufikia dhamira yake ya kuondoa idadi kubwa ya watu ambao hawatumii nishati safi huku akitaja baadhi ya athari za matumizi ya nishati isiyo safi ikiwemo uharibifu wa mazingira.
Ameongeza kuwa Afrika ina vyanzo vingi vya kuzalisha nishati, mfano Tanzania kuna vyanzo k**a vile jua, maji na gesi asilia. Hata hivyo barani humo hakuna uhuru wa kutumia makaa ya mawe licha ya kuwepo kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwa nchi kubwa duniani zinaweza kufanya hivyo.
“ Hivyo iangaliwe namna kwa kila nchi kutumia raslimali zake ili kuzalisha nishati, mfumo uliopo unazifanya nchi zote kuwa sawa lakini ukweli ni kwamba hatuko sawa. Kwa mfano Afrika inachangia asilimia 3 hadi 4 pekee ya uchafuzi wa mazingira, lakini imepewa mzigo mkubwa zaidi.” Amesema Dkt. Biteko.
Amesisitiza” Kila nchi itumie utaratibu wake wa kuzalisha nishati lakini kwa lengo la kupunguza uchafuzi wa mazingira.”
Amezungumzia uhusiano mzuri uliopo wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi na kusema kuwa uendelee kuwa wa kuheshimiana na kukubaliana.
Ambapo ametaja manufaa yake kuwa ni pamoja na kubadilishana ujuzi na kuisaidia Tanzania katika mitaji ya miradi nishati.
Amebainisha kuwa Tanzania ina mpango wa kutumia makaa ya mawe kwa ajili ya kuzalisha takribani megawati 120 za umeme.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Urusi, Mhe. Sergey Tsivilev amesema kuwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Vladimir Putin amekuwa na jitihada mbalimbali za kuhakikisha zinaungana na nchi zingine katika kupatia ufumbuzi changamoto za masuala ya nishati.
Naye, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya African Energy Chamber, Bw. NJ Ayuk amesema kuwa ni muhimu kwa nchi za Afrika na Urusi kuungana na kuhakikisha sauti ya Afrika inasikika na kutekeleza wanayokubaliana ili wote waweze kunufaika na uhusiano kati yao.
Aidha, ameiomba Serikali ya Urusi kuwezesha kampuni kutoka nchini humo ili ziweze kuwekeza zaidi Afrika hususan katika sekta ya nishati.
Pia, ameipongeza Tanzania katika hatua iliyopiga na mafanikio yake katika sekta ya nishati sambamba na kutoa wito kwa nchi za Afrika kujifunza zaidi kutokana na mafanikio yaliyopo nchini Urusi.
Jukwaa hilo la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg linatarajiwa kuwa na washiriki kutoka takribani nchi 140.
07/06/2025
EID MUBARAK
03/06/2025
Wizara ya Nishati Tanzania on TikTok .ya.nishati 2 Followers, 0 Following, 3 Likes - Watch awesome short videos created by Wizara ya Nishati Tanzania
30/05/2025
MAWAZIRI WA NISHATI JUMUIYA YA SADC KUKUTANA NCHINI ZIMBABWE.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameongoza jopo la Wataalam kutoka Wizara ya Nishati katika Kikao cha awali cha Kamati Ndogo ya Nishati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kilicholenga kujadili maandalizi ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Mawaziri wa SADC wanaoshughulikia masuala ya Nishati utakaofanyika nchini Zimbabwe.
Kikao hicho cha awali kimefanyika tarehe 30 Mei 2025 katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.
Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa SADC unatarajia kufanyika nchini Zimbabwe Mei 30 had 04 Juni 2025 ukitanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Nishati wa SADC.
Kikao hicho cha Mawaziri kitajadili ajenda mbalimbali ikiwemo hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika Kanda; Maendeleo ya sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Nishati Safi na kujadili nafasi na utayari wa Kanda katika kutekeleza Azimo la Dar es Salaam lililotokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300.
Washiriki wengine katika kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao wametoka katika nchi zote zilizopo katika Jumuiya ya SADC.
30/05/2025
The Ministry of Energy, in collaboration with the United Nations Capital Development Fund (UNCDF) and with funding from the European Union, is set to launch the National Clean Cooking Communication Strategy alongside the National Clean Cooking Awareness Campaign.
The launch will take place on 2nd June 2025 at the PSSSF Hall, located along Makole Road in Dodoma, starting at 8:00 a.m. The Guest of Honour at the event will be Hon. Dr. Doto Mashaka Biteko, Deputy Prime Minister and Minister for Energy.
You are all warmly welcome!
30/05/2025
Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya inatarajia kuzindua Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji na Uelimishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Uzinduzi huo utafanyika tarehe 2 Juni 2025 katika ukumbi wa PSSSF uliopo Barabara ya Makole jijini Dodoma kuanzia saa 2.00 asubuhi. Mgeni rasmi katika uzinduzi huu ni Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Karibuni sana!
29/05/2025
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza miradi ya umeme katika Vitongoji kwa kuzingatia vigezo vya ziada ikiwemo ukubwa wa vitongoji, ukubwa wa Jimbo pamoja na mahitaji ya kiuchumi na kijamii.
Lengo la kuweka vigezo hivyo ni kuhakikisha kuwa kila jimbo linakuwa na vitongoji vingi vilivyofikiwa na nishati ya umeme.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 29, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Simanjiro, Mhe. Christopher Olesendeka aliyeuliza kwamba Serikali imejipangaje kutekeleza miradi ya Vitongoji kulingana na jiografia ya Wilaya ya Simanjiro ambapo umbali kutoka Kitongoji kimoja hadi kingine ni zaidi ya kilometa kumi.
"Mheshimiwa Naibu Spika, tunatekeleza miradi hii ya Vitongoji kwa kuzingatia vigezo vya ziada, tumeangalia ukubwa wa jimbo husika, ukubwa wa Vitongoji na mahitaji ya kiuchumi na kijamii katika jimbo husika. Niwahakikishie Wabunge mtaona utofauti katika miradi hii tunayoitekeleza hivi sasa." Amesema Kapinga
Akijibu swali la Mbunge wa Nyasa Mhe. Stella Manyanya aliyeuliza kuhusu kitongoji cha Songea Pori kilichopo katika Kijiji cha Lunyele na Kitongoji cha Nindi kilichopo Kijiji cha Konganywita kufikishiwa nishati ya umeme, Mhe. Kapinga amesema Vitongoji hivyo vimefanyiwa upembuzi yakinifu na kubainika vinahitaji njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kati kwa umbali wa kilometa tatu.
Amesema Serikali inatarajia kuvipelekea umeme vitongoji hivyo kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini Awamu ya Pili B (HEP IIB) ambao utekelezaji wake utaanza mwaka wa fedha 2025/2026.
Kuhusiana na kasi ndogo ya Mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme katika Jimbo la Nyasa Mhe. Kapinga amesema tayari Serikali imeshakutana na Mkandarasa na kumuagiza kuweka Wakandarasi wadogo (sub contractors) katika miradi yake anayotekeleza.
Akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Aida Khenani aliyetaka kauli ya Serikali kuhusu kusuasua kwa Mkandarasi ambaye amepewa kazi ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji vilivyozunguka ziwa Tanganyika, Mhe. Kapinga amesema katika utekelezaji wa miradi ya Vitongoji Serikali imehakikisha inawapata wakandarasi wenye weledi.
Kuhusu Wakandarasi ambao wanasuasua, Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kumsimamia Mkandarasi anayetekeleza mradi huo wa umeme kwenye Vitongoji vilivyozunguka ziwa Tanganyika.
Aidha, amemuagiza kuchukua hatua za ziada kwa Mkandarasi huyo kuhakikisha anatekeleza mradi huo kwa haraka na kwa weledi.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Nishati Street, Mtumba
Dodoma
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 16:30 |
| Tuesday | 07:30 - 16:30 |
| Wednesday | 07:30 - 16:30 |
| Thursday | 07:30 - 16:30 |
| Friday | 07:30 - 16:30 |
