BAHI DC

BAHI DC

Share

Tuna tekeleza ila ya chama cha mapinduzi kwa kuwatumikia wanachanchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

01/06/2026

VIJANA PLATFORM waukarikibisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Bahi kupitia Ufunguzi wa kongamano la vijana

Photos from BAHI DC's post 01/06/2026

VIJANA PLATFORM WAMECHAFUA MJI WA BAHI.

Vijana kwa umoja wao ujulikanao k**a "Vijana Platform" wamefanya jogging na kutanda ndani ya Mji wa Bahi kuonyesha bashasha yao na shauku ya ukaribisho wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Bahi 02 Juni 2026.

Photos from BAHI DC's post 01/06/2026

‎VIJANA WAHIMIZWA KUWA WAZALENDO NA KUTUMIA FURSA ZA MAENDELEO

‎Vijana wa Wilaya ya Bahi wamehimizwa kuwa wazalendo, kulinda amani na kutumia fursa mbalimbali za maendeleo zinazotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa

‎Wito huo umetolewa leo tarehe 1 Juni 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi wakati wa Kongamano la Vijana na Uzinduzi wa Jukwaa la Vijana (Youth Platform) la Wilaya ya Bahi, lililowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo lililobeba kaulimbiu isemayo "Vijana Tuyajenge, Tanzania ni Yetu Sote", sambamba na kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru ya mwaka 2026 isemayo "Tanzania ni Yetu Sote, Tushik**ane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo"

‎Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Jane Ng'ondi, amewataka Vijana kuzingatia Maadili ya Taifa, kuunda vikundi, kujisajili na kuanzisha miradi mbalimbali ili kunufaika na fursa zinazotolewa na Serikali

‎"Vijana ni kioo cha taifa letu, tujiepushe na vurugu kwani vurugu zinaharibu amani yetu , tulinde amani ya nchi yetu na tuwe wazalendo," alisema Bi. Ng'ondi

‎Aidha, Bw. Omari Abdullah Pumzi kutoka k**ati ya Vijana Wazalendo, alipokuwa akifafanua kuhusu Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, amewahimiza vijana kutumia Tekinolojia na mitandao ya kijamii kutafuta taarifa na fursa mbalimbali za maendeleo

‎"Wizara zote zinatutegemea sisi vijana Usigombane na watu wewe ng'ang'ania fursa, Fursa haikufuati nyumbani; ifuate mtandaoni, katika ofisi za maendeleo ya jamii na sehemu nyingine zinazotoa huduma za maendeleo," alisema Punai

‎Lengo la kongamano hilo lilikuwa kuchagua viongozi wa Jukwaa la Vijana la Wilaya ya Bahi na kuwawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo katika halmashauri likiambatana na mafunzo kuhusu elimu ya uraia na uzalendo, ujasiriamali, usimamizi wa biashara, elimu ya fedha, upatikanaji wa mikopo na fursa za uwezeshaji wa vijana, pamoja na ushiriki wa vijana katika shughuli za maendelo

Mada hizo zimewasilishwa na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali akiwemo Dkt. Samson Msilu, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Serikali za Mitaa; CPSP Scholastica Nyabweke kutoka Hombolo(lgti)

Photos from BAHI DC's post 31/05/2026
31/05/2026
25/05/2026

Tanzania ni yetu sote tushik**ane kwa pamoja kuleta maendeleo.

21/05/2026

Mwambie mwenzio

17/05/2026

Sikiliza madini kutoka kwa Afisa Elimu ya awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Bahi akiwaonesha walimu wa muhimu WA kufanya tahimini kwa kina.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Info@bahidc. Go. Tz
Dodoma
SLP2993

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00