04/09/2026
UVCCM MKOA DODOMA YAIOMBA CCM KUWACHUKULIA HATUA BAADHI YA WASTAAFU, YAUNGA MKONO KUFUKUZWA NCHIMBI
> • Yasema CCM haiwezi kuvumilia dalili za usaliti kwa baadhi ya wastaafu
> • Wasisitiza kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dodoma, Ndugu Abdulhabibu Mwanyemba amesema Vijana wa mkoa wa Dodoma wanaunga mkono maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM ya kumfuta uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Ndugu Mwanyemba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma, amesema wanampongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi kushika nafasi hiyo na kauli yake ya 'Hawezi kuwazingua Wana na Hawezi kumzingua Mama' ikiakisi kuwa hatowaangusha vijana wa Tanzani pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kuamini katika vijana.
Katika hatua nyingine, Ndugu Mwanyemba amesema Vijana wa mkoa wa Dodoma wanampongeza Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu baadhi ya Wastaafu kukipangia Chama na Serikali vitu vya kufanya pia kutofuata maadili ya Chama cha Mapinduzi.
"Nitumie fursa hii kukiomba Chama cha Mapinduzi kwenda kubadili kidogo suala la maadili ili viongozi hawa wastaafu ambao mara nyingine wanakiuka miiko ya CCM wachukuliwe hatua au kufukuzwa uanachama," amesema Mwanyemba