Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala

Share

ni chombo cha kisheria kilichoundwa kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 2002 kwa lengo la kusimamia, kuratibu na kuendelea Tiba Asili na Tiba Mbadala.

03/02/2024

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza kwenye kikao kilichofanyika tarehe 01-02/02/2024 katika Ukumbi wa SUA Morogoro.

12/08/2022

TANGAZO|Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika.

16/06/2022

Mfululizo wa kozi za kitaalam za uendelezaji wa dawa asilia katika ngazi tofauti tatu, zitakazofanyika katika Taasisi ya Madawa Asili-MUHAS kati ya 3 Oktoba, 2022 mpaka tarehe 21 Octoba 2022.

K**a mwongozo wa kuchagua pendekezo lako soma maelezo haya.


1. Kozi ya kwanza (Ngazi ya Kwanza): ​​ni kwa Wataalam na matabibu wa Tiba asili ambao wana hamu ya kujua ili waweze kufuata Miongozo mizuri ya taaluma yao (Yaani taaluma na ustadi wa taaluma) –inahusisha mihadhara zaidi, kazi za mikono/maabara chache na hutolewa kwa lugha ya Kiswahili; fomu za matangazo na maombi Pakua katika toviti


2. Kozi ya pili (Ngazi ya Pili) ni kwa wale ambao wana hamu ya kujua kanuni za kitaifa na kimataifa zinazosimamia usalama na ubora wa mimea dawa na bidhaa zake –Inahusisha, nusu mihadhara, nusu kazi za mikono/maabara na hutolewa kwa lugha kwa Kiingereza, ingawa lugha ya Kiswahili kutumika pia; fomu za matangazo na maombi pakua katika tovuti

3. Kozi ya tatu (Ngazi ya III) inashughulikia azma ya kuelewa vigezo na taratibu katika kudhibiti ubora na uhakikisho wa ubora wa bidhaa za mimea kutoka kuvuna hadi bidhaa zilizozalishwa ikiwa ni hitaji muhimu la usalama na ubora katika usajili wa dawa. – Inahusisha mihadhara michache, kazi za mikono/maabara zaidi & Imetolewa kwa Kiingereza, ingawa lugha ya Kiswahili hutumiwa pia; Tangazo na fomu za maombi pakua katika tovuti


Pia unaweza fika ofisini kupata form hizi.

Unaweza kupiga simu 0755450465 kwa maelezo zaidi.

Wako mratibu mafunzo ITM
Asante

16/06/2022

Tukutane Saba

30/05/2022

Timu ya wataalamu kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala itaendesha zoezi maalumu la Usajili wa Waganga, Wasaidizi, Vituo/Maduka ya Tiba Asili katika Halmashauri ya Nzega Mji leo tarehe 30/05/2022.

Waganga wote wa Halmashauri ya Vijijini na Nzega Mji wanakaribishwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya zamani kuanzia saa 2:30 asubuhi.

Kazi Iendelee|Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa!

28/05/2022

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaendelea na zoezi la kutatua changamoto mbalimbali za waganga papo kwa papo katika Halmashauri za Mkoa wa Tabora.

Timu ya wataalamu kutoka Baraza imetoa huduma za kusajili waganga, vituo vya tiba asili pamoja na kuhuisha leseni zilizokwisha muda. Aidha, Kaimu Msajili Bw. Ndahani Msigwa alifafanua mambo kadhaa ikiwemo kuhusu usajili wa nyara katika mamlaka husika pamoja na kuhakikisha kila mganga anajiepusha na vitendo viovu.

Zoezi hili litaendelea katika Wilaya za Nzega, Uyui na Tabora Manispaa.

Mashimba Mashimba. Kazi Iendelee|
Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa!

27/05/2022

Waganga wa Tiba Asili wilaya ya Kaliua wakiimba wimbo wa hamasa na burudani huku wakisubiri kupatiwa vyeti vyao vya usajili katika chuo cha Veta-Ulyankulu.

Zoezi ya kuhamasisha usajili wa waganga, vituo pamoja na kuhuisha leseni linaendelea katika Mkoa wa Tabora k**a ifuatavyo

Tarehe 27/05-Wilaya ya Igunga
Tarehe 30/05- Wilaya ya Nzenga
Tarehe 31/05- Wilaya ya Uyui
Tarehe 1-2/06-Manispaa ya Tabora.

Waganga wote katika Wilaya hizo wawasiliane na waratibu ili kupata utaratibu wa kufika na kupata huduma.

Kazi iendelee|Jiandae Kuhesabiwa

07/09/2021

Taarifa kwa waganga na wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala.

22/01/2021

Waganga wa Tiba Asili wakielezea dawa zao katika maonesho ya dawa za tiba asili kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mkoa wa Morogoro.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Traditional And Alternative Health Practice Council
Dodoma

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30