30/06/2023
Asante mungu kwa kunilindaaa adiiii cku nyingine kuufikia mwaka mwingine sio kwa uweza wangu balii ni kwa uweza wakoππππ happy reborn to meππ¨πΏπ’π±
This is Multimedia place of all news and political event's.
30/06/2023
Asante mungu kwa kunilindaaa adiiii cku nyingine kuufikia mwaka mwingine sio kwa uweza wangu balii ni kwa uweza wakoππππ happy reborn to meππ¨πΏπ’π±
17/04/2023
Siku ya Jumanne, Mahak**a ya Juu ya India itaanza kusikiliza hoja za mwisho kuhusu malalamishi kadhaa ya kutaka kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja. Mahak**a imesema kesi hiyo "itapeperushwa mubashara kupitia runinga kwa maslahi ya umma".
17/04/2023
SpaceX Starship: Kampuni ya Elon Musk yaahirisha kurusha roketi kubwa kuwahi kufanyikaMwanaharakati wa upinzani nchini Urusi Vladimir Kara-Murza amehukumiwa miaka 25 jela kwa kosa la uhaini na mash*taka mengine kuhusiana na ukosoaji wa vita vya Ukraine.
17/04/2023
Jaribio la kurusha roketi yenye nguvu zaidi kuwahi kutokea angani limeahirishwa kwa angalau saa 48.
Chombo hicho kinachojulikana k**a Starship, kimetengenezwa na mjasiriamali wa Marekani Elon Musk na kampuni yake SpaceX
10/04/2023
ππ
Robert Mugabe, Rais wa zamani wa Zimbabwe, kupitia kitabu chake βJulius Nyerere, Asante Sanaβ ameacha ujumbe unaoweza kuutafsiri k**a wosia kwa Afrika. Maudhui ya kitabu ni kueleza kinagaubaga mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa ukombozi wa Zimbabwe na bara la Afrika. Katika kitabu hicho, Mugabe aliandika kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa na maono ya mbali kuhusu ukombozi.
Aliwaonyesha wanaharakati waliokuwa wanapigania uhuru wa nchi za Afrika kuwa wangeweza kupata marafiki wa kuwaunga mkono hata nje ya bara hili.
Mugabe amesimulia kwenye kitabu kuwa Mwalimu Nyerere alitumia uhusiano wake mzuri na China kuwaunganisha wanaharakati wa ukombozi Afrika na taifa hilo la Mashariki. Kisha Afrika yote ikawa rafiki wa China.
10/04/2023
Muktasari:
Chadema Mufindi wanatarajia kufanya kampeni maalumu iliyoambatana na mikutano ya hadhara kusajili wanachama wao kwa mfumo wa kidigitali.
MUFINDI. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mufindi kinatarajia kufanya kampeni maalum ya kuwasajili wanachama wao katika jimbo la Mafinga Mjini kwa mfumo wa kidigitali.
Hayo yamebainishwa leo Jumanne AprilI 4,2023 na Katibu wa Chadema Wilayani Mufindi, Jonas Kitiga wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu namna ambavyo wamejipanga kufanya kampeni hiyo.
Aidha Kitiga amesema kuwa usajili huo kwa njia ya Kidigitali utaenda sambamba na mikutano ya hadhara kwa lengo la kuipa nguvu chama hicho ili wananchi waweze kufahamu mambo mbalimbali ambayo yanakihusu pamoja na Serikali yao iliyopo madarakani.
Ijumaa, Aprili 07, 2023
10/04/2023
Muktasari:
Kufuatia hukumu ya mahak**a kuu iliyobatilisha mtindo wa kupita bila kupingwa, Mwanasheria Matoja Kosata ameataka wabunge wote walipatikana kwa mtindo wa kupita bila kupingwa wavuliwe ubunge wao.
Dar es Salaam. Wiki moja baada ya Mahak**a Kuu kutoa hukumu ya kuzuia wagombea nafasi mbalimbali kupita bila kupingwa, mwanasheria Matoja Kosata ameataka wabunge wote walipatikana kwa mtindo huo wavuliwe ubunge wao.
Hukumu hiyo inatokana na kesi namba 19 ya 2021 iliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Joran Bashange.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wabunge waliopita bila kupingwa wako 28.
10/04/2023
Muktasari:
Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo, amesema uamuzi wa Mahak**a Kuu uliotengua utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa umeleta matumaini ya kuwa na uchaguziu ulio huru na wa haki siku za usoni.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo, amesema uamuzi wa Mahak**a Kuu uliotengua utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa umeleta matumaini ya kuwa na uchaguziu ulio huru na wa haki siku za usoni.
Doyo ameyasema hayo leo Jumatano Machi 5, 2023 alipokuwa akichangia mada katika mjadala wa Twitter Space, unaoendeshwa na Mwananchi Communications Ltd uliobeba mada βZuio la wabunge kupita bila kupingwa litachagiza uwezo wa uchaguzi huru 2025?β
Doyo ameseama wanaopenda mambo ya kupita bila kupingwa wamekuwa wakifanya mbinu za kuruhusu mazingira yao na sasa sheria inakwenda kuweka wazi kwamba hakuna kupita bila kupingwa.