11/05/2026
Kuanzia tarehe 04 hadi 08 Mei 2026, Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA, kwa kushirikiana na Kamitei Foundation, imefanikiwa kugawa vitabu vya kufundishia pamoja na vifaa mbalimbali vya elimu kwa shule za msingi zilizopo katika maeneo yetu.
Shule zilizonufaika na zoezi hili ni Mahuninga, Kisilwa, Ihanzutwa, Igomaa, Nyamakuyu, Nyakadete, Mahango, Iheha, Nyakazombe, Magigiwe, Mapogoro A, Mapogoro B, Mlungu pamoja na Msagaji Mpya.
Katika zoezi hilo, zaidi ya vitabu 1,547 viligawiwa sambamba na vifaa vya kufundishia na kujifunzia zaidi ya 4,128, vikiwemo atlas, kamusi, manila paper, paper plates, gundi, cartons za box za chaki chaki pamoja na vifaa vingine muhimu vya elimu.
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inaamini kuwa elimu bora ni msingi muhimu katika kujenga jamii yenye uelewa wa uhifadhi wa mazingira na rasilimali za asili kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kupitia msaada huu, tunalenga kuchochea maendeleo ya elimu sambamba na kuimarisha ushiriki wa jamii katika masuala ya uhifadhi.
Walimu waliopokea vifaa hivyo walitoa shukrani zao za dhati na kuahidi kuwasilisha taarifa hizi kwa Afisa Elimu wa Wilaya ili kuthibitisha mchango mkubwa uliotolewa katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Kwa niaba ya uongozi wa WAGA, tunatoa shukrani za dhati kwa Kamitei Foundation pamoja na wadau wengine wote waliofanikisha zoezi hili muhimu la kusaidia elimu kwa watoto wetu na jamii kwa ujumla.
08/05/2026
Tarehe 5 Mei 2026, Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA ilifanya kikao na kampuni ya carbon Tanzania Mjini Iringa kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mradi wa biashara ya hewa ukaa ndani ya maeneo ya hifadhi.
Kikao hicho kilifanyika katika mazingira mazuri na yenye tija, kikilenga kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za asili pamoja na kutathmini fursa za uwekezaji zitakazonufaisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.
Majadiliano yalijikita katika namna bora ya kuendeleza mradi huo kwa kuzingatia misingi ya uhifadhi endelevu, ushirikishwaji wa jamii, na manufaa ya kiuchumi pamoja na kimazingira yatokanayo na biashara ya hewa ukaa.
Wadau mbalimbali walihudhuria kikao hicho wakiwemo , Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Jamii (CWMAC), Honeyguide foundation,STEP pamoja na mkuu wa idara ya wanyamapori kutoka Wilaya ya Iringa na mufindi
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Carbon Tanzania na wadau wote kwa ushirikiano na mchango wao katika kufanikisha kikao hicho, huku ikiendelea kuhimiza ushirikiano wa pamoja katika uhifadhi endelevu wa mazingira na maendeleo ya jamii.
05/04/2026
Heri ya Sikukuu ya Pasaka! 🐣🌿
Kutoka Waga WMA, tunawatakia Pasaka yenye furaha, amani na matumaini mapya. 💚✨
🌳
04/04/2026
Mnamo tarehe 1 april 2026 Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga ilifanikiwa kufanya kikao cha kikatiba na wajumbe wa Baraza la Jumuiya.
Katika kikao hicho, masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na;Mafanikio yaliyopatikana kupitia ushiriki wa Ranger Challenge 2025/2026, Utekelezaji wa ahadi za mwekezaji, Shughuli zilizotekelezwa katika kipindi cha Januari hadi Machi, Taarifa za fedha (mapato na matumizi)
Wajumbe wa Baraza walipongeza juhudi zote zilizofanyika na maendeleo yaliyopatikana. Aidha, waliomba kuondoka na nakala za taarifa za mapato na matumizi ili waweze kuziwasilisha na kuzichambua katika mikutano yao ya vijiji.
, , , ,
04/04/2026
Mnamo tarehe 1 april 2026 Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga ilifanikiwa kufanya kikao cha kikatiba na wajumbe wa Baraza la Jumuiya.
Katika kikao hicho, masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na;Mafanikio yaliyopatikana kupitia ushiriki wa Ranger Challenge 2025/2026, Utekelezaji wa ahadi za mwekezaji, Shughuli zilizotekelezwa katika kipindi cha Januari hadi Machi, Taarifa za fedha (mapato na matumizi)
Wajumbe wa Baraza walipongeza juhudi zote zilizofanyika na maendeleo yaliyopatikana. Aidha, waliomba kuondoka na nakala za taarifa za mapato na matumizi ili waweze kuziwasilisha na kuzichambua katika mikutano yao ya vijiji. , , ,
21/03/2026
Eid Mubarak! 🌙✨️
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, inawatakia heri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr Waislamu wote.
Tunawatakia nyakati za shangwe, utulivu wa moyo na baraka tele katika siku hii adhimu. Tunahimiza kuendelea kudumisha mshikamano wa kijamii na kujali mazingira yetu, ili kulinda urithi wa asili unaotegemewa na jamii zetu.
❤️
07/03/2026
Kupitia utekelezaji wa Mradi wa SEGA,Tarehe 06 Machi 2026_ Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga kwa kushirikiana na shirika la honeyguide foundation- tulifanikiwa kufanya kikao muhimu na wadau pamoja na wanajamii kutoka vijiji wanachama. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Afisa Wanyamapori wa Wilaya ya Mufindi na watendaji wa vijiji wanachama pia
Kupitia majadiliano ya wazi na ushirikishwaji wa wananchi, walifanikiwa kuunda Kamati ya Maadili na Haki za Binadamu ambayo itashirikiana na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga katika kuimarisha utawala bora, maadili na ulinzi wa haki za binadamu ndani ya shughuli za uhifadhi.
Wananchi walipata nafasi ya kutoa maoni yao kwa uwazi, na wengi walionesha hisia na matumaini makubwa kuhusu hatua hii. Baadhi yao waliipongeza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga kwa kuchukua hatua muhimu ya kuanzisha kamati hii, wakieleza kuwa ni mwanzo mzuri wa kuimarisha uwazi, ushirikishwaji wa jamii na heshima ya haki za binadamu katika uhifadhi.
05/03/2026
Kupitia utekelezaji wa Mradi wa SEGA, kuanzia tarehe 02–04 Machi 2026, Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga kwa kushirikiana na Shirika la Honeyguide walitembelea vijiji vitatu wanachama: Mahuninga, Ihanzutwa na Nyakadete.
Ziara hiyo ililenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya mila na desturi ndani ya eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, pamoja na kuwapa muongozo wa namna ya kupata kibali kabla ya kuingia ndani ya eneo hilo.
Vilevile, katika ziara hizo tuliunda timu za vijana watano katika kila kijiji zitakazosaidia kukabiliana na changamoto ya wanyama wanaoharibu mazao na mifugo.
Tunawashukuru wanajamii kwa mwitikio wao mzuri na ushirikiano waliouonyesha katika kufanikisha zoezi hili.
04/03/2026
Mnamo tarehe 26/02/2026 Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, walifanya ziara katika ofisi za Wembere Hunting Safari.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa ahadi za kimkataba pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za uhifadhi.
Ziara hii inaonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha uwajibikaji, ushirikiano endelevu na maendeleo ya sekta ya uhifadhi kwa manufaa ya jamii na rasilimali zetu
03/03/2026
Heri ya Siku ya Wanyamapori Duniani 2026 kutoka Waga WMA!
Leo tunaadhimisha thamani ya wanyamapori na maliasili zetu katika kuimarisha mifumo ya ikolojia na ustawi wa jamii. Katika Jumuiya ya Waga, ushiriki wa jamii katika uhifadhi umeendelea kuleta matokeo chanya, kulinda rasilimali za asili huku ukichochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Maadhimisho ya siku hii yanatukumbusha kuwa uhifadhi ni uwekezaji wa muda mrefu. Kwa kuendeleza ushirikiano na kulinda bioanuwai yetu, tunahakikisha kuwa rasilimali hizi zinaendelea kunufaisha kizazi cha sasa na kijacho.
01/03/2026
Mnamo tarehe 28 Februari 2026, Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA kwa kushirikiana na Honeyguide Foundation iliendesha mkutano wa wadau wa uhifadhi uliowakutanisha viongozi wa vijiji wanachama, DGOs,wajumbe wa Jumuiya na wadau wengine.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kutambua na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na changamoto za uhifadhi wa wanyamapori, pamoja na kusaini hati ya makubaliano ya utekelezaji wa mikakati hiyo kwa kila mdau. Hatua hii ni sehemu ya kuimarisha uwajibikaji na usimamizi shirikishi wa rasilimali za wanyamapori.
Wadau wote walipongeza hatua iliyofikiwa na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA, wakieleza kuwa ni mfano bora wa ushirikishwaji wenye tija na unaoleta matokeo chanya katika uhifadhi.
Tunatoa shukrani za dhati kwa Honeyguide Foundation na DAWIN Initiative kupitia Mradi wa SEGA kwa ushirikiano na mchango wao mkubwa katika kufanikisha hatua hii muhimu.
Kwa pamoja tunaendelea kulinda rasilimali zetu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.