Nipige TAFU

Nipige  TAFU

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Nipige TAFU, Social service, Umoja, Kasulu.

Ukurasa rasmi wa kikundi jamii chenye usajili namba
KSTC/CBO/1024
(Community Base Organization)
Call/SMS:+255762223499
WhatsApp:+255762223499
Email:[email protected]
Area:Kasulu Kigoma Tz🇹🇿
TUNAGUSWA TUNASAIDIA
#Katilihaendimbinguni🚫

20/05/2026

1.TUUNGANE KUPINGA NDOA ZA UTOTONI

Ndoa za utotoni bado zinaendelea kuwa changamoto kubwa ndani na nje ya taifa letu. Watoto wengi wananyimwa haki yao ya elimu, afya bora na nafasi ya kutimiza ndoto zao kutokana na kuingizwa kwenye ndoa wakiwa bado wadogo.

Tunaziomba serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi wa dini, jamii pamoja na wadau wote wa maendeleo tuungane kwa pamoja kupinga na kutokomeza vitendo hivi. Kila mtoto anastahili kulindwa, kupewa elimu na kuishi maisha salama yenye matumaini ya kesho bora.

✋ Tuseme kwa sauti moja:
“Mtoto ni wa shule na malezi bora, si wa ndoa za utotoni.”






Katilihaendimbinguni

2.🚫LET'S UNITE TO OPPOSE CHILD MARRIAGE

Child marriage continues to be a major challenge within and outside our nation. Many children are denied their right to education, good health and the opportunity to fulfill their dreams due to being forced into marriage at a young age.

We call on governments, non-governmental organizations, religious leaders, communities and all development stakeholders to unite together to oppose and eradicate these practices. Every child deserves to be protected, educated and live a safe life with hope for a better tomorrow.

✋ Let's say with one voice:
“A child belongs to a good school and upbringing, not to child marriage.”

StopChildMarriage
CareForChild
EducationFirst
UniteAgainstViolence
StopChildMarriage
A murderer does not go to heaven.

17/05/2026

1.Tafakari na uchukue hatua ya kuwasaidia wahitaji walioko karibu yako au mbali yako. Hicho kidogo ulichonacho kinaweza kuwa msaada mkubwa sana kwao. Usisubiri kuwa na vingi ndipo utoe msaada — moyo wa kujali ndiyo zawadi ya kweli.

2.Think about and take action to help those in need near or far. The little you have can be a great help to them. Don't wait until you have a lot to help — a caring heart is the true gift.

15/05/2026

Leo Ijumaa tarehe 15 MAY 2026, Mratibu wa Mkono wa Pole, Hongera na Rufaa Ndugu ALPHANCE KACHECHE (KIBUYU) ameongoza tukio la kutoa mkono wa pole kwa mwanachama na Mlezi No.2 wa taasisi yetu Madame GODELLA ATHANASI kufuatia kufiwa na Baba mkwe wake.

Tukio hilo limefanyika nyumbani kwa mlezi ambapo wanachama na viongozi mbalimbali walishiriki kuonesha upendo, mshikamano na faraja katika kipindi hiki kigumu.

Miongoni mwa viongozi na wanachama walioshiriki tukio hilo ni Mwenyekiti wa NIPIGE TAFU GROUP GCO Bosco Rufatiye, Afisa Muhamasishaji ambaye pia ni Kaimu Katibu MULA MULA, pamoja na Madame Neema Kayagambe.

Tunamuombea Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi na kuwapa familia moyo wa subira na uvumilivu. 🙏🕊️

“Ni Familia Moja, Kuelimisha Jamii ni Wajibu Wetu.”



2.Today, Friday, 15 MAY 2026, the Coordinator of the Sympathy, Congratulations and Appeal, Brother ALPHANCE KACHECHE (KIBUYU), led an event to offer a hand of sympathy to member and Guardian No. 2 of our institution, Madame GODELLA ATHANASI, following the death of her Father-in-law.

The event was held at the guardian's home where various members and leaders participated to show love, solidarity and comfort during this difficult period.

Among the leaders and members who participated in the event were the Chairman of NIPIGE TAFU GROUP GCO Bosco Rufatiye, the Promotion Officer who is also the Acting Secretary of MULA MULA, as well as Madame Neema Kayagambe.

We pray to God to grant the deceased a good place in paradise and give the family the heart of patience and tolerance. 🙏🕊️

“We are One Family, Educating the Community is Our Duty.”

10/05/2026

.KHERI YA SIKU YA MAMA DUNIANI

Tunawapongeza na kuwathamini kina mama wote wenye malezi ya heshima, upendo na maadili mema katika jamii.
Hongereni kwa kuendelea kuwa nguzo ya familia, walezi wa watoto, na mfano bora wa tabia njema kwa kizazi cha sasa na kijacho. 🙏

Siku hii maalum iwe pia ukumbusho wa kuthamini utu, heshima na wajibu wa mama katika kulea watoto kwa upendo, kuwakinga dhidi ya ukatili wa aina yoyote, na kuishi maisha yenye staha na mfano mwema kwa jamii.

“Mama mwenye maadili mema huijenga jamii yenye heshima.” ❤️



.

2.HAPPY MOTHER’S DAY IN THE WORLD

We congratulate and appreciate all mothers who have nurtured respect, love and good morals in society.
Congratulations on continuing to be the pillar of the family, the guardians of children, and a good example of good behavior for the current and future generations. 🙏

May this special day also be a reminder to appreciate the dignity, respect and responsibility of mothers in raising children with love, protecting them from any kind of cruelty, and living a dignified life and a good example to society.

“A mother with good morals builds a respectful society.” ❤️



EthicsAndHonor

28/04/2026

1.Kwa masikitiko makubwa, tunatoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia ya wasanii wa Bongo Fleva kufuatia kifo cha msanii SPACK TZ. Taasisi ya inaungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu mzito. Tutaendelea kukumbuka mchango wake kupitia muziki wake uliogusa jamii, ukihamasisha mema na kupinga ukatili. Pumzika kwa amani.

2.With great sadness, extends its condolences to the relatives, relatives, friends and family of Bongo Fleva artists following the death of artist SPACK TZ. The Foundation joins all Tanzanians in mourning this great loss. We will continue to remember his contribution through his music that touched the community, inspiring good and opposing cruelty. Rest in peace.

26/04/2026
14/04/2026

1.Hongera kwa msimamo thabiti, Mh
Ukweli usemwe—taharuki hizi zisizo na msingi hazina nafasi katika jamii yetu. Tusimame pamoja kukemea upotoshaji na kulinda utu wa kila mmoja.


2.Congratulations on your strong stance Mh
The truth be told—these baseless fears have no place in our society. Let us stand together to denounce misinformation and protect each other's dignity.

14/01/2026

Katika kuelekea muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2026, imekabidhi mahitaji mbalimbali yakiwemo vifaa vya shule pamoja na mahitaji yote muhimu ya masomo, sambamba na fedha taslimu kwa ajili ya kugharamia michango mbalimbali inayowakabili wanafunzi. Msaada huo umetolewa na kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

Wanafunzi hao ni wanufaika wa mkono wa nne wa Faraja kwa Jamii na Makundi Maalum chini ya mpango wa “TUNAGUSWA TUNASAIDIA”, wakitokea shule mbili tofauti ambazo ni shule ya Msingi na Sekondari.

Tukio la kukabidhi mahitaji hayo lilifanyika tarehe 12/01/2026, siku ya Jumatatu, katika viunga vya Shule ya Sekondari Murubona. Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji Kasulu , Ndugu Salumu Shaban Massagah, akiambatana na viongozi wengine kutoka Kata ya Murubona, akiwemo Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Misheni ambaye pia ni Kaimu Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Umoja, pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Umoja, Mheshimiwa Richard Martine Kahurananga (CHOBA). Aidha, walihudhuria walimu kutoka Shule ya Msingi Kiganamo na Shule ya Sekondari Murubona, ambako wanafunzi hao wanasoma.

26/12/2025

DONT MISS ☝️

Want your business to be the top-listed Government Service in Kasulu?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Umoja
Kasulu
MURUBONA