27/05/2026
Eid Mubarak!!
MJNLS was jointly established by the Former Liberation Movements of Southern Africa including the CC
27/05/2026
Eid Mubarak!!
With hearts full of gratitude, we extend our sincere appreciation to all liberation movements, facilitators, leaders, organizers, and participants who made the 2026 Workshop for Leading Cadres of Former Liberation Movements of Southern Africa a historic success. Your unity, wisdom, brotherhood, and shared vision for Africa have strengthened the spirit of solidarity and inspired a new generation of leaders committed to protecting the legacy of liberation and building a stronger, united Africa for the future.
23/05/2026
DKT DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO YA VIONGOZI KUTOKA VYAMA SITA RAFIKI KUSINI MWA AFRIKA
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dkt. Mohamed Dimwa Leo tarehe 23 Mei 2026 amehitimisha mafunzo maalum yaliyokuwa yakifanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Mei 2026 kwa viongozi kutoka vyama sita rafiki vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambavyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM - Tanzania), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), na African National Congress (ANC - Afrika Kusini).katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Leadership School uliopo Kibaha Mkoa wa Pwani.
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na kaulimbiu isemayo, “Kusalia Waaminifu kwa Misingi na Dhima Yetu ya Awali, Tukisonga Mbele Pamoja Kuelekea Maendeleo ya Kisasa,” yameelezwa kuwa yamekuja katika wakati muafaka ambapo dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yanayohitaji uimara wa misingi ya vyama vya ukombozi. Viongozi walisisitiza kuwa vyama hivi vina wajibu mkubwa wa kuendelea kulinda mamlaka ya wananchi, kuimarisha mshikamano wa kikanda, na kuhakikisha maendeleo ya nchi zao yanaendelea kujengwa kwa misingi ya uhuru, utu, uzalendo na kujitegemea bila kuendeshwa na misukumo ya kimagharibi inayoweza kupotosha dira ya mataifa yao.
Aidha, imeelezwa kuwa kupitia mafunzo haya na ushirikiano wa kimkakati baina ya vyama hivyo, juhudi zaidi zitaelekezwa katika kuimarisha ideolojia, kukuza uongozi wenye maadili, na kujenga kizazi kipya cha viongozi watakaolinda historia, misingi na malengo ya vyama vya ukombozi vilivyopigania uhuru wa mataifa yao. Viongozi hao wameahidi kuendeleza mshikamano huo wa kihistoria kwa vitendo, wakiamini kuwa umoja wao ndio nguzo ya kudumu ya maendeleo, amani na ustawi wa Kusini mwa Afrika.
MPLA
ANC
23/05/2026
HAFLA YA KUHITIMISHA MAFUNZO YA VIONGOZI KUTOKA VYAMA SITA RAFIKI KUSINI MWA AFRIKA
Leo tarehe 23 Mei 2026, katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Leadership School uliopo Kibaha Mkoa wa Pwani, Imefanyika hafla ya kufunga mafunzo maalum yaliyokuwa yakifanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Mei 2026 kwa viongozi kutoka vyama sita rafiki vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambavyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM - Tanzania), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), na African National Congress (ANC - Afrika Kusini). Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Dkt. Mohammed Said Mohammed (DIMWA) ambaye aliongoza hitimisho la mafunzo hayo yaliyobeba tafakuri ya kina kuhusu mustakabali wa vyama vya ukombozi na uongozi wa kizalendo barani Afrika.
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na kaulimbiu isemayo, “Kusalia Waaminifu kwa Misingi na Dhima Yetu ya Awali, Tukisonga Mbele Pamoja Kuelekea Maendeleo ya Kisasa,” yameelezwa kuwa yamekuja katika wakati muafaka ambapo dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yanayohitaji uimara wa misingi ya vyama vya ukombozi. Viongozi walisisitiza kuwa vyama hivi vina wajibu mkubwa wa kuendelea kulinda mamlaka ya wananchi, kuimarisha mshikamano wa kikanda, na kuhakikisha maendeleo ya nchi zao yanaendelea kujengwa kwa misingi ya uhuru, utu, uzalendo na kujitegemea bila kuendeshwa na misukumo ya kimagharibi inayoweza kupotosha dira ya mataifa yao.
Aidha, imeelezwa kuwa kupitia mafunzo haya na ushirikiano wa kimkakati baina ya vyama hivyo, juhudi zaidi zitaelekezwa katika kuimarisha ideolojia, kukuza uongozi wenye maadili, na kujenga kizazi kipya cha viongozi watakaolinda historia, misingi na malengo ya vyama vya ukombozi vilivyopigania uhuru wa mataifa yao. Viongozi hao wameahidi kuendeleza mshikamano huo wa kihistoria kwa vitendo, wakiamini kuwa umoja wao ndio nguzo ya kudumu ya maendeleo, amani na ustawi wa Kusini mwa Afrika.
MPLA
ANC
23/05/2026
✍✍✍PROF. KABUDI AWAFUNZA VIONGOZI HARAKATI ZA UKOMBOZI NA MIKAKATI KUSINI AFRIKA.
Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (mb) ameshiriki kutoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere amewafunza viongozi vijana kihistoria mitazamo na mikakati ya harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika na Afrika kwa ujumla
23/05/2026
MJNLS Heart of Leadership in six sister Southern African Parties
23/05/2026
MJNLS Heart of Southern Africa Leaders ❤️
23/05/2026
Ambassador Omar R. Mjenga President and Chief Executive Officer, Centre for International Policy Africa Training at Mwalimu Julius Nyerere Leadership School for 2026 Wokshop for Leading cadres of Former Liberation Movements of Southern Africa.
23/05/2026
DAY 7:
Workshop for Leading Cadres of the Former Liberation Movements in Southern Africa - 16th – 25th May 2026