17/01/2025
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeendesha Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi Tanzania (NeST), kwa Wakuu wa Shule, Wahasibu wa Shule, Maafisa Elimu Kata pamoja na Wadhibiti Ubora wa Shule, lengo ikiwa ni kutatua changamoto wanazokutananazo wakati wa kufanya manunuzi kupitia mfumo huo.
Aidha Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kufanya Manunuzi kwa wakati kupitia Mfumo wa NeST ili kuondoa changamoto ya ukamilishaji wa Miradi kwa wakati.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa Siku mbili kuanzia Januari 16 hadi 17, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya kilwa sekondari.
30/09/2024
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WILAYA YA KILWA ATOA SEMINA KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemedi Said Magaro ametoa semina kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi juu ya kanuni na maelekezo yanayoongoza uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 leo tarehe 30 Septemba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilwa, Kilwa Masoko.
Katika semina hii jumla ya wasimamizi wasaidizi 113 kutoka katika kata 23, vijiji 90 na miji midogo 2 wamekula kiapo cha uaminifu na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Alice M. Mkasela, Kisha kupewa elimu juu ya kanuni zitakazo waongoza kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024
Aidha msimamizi wa uchaguzi amewasisitiza wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuwahimiza wananchi katika maeneo yao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura utakaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 20 Octoba 2024 na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 Novemba 2024.
"Serikali za mitaa, sauti ya wananchi, jitokeze kushiriki uchaguzi"
29/09/2024
BONANZA LA KIVINJE KIVINJE JOGGING CLUB LAFANA.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameshiriki katika Bonanza la michezo la Kivinje Jogging mapema leo tarehe 29 Septemba 2024 Kilwa Kivinje.
Hii ni hatua ya kudumisha hali ya amani, umoja na mshikamano baina ya vijana wa Lindi na vijana kutoka sehemu mbalimbali nje ya Mkoa wa Lindi.
Pia Mkuu wa Mkoa huyo amewahimiza wananchi wa Kilwa na Lindi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiri zoezi la uandikishaji wa wapiga kura ifikapo tarehe 11- 20 Octoba 2024 na kupiga kura tarehe 27 Novemba 2024 ili waweze kupata viongozi bora.
Katika Bonanza hilo pia wameshiriki viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemedi Magaro pamoja timu ya waratibu wa Shughuli za uchaguzi ngazi ya Mkoa na Wilaya.
"Serikali za mitaa, sauti ya wananchi, jitokeze kushiriki uchaguzi"
27/09/2024
MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2025
26/09/2024
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WILAYA YA KILWA ATOA MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemedi Magaro ametoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024 kwa wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini, vyama vya siasa na viongozi mbalimbali wa Asasi za kiraia leo tarehe 26 Septemba 2024 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kilwa Masoko.
Hata hivyo Ndg. Magaro ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu taratibu, sheria na kanuni zinazohusiana na zoezi zima la uandikishaji wa wapiga kura ambalo litafanyika kwenye maeneo yote ya wilaya hiyo kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.
Vilevile Msimamizi wa Uchaguzi amesisitiza kuwa wananchi wanaojiandikisha katika zoezi hili ndio watakaopata nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa na zoezi hilo la uandikishaji lina tofauti na lile la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura la uchaguzi mkuu.
Sambamba na yote Ndg. Magaro ametoa rai kwa wananchi wote wa Wilaya ya Kilwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la uandikishaji kwani ni muhimu na ni haki ya msingi kujiandikisha kwa kila mwananchi ili aweze kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
26/09/2024
MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUTOLEWA LEO TAREHE 26 SEPTEMBA 2024 NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA.
25/09/2024
MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO NA KUTEMBELEA MRADI WA BANDARI YA UVUVI WILAYANI KILWA.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wamefanya ziara katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa lengo la kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuboresha na kuendesha uchumi wa bahari (uchumi wa Bluu) katika wilaya hiyo.
Ziara hiyo imefanyika siku ya tarehe 24 september 2024 ikiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika nyanja ya ukusanyaji mapato pamoja na uchumi wa Bluu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Mhe. Mohamedi Usinga amewashukuru Madiwani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa ukarimu wao katika kuupokea ugeni huo.
Aidha madiwani nao walipata nafasi ya kutembelea miradi mingine ikiwemo mradi wa bandari ya uvuvi, ukarabati wa hospitali ya Wilaya (Kinyonga) na ujenzi wa Makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.
21/09/2024
NAFASI ZA UONGOZI ZINAZOGOMBEWA KATIKA SERIKALI ZA MITAA
08/08/2024
TUNAWAKARIBISHA KWENYE BANDA LETU LA HALMASHAURI
YA WILAYA YA KILWA KATIKA MAONESHO YA NANENANE LINDI,
NGONGO UPATE ELIMU BORA YA KILIMO KUTOKA KWA
WATAALAMU WETU