21/10/2026
TIMU YA WATAALAMU KUTOKA OFISI YA RAIS YAWASILI MANISPAA YA LINDI KUKAGUA USIMAMIZI WA AJIRA
Lindi, Oktoba 21, 2026.
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imepokea timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma, kwa ajili ya kukagua na kutathmini usimamizi wa ajira, utekelezaji wa taratibu za kiutumishi na uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utumishi wa umma.
Ukaguzi huo unalenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika usimamizi wa rasilimali watu, ikiwemo matumizi ya mifumo ya taarifa za watumishi, ajira za mikataba, fidia kwa watumishi wanaopata ajali na uzingatiaji wa anuwai za kijamii mahali pa kazi.
Aidha, ukaguzi huo utasaidia kubaini changamoto na kuimarisha haki na maslahi ya watumishi pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Timu hiyo itafanya ukaguzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwa siku nne, kuanzia Oktoba 21 hadi 24, 2026.