Manispaa ya Lindi

Manispaa ya Lindi

Share

This is the official page of Lindi Municipal Council

13/05/2026

Innalillahi wa inna ilaihi raji’un

Pole Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

12/05/2026

T A N G A Z O.

ULIPAJI WA LESENI ZA BIASHARA, USHURU WA HUDUMA, USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI, MABANDA YA BIASHARA, VIWANJA NA TOZO

Photos from Manispaa ya Lindi's post 11/05/2026

ELIMU YA USALAMA BARABARANI NA MAZINGIRA YATOLEWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA AWALI NA MSINGI WAILES

Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Wailes Manispaa ya Lindi wamepatiwa elimu ya usalama barabarani pamoja na uhifadhi wa mazingira kupitia mradi wa ujenzi wa barabara ya Wailes–Mpilipili, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya miundombinu na utunzaji wa mazingira.

Elimu hiyo imelenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa kuzingatia alama za barabarani, namna salama ya kuvuka barabara pamoja na umuhimu wa kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mradi huo.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Ndg. Alusaria Mushi amesema utoaji wa elimu hiyo unalenga kujenga uelewa kwa watoto mapema ili wawe mabalozi wazuri wa usalama barabarani na utunzaji wa mazingira katika jamii zao.

Mradi wa barabara ya Wailes–Mpilipili unatarajiwa kuboresha usafiri na kuongeza maendeleo kwa wakazi wa eneo hilo huku ukihusisha pia utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya usalama na mazingira.

11/05/2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndg. Juma Mnwele, amesema wanahabari wanapaswa kupewa kipaumbele katika upatikanaji wa taarifa muhimu zinazohusu jamii ili waweze kuzifikisha kwa wananchi kwa wakati na usahihi. Aidha, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kuhabarisha na kuelimisha jamii.

11/05/2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndg. Juma Mnwele, akiwa katika mahojiano na Mashujaa FM leo Mei 11, 2026 akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha University of Dar es Salaam Ndaki ya Kilimo pamoja na fursa za ajira, biashara na maendeleo zitakazowanufaisha wananchi wa Manispaa ya Lindi na Mkoa kwa ujumla.


Photos from Manispaa ya Lindi's post 11/05/2026

MKURUGENZI WA MANISPAA YA LINDI AZUNGUMZIA FURSA ZA CHUO CHA UDSM NDAKI YA KILIMO MANISPAA YA LINDI

Leo tarehe 11 Mei 2026, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndg. Juma Mnwele, ametembelea kituo cha redio cha Mashujaa FM na kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya jamii pamoja na utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika manispaa hiyo.

Katika mahojiano hayo, Mkurugenzi ameeleza kuwa ujenzi wa Chuo cha University of Dar es Salaam Ndaki ya Kilimo unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Lindi kupitia ajira, ongezeko la biashara, huduma za kijamii na fursa za elimu kwa vijana wa eneo hilo.

Aidha, amewahimiza wananchi kutumia vyema fursa zitakazotokana na uwekezaji huo mkubwa wa elimu ili kuchochea maendeleo ya Manispaa ya Lindi na Mkoa kwa ujumla.


Photos from Manispaa ya Lindi's post 08/05/2026

KATIBU TAWALA MKOA LINDI AKAGUA MRADI WA MACHINJIO YA KISASA NGONGO

Leo tarehe 8, Mei 2026, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omari ametembelea mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Ngongo, mtaa wa Kiduni kata ya Jamhuri, Manispaa ya Lindi.

Katika ziara hiyo, Bi. Zuwena amepongeza hatua iliyofikiwa ambapo awamu ya kwanza ya mradi huo imekamilika kwa asilimia 100 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.4.

Mradi huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa uchinjaji kutoka ng’ombe 8 hadi 10 na mbuzi 4 hadi 6 wanaochinjwa kwa sasa katika machinjio ya Rasbura, hadi kufikia ng’ombe 50 hadi 100 pamoja na mbuzi 100 kwa siku mara baada ya kukamilika kwake.

Aidha, awamu ya pili ya mradi itahusisha usimikaji wa mitambo na vifaa vya uchinjaji, uchakataji pamoja na uhifadhi wa nyama ndani ya jengo la machinjio, ambapo inatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.5.

Katika ukaguzi huo, Bi. Zuwena aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndg. Juma Mnwele pamoja na wataalamu wa halmashauri.

Photos from Manispaa ya Lindi's post 07/05/2026

MKURUGENZI MNWELE AONGOZA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA LINDI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndugu Juma Mnwele, ameongoza ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika manispaa ya Lindi kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wake unakidhi viwango na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katika ziara hiyo, viongozi na wataalamu walitembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Rutamba unaogharimu shilingi milioni 666.2. Mradi huo umeanza kwa ujenzi wa majengo ya kipaumbele ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, jengo la kufulia, kichoma taka cha kisasa, kibanda cha kuchomea taka pamoja na shimo la kutupia kondo la nyuma la uzazi (placenta pit).

Aidha, Mkurugenzi alikagua ujenzi wa soko la mbogamboga Rutamba lenye thamani ya shilingi milioni 20, linalojengwa katika eneo la heka moja kijijini Rutamba kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ndugu Juma Mnwele amesema halmashauri itaendelea kusimamia miradi yote kwa karibu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi k**a ilivyokusudiwa.

Photos from Manispaa ya Lindi's post 06/05/2026

MANISPAA YA LINDI YAFANYA TATHMINI, YAPIGA HATUA MATUMIZI YA IFTMIS

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imefanya kikao cha tathmini na mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Fedha (IFTMIS), kikilenga kuboresha usimamizi wa fedha na kuongeza uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Kikao hicho kimewakutanisha wataalam wa Halmashauri, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, na kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndugu Juma Mnwele, amesisitiza umuhimu wa watumishi kuelewa kwa kina mfumo wa IFTMIS ili kuimarisha utendaji kazi na kuhakikisha rasilimali za umma zinasimamiwa kwa ufanisi.

Lengo kuu la mafunzo hayo lilikuwa kupitisha na kuongeza uelewa wa maeneo yanayohitaji maboresho ndani ya mfumo huo, ili kuufanya uwe na tija zaidi katika usimamizi wa fedha.

Kwa upande wao, wawezeshaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi walieleza kuwa mfumo wa IFTMIS unasaidia kuongeza ufanisi wa ukaguzi wa fedha na kurahisisha taasisi kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Vilevile, walibainisha kuwa mfumo huo unarahisisha ufuatiliaji wa taarifa za kifedha kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika usimamizi wa fedha za umma, kwa lengo la kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.

Photos from Manispaa ya Lindi's post 06/05/2026

DC MWANZIVA AAGIZA MAAFISA BBT KUBORESHA UZALISHAJI WA KOROSHO LINDI

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, amewataka Maafisa Kilimo wanaotekeleza programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kutumia ipasavyo ujuzi na rasilimali walizonazo ili kuongeza tija na ubora wa zao la korosho.

Agizo hilo amelitoa wakati akifungua mkutano wa Maafisa Kilimo wa BBT ulioratibiwa na Bodi ya Korosho Tanzania, uliowakutanisha wataalamu kutoka Halmashauri ya Mtama na Manispaa ya Lindi.

Katika mkutano huo, washiriki walifanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za kilimo, wakajadili mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili katika kuwahudumia wakulima.

Bodi ya Korosho Tanzania iliwasilisha taarifa ya hali ya uzalishaji wa korosho na kubainisha mikakati ya kuimarisha sekta hiyo, ikiwemo kuboresha huduma za ugani na kuongeza uwezo wa Maafisa Kilimo.

Aidha, maafisa hao walibadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa korosho katika Wilaya ya Lindi.

Mkutano huo umetajwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya korosho kupitia wataalamu wa kilimo chini ya programu ya BBT, inayolenga kuongeza ajira na kukuza uchumi kupitia kilimo chenye tija.

mwanziva

03/05/2026

Kila la Heri kidato cha sita.

Want your business to be the top-listed Government Service in Lindi?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Lindi
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30