Mbulu dc

Call Directions Website Contact the organization

Mbulu dc Ukurasa rasmi wa Halmashauri ya Wilaya ya mbulu

DC KAMBANGWA APONGEZA JITIHADA ZA KAMATI YA MAAFA KATIKA KUJIWEKA TAYARI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑOMkuu wa...
12/10/2026

DC KAMBANGWA APONGEZA JITIHADA ZA KAMATI YA MAAFA KATIKA KUJIWEKA TAYARI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Mbwana Kambangwa, amepongeza jitihada zinazochukuliwa na Kamati ya kukabiliana na Maafa ya Halmashauri ya Wilaya katika kubaini maeneo hatarishi na kuandaa mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño.

Mhe. Kambangwa ametoa pongezi hizo leo tarehe 12/10/2026 wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yenye changamoto ndani ya Wilaya ya Mbulu, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na timu ya kukabiliana na maafa, kwa lengo la kujionea hali halisi ya maeneo hayo na kutathmini hatua zinazochukuliwa katika kujiandaa kukabiliana na athari za mvua kubwa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya alisema, “Nipongeze jitihada mlizochukua na mnazoendelea kuchukua kwa kuainisha maeneo hatarishi na kutoa uelewa kwa wananchi. Elimu iendelee kutolewa kupitia mikutano ya vijiji ili wananchi wafahamu namna ya kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.”

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maeneo hatarishi, kuzingatia taarifa za tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika na kuchukua hatua mapema ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa madhara kwa maisha ya watu, mali na miundombinu.

Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi, wataalamu na wananchi ni muhimu katika kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na maafa. Hivyo, ameitaka Kamati ya kukabiliana na Maafa kuendelea kuratibu hatua za tahadhari na kuhakikisha elimu inawafikia wananchi kupitia mikutano ya vijiji na njia nyingine za mawasiliano.

Timu ya kukabiliana na maafa inaendelea kushirikiana na viongozi na wadau husika katika kubaini changamoto zilizopo katika maeneo mbalimbali na kuhamasisha wananchi kuchukua hatua za kujikinga na athari za mvua kubwa.

DC KAMBANGWA ASISITIZA UWAZI WA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA KATIKA VYOMBO VYA HUDUMA YA MAJIMkuu wa Wilaya ya Mb...
12/10/2026

DC KAMBANGWA ASISITIZA UWAZI WA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA KATIKA VYOMBO VYA HUDUMA YA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Mbwana Kambangwa, amesisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma ili kuondoa manung’uniko kwa wananchi na kuimarisha imani yao kwa vyombo vinavyotoa huduma ya maji.

Mhe. Kambangwa ameyasema hayo leo, Oktoba 12, 2026, wakati akifungua kikao cha utambulisho na kujengeana uelewa kwa kamati tendaji za Vyombo vya watoa huduma ya Maji ngazi ya jamii (CBWSOs), kilichoandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Kikao hicho kimehusisha ofisi ya Mkuu wa wilaya na kamati ya usalama wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi mtendaji, viongozi kutoka Ruwasa na wawakilishi wa vyombo 10 vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii, ambapo saba vinahudumia maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na vitatu Halmashauri ya Mji wa Mbulu.

Vyombo hivyo vimeundwa kwa makubaliano ya jamii husika na kusajiliwa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira, vikiwa na jukumu la kuwakilisha wananchi katika usimamizi na utoaji wa huduma ya maji.

Aidha, Mhe Kambangwa amevipongeza vyombo viwili vilivyokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kupata hati safi, akieleza kuwa matokeo hayo ni kiashiria cha uzingatiaji wa taratibu za usimamizi wa fedha na misingi ya utawala bora.

Amesisitiza kuwa viongozi na kamati tendaji za vyombo hivyo wanapaswa kusimamia mapato na matumizi kwa uwazi, kuweka kumbukumbu sahihi za fedha na kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu namna fedha zinavyokusanywa na kutumika, ili kuimarisha uwajibikaji na kuzuia malalamiko yasiyo ya lazima.

Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za RUWASA za kuimarisha uelewa wa viongozi wa vyombo vya huduma ya maji kuhusu majukumu yao, usimamizi bora wa rasilimali na uwajibikaji kwa jamii wanazozihudumia.

Fainali za Nuwas Jimbo Cup 2026 zimetamatika jana Oktoba 10,2026. Fainali hizo zimefanyika katika Tarafa ya Dongobesh.Mg...
11/10/2026

Fainali za Nuwas Jimbo Cup 2026 zimetamatika jana Oktoba 10,2026. Fainali hizo zimefanyika katika Tarafa ya Dongobesh.

Mgeni rasmi kwenye fainali hizo ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Mbwana Kambangwa ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Ndugu Paulo Bura.

Katika fainali hizo Mshindi wa kwanza aliondoka na kombe na zawadi ya Shilingi Milioni 1.5, Mshindi wa pili Shilingi Milioni 1 na mshindi wa tatu laki 8.

Timu ya mpira ya Dongobesh FC iliibuka Mshindi wa kwanza huku timu ya Bashay FC ikichukua mshindi wa pili na Stendi FC kutoka Muslur ikiibuka mshindi wa tatu.

Mwisho fainali hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Yeconia Deles, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Abubakar Kuuli na Waheshimiwa Madiwani kutoka Kata za Tarafa ya Dongobesh.

Manyara Rs
Mhe. Dkt. Emanuel Nuwas
Abubakar Kuuli

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo tarehe 10 Oktoba 2026, wameshiriki kufanya usafi wa pamoja kusafisha mae...
10/10/2026

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo tarehe 10 Oktoba 2026, wameshiriki kufanya usafi wa pamoja kusafisha maeneo ya mji wa Dongobesh.

Usafi huo umehusisha kusafisha mifereji,kuzoa taka na kuzibua mifereji.

Aidha, usafi huo umefanyika ikiwa ni maandalizi ya kukabiliana na athari zitakazoweza kusababishwa na mvua za El Nino kwa kuhakikisha mifereji yote inakua safi.

Mvua za El Nino zinatarajiwa kunyesha kuanzia mwezi Oktoba 2026 hadi mwezi Januari 2027.

Manyara Rs
Maelezo News
Abubakar Kuuli
MBUNGE JIMBO LA MBULU VIJIJINI

Kamati ya kukabiliana na maafa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo Oktoba 7, 2026 imefanya ziara ya kukagua maeneo yanayo...
07/10/2026

Kamati ya kukabiliana na maafa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo Oktoba 7, 2026 imefanya ziara ya kukagua maeneo yanayoweza kupata athari za mafuriko ya mvua za El-Nino.

Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Shule ya Msingi Bashay, Shule ya Msingi Mangisa, kaya zinazoishi pembezoni mwa Mto Yaeda, kata ya Tumati na Stendi ya mabasi Dongobesh.

Wakiwa katika ziara hiyo, kamati imewaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kuwataarifu Wananchi wote wanaoishi mabondeni kuhama kwa kuwaandikia barua na kuitisha mikutano ya Vijiji na Vitongoji.

Pia imewataka Wananchi wahifadhi chakula sehemu salama na za juu kabla ya Mvua kuanza.

Aidha, kamati imewasihi Wananchi kusaidia nguvu kazi kwenye kuzibua mitaro na kufanya usafi ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na Mvua za El Nino.

Mvua za El Nino zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya Mwezi Oktoba,2026 na kumalizika Januari 2027.

Manyara Rs
Maelezo News
Abubakar Kuuli
MBUNGE JIMBO LA MBULU VIJIJINI

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Mbwana Kambangwa leo Oktoba 5, 2026 ameapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Martine Shig...
05/10/2026

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Mbwana Kambangwa leo Oktoba 5, 2026 ameapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Martine Shigela tayari kwa kuanza rasmi kazi ya kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Mbulu.

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,dini na mila.

Pamoja Tunaijenga Mbulu Yetu.

Manyara Rs
Michael Semindu
Abubakar Kuuli

Kila la Kheri darasa la nne katika Mitihani yenuManyara Rs Abubakar Kuuli
05/10/2026

Kila la Kheri darasa la nne katika Mitihani yenu

Manyara Rs
Abubakar Kuuli

Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu (Mbulu DC) lililopo kwenye kata ya Dongobesh.  Pamoja Tunaijenga Mbulu Yetu.Many...
02/10/2026

Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu (Mbulu DC) lililopo kwenye kata ya Dongobesh.

Pamoja Tunaijenga Mbulu Yetu.

Manyara Rs
Maelezo News

TANGAZO TANGAZOTangazo la Ajira ya MkatabaManyara Rs Maelezo News Mhe. Dkt. Emanuel Nuwas Abubakar Kuuli
30/09/2026

TANGAZO TANGAZO

Tangazo la Ajira ya Mkataba

Manyara Rs
Maelezo News
Mhe. Dkt. Emanuel Nuwas
Abubakar Kuuli

Address

Mbulu
Manyara

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255743583078

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbulu dc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mbulu dc:

Shortcuts

Share