Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame

Share

Hivi sasa eneo hili tumelitenga kwa ajili ya uhifadhi, usimamizi na matumizi endelevu ya wanyamapori.

Jumuiya yetu ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame ilianzishwa baada ya vijiji vitano vya wafugaji kuungana ili kulinda eneo letu la marisho ya mifugo dhidi ya kilimo cha mazao.

05/04/2026

Heri ya Sikukuu ya Pasaka! ๐Ÿฃ๐ŸŒฟ

Makame WMA tunawatakia Pasaka njema iliyojaa upendo, amani na matumaini mapya. ๐ŸŒ…โœจ

Katika msimu huu wa kusherehekea sikukuu ya Pasaka, tukumbuke pia kulinda na kuthamini mazingira yetu na urithi wa asili unaotuzunguka kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho. ๐ŸŒ๐Ÿ’š

๐ŸŒณ

21/03/2026

Eid Mubarak! โœจ๏ธ๐ŸŒ™

Jumuiya ya Makame inapenda kuwatakia Waislamu wote Sikukuu njema ya Eid al-Fitr, baada ya kukamilisha ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Siku hii iwe chanzo cha furaha, amani na mshik**ano miongoni mwetu, huku ikiimarisha moyo wa kujali na kuhifadhi rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Ushirikiano wenu ni nguzo muhimu katika kulinda urithi wetu wa mazingira.

Photos from Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame's post 05/03/2026

Ujumbe ni mfupi lakini wenye nguvu: Kubadili simulizi la uhifadhi: Ni jukumu la kila mtu barani Afrika na kwingineko.

Katika mkutano wa Business of Conservation Conference, viongozi wetu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Bw. Lendukushi Keiya, na Afisa Tawala na Rasilimali Watu, Bw. Mitiaki Nairaba, wamehudhuria kuonyesha kuwa kuwawezesha jamii za wenyeji si mbadala wa uhifadhi, bali ndiyo mkakati wenye ufanisi zaidi katika kulinda mandhari pana na muhimu ya Afrika kwa kuonesha mfano wa jinsi gani Makame WMA kwa kushirikiana na wadau wengine k**a Honeyguide Foundation na Carbon Tanzania wanavyofanya vyema katika hili.

Kwa pamoja tunaweza kulinda urithi wa asili wa Afrika kwa vizazi vya sasa na vijavyo. ๐ŸŒ๐ŸŒฟ

************

The theme is short but powerful: Changing the conservation narrative: It is everyoneโ€™s responsibility in Africa and beyond.

At the Business of Conservation Conference, our leaders, Chairman of the Board of Trustees Mr. Lendukushi Keiya and Administration and Human Resources Officer Mr. Mitiaki Nairaba are participating to demonstrate that empowering local communities is not an alternative to conservation but the most effective strategy for protecting Africaโ€™s vast and vital landscapes.

They are also showcasing how Makame WMA, in collaboration with various conservation partners like Honeyguide Foundation and Carbon Tanzania, is successfully putting this approach into practice.

Together, we can protect Africaโ€™s natural heritage for present and future generations. ๐ŸŒ๐ŸŒฟ

03/03/2026

Heri ya Siku ya Wanyamapori Duniani 2026! ๐Ÿ˜

Siku hii muhimu inatukumbusha thamani kubwa ya wanyamapori na maliasili zetu katika maisha ya kila siku. Wanyamapori ni urithi wetu wa asili, chanzo cha ajira na kipato, na nguzo ya utalii na maendeleo ya kiuchumi. Kulinda viumbe hawa ni kulinda mizani ya mazingira na ustawi wa jamii zetu.

Maadhimisho ya leo yanatuhamasisha kuendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi bioanuwai kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Kwa kushirikiana k**a jamii, taasisi, na wadau wa uhifadhi, tunaweza kuhakikisha kuwa rasilimali hizi zinaendelea kuwepo na kunufaisha taifa letu kwa miaka mingi ijayo.

Picha na: .dalmasso

Photos from Tanzania Wildlife Management Authority - TAWA's post 12/02/2026

Asanteni sana Tanzania Wildlife Management Authority - TAWA kwa makala ya kuvutia inayoelezea juhudi na mafanikio ya Jumuiya yetu katika uhifadhi wa wanyamapori na misitu. Ni kweli, kwetu uhifadhi si nadharia, ni wajibu, ni uchumi, ni maisha. Pamoja tunahifadhi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Photos from Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame's post 04/02/2026

Hongera kwa Anderson Nambunga, mshindi wetu katika Chemsha Bongo ya (Facebook).

02/02/2026

"....Sisi tumefurahi, tumefurahi kuwa serikali imetambua na kuthamini jitihada za jamii katika uhifadhi wa wanyamapori na misitu ...." Sehemu ya nukuu kutoka kwa Supuk Olekao, Katibu Jumuiya yetu ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame (Makame WMA) mara baada ya kupokea tuzo ya Jumuiya Bora katika tuzo za zilizoandaliwa na

Photos from Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame's post 01/02/2026

Wapendwa wahifadhi na wadau wengine muhimu!

Tunayo furaha kubwa kutangaza kuwa Jumuiya yetu ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame (Makame WMA) imeibuka mshindi wa Tuzo za Serengeti 2025 (Serengeti Awards 2025). Mafanikio haya ni matokeo ya ushirikiano imara na kujitolea kwa wanajamii wetu, mamlaka za serikali za vijiji, Viongozi na wataalamu wa Wilaya yetu ya Kiteto , mashirika yasiyo ya kiserikali tunayoshirikiana nayo, wawekezaji pamoja na wafanyakazi wa Makame WMA. Umoja, umiliki, na kujitolea kwa jamii yetu katika uhifadhi ndio imekua misingi ya mafanikio haya.

Tuzo hii inathibitisha kwamba jamii za wenyeji zina uwezo wa kusimamia rasilimali za wanyamapori kwa uwajibikaji na kufaidika kwa njia endelevu kupitia shughuli za uhifadhi wa wanyamapori na mazingira kwa ujumla.

Jumuiya ya Makame inatoa shukrani za dhati kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, na wadau wote kwa mwongozo, uaminifu, na msaada wenu endelevu. Tuzo hii ni yetu sote tulio na ndoto moja ya uhifadhi endelevu na maendeleo ya jamii.

"Uhifadhi wetu, urithi wetu".

| | | |

01/01/2026

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame inawatakia Heri ya Mwaka Mpya 2026 uliojaa furaha na mafanikio! ๐ŸŽ†

25/12/2025

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame inawatakia heri ya Krismasi ๐ŸŽ„na msimu mwema wa sikukuu.

09/12/2025

Heri ya siku ya uhuru. Tunawatakia watanzania wote maadhimisho mema ya miaka 64 ya uhuru.

27/11/2025

Uhifadhi endelevu huanza pale jamii inapokuwa katika kitovu cha uhifadhi.

Hivyo, unadhani kwa nini ushiriki wa wananchi (jamii) ni muhimu katika uhifadhi wa eneo letu la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame?

Shiriki (share) nasi maoni yako, tunakusikiliza!

Want your business to be the top-listed Government Service in Manyara?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


P. O. Box 153, Kibaya-Kiteto
Manyara