01/12/2025
Wote Mnakaribishwa
Ukurasa rasmi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
01/12/2025
Wote Mnakaribishwa
27/11/2025
FIFA YATOA MAFUNZO YA GRASSROOT MANYONI – KAIMU MKURUGENZI C. KISWAGA AFUNGA RASMI
Manyoni, 27 Novemba 2025
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Bw. Cainan Kiswaga, leo amefunga rasmi mafunzo ya Grassroot yaliyoendeshwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa kushirikiana na TFF, kwa walimu wa michezo na makocha wa ngazi ya jamii.
Mafunzo hayo ya siku 5 yamefanyika wilayani Manyoni kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu na makocha juu ya mbinu bora za kufundisha mpira wa miguu kwa watoto na vijana wadogo kuanzia ngazi ya msingi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo, Bw. Kiswaga aliipongeza FIFA na TFF kwa kuchagua Manyoni kuwa sehemu ya mpango huo wa kukuza soka la vijana, na kusisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano ili vipaji vipatikane mapema na kulelewa kitaaluma.
"Grassroot ni msingi wa mafanikio ya mpira wa miguu wa taifa. Tunapowajengea uwezo makocha hawa, tunajenga kesho ya soka la Tanzania," alisema Kiswaga.
Washiriki waliopata mafunzo wamesena kuwa mafunzo hayo kwao imekua ni bahati na kitu muhimu kwao na kuahidi kuendeleza walichojifunza kwa vitendo mashuleni na katika jamii zao.
Kwa upande wake, Raymond Gweba Mkufunzi wa FIFA, aliyeongoza mafunzo hayo, alitoa pongezi kwa Halmashauri ya Manyoni ikiongozwa na Mkurugenzi kwa maandalizi mazuri na ushirikiano mkubwa walioupata kutoka kwa washiriki.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida Hamisi Kitila amewashukuru TFF kwa kukubali kuja kutoa Mafunzo hayo na ameshukuru pia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kuwapongeza waliopata mafunzo.
"Nawapongeza sana kwa mafunzo haya mliyoyapata kwa Siku hizi na sasa k**a Mkoa tutarajie Mapindizi makubwa kwenye Mpira wa Miguu"
17/07/2025
Bado Siku 07 Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarehe 24 JULAI 2025
Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru yanafanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tambukareli
Wananchi wote Mnakarbishwa 🇹🇿
TAARIFA KWA UMMA/ VYOMBO VYA HABARI
Mhe. Dkt Vincent Mashinji Mkuu wa Wilaya ya Manyoni akizungumza na Wananchi wa Manyoni kupitia Vyombo vya Habari kuwataarifu juu ya Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 katika Wilaya ya Manyoni
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni utapokelewa kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tambukareli na Mkesha utakuwa Katika Uwanja wa Jumbe
Wananchi wote Mnakarbishwa 🇹🇿✍️
16/07/2025
Bado Siku 8 Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 24 JULAI 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Utatembelea, Utakagua, Utaweka Mawe ya Msingi na Kuzindua Miradi Mbalimbali, Lakini pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge atatupa Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2025 🇹🇿✍️
Wananchi wote Mnakarbishwa
13/07/2025
Uzinduzi wa Ligi ya Mwenge wa Uhuru 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarehe 14 JULAI Siku ya Jumatatu kuanzia saa 8:00 Mchana katika Uwanja wa Jumbe na Mgeni Rasmi atakua ni Mkuu wetu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji..... Wananchi Wote Mnakarbishwa 🇹🇿✍️
Kauli Mbiu: Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu 🇹🇿✍️
Nikukumbushe tuu kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tunatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 24 JULAI 2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chikuyu na Mkesha utakua Katika Uwanja wa Jumbe Manyoni.
12/07/2025
Kuelekea Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 24 JULAI 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Tutakua na Makongamano ya Vijana kujadili Mambo Mbalimbali k**a ilivyoainishwa Ili kubadilishana Mawazo na kujifunza.
Tarehe 14 Siku ya Jumatatu tutakua na Kongamano litakalofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Solya kuanzia saa 8:00 Mchana
WOTE MNAKARIBISHWA 🇹🇿✍️
07/07/2025
Heri ya Sikukuu ya Sabasaba 2025
06/07/2025
Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarehe 24 JULAI 2025
Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki 🇹🇿✍️
| Monday | 07:30 - 15:30 |
| Tuesday | 07:30 - 15:30 |
| Wednesday | 07:30 - 15:30 |
| Thursday | 07:30 - 15:30 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |