Sukamahela the Great

Sukamahela the Great

Share

Wellcome/Karibu Suk**ahela the great ili tujuane, tujuzane habari, historia, jiografia na mambo kemk

28/02/2018

ucku mwemaaaa...

25/12/2017

CHRISTMAS ni MUUNGANO wa maneno mawili yaani *CHRIST + MAS.*

Hapo zamani, siku ya Tarehe 25 December, ilikua siku ya Kusherehekea MATAMBIKO YA KIPAGANI kabla MWANA WA MUNGU, YESU KRISTO hajazaliwa.

Baadae mwaka 533 AD, Mtakatifu Constantine, aliyekua Mkuu wa Kanisa la WARUMI, ambalo siku hizi linajulikana k**a Kanisa la Katoliki (Kanisa la kwanza), aliibadili siku hiyo isiwe tena ya MATAMBIKO YA KIPAGANI badala yake siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa MKOMBOZI MWANA WA MUNGU YESU KRISTO na kuiita *Siku ya kusanyiko la KRISTO* yaani *CHRISTMAS.*

1. *CHRIST* ni neno la kiingereza ambalo tafsiri yake ni KRISTO yaani MASIA au MPAKWA MAFUTA au ALIYETENGWA KWA KAZI MAALUMU.

2. *MAS* ni neno la KIYUNANI ambalo maana yake ni *KUSANYIKO.*

Kwa hiyo maana ya neno CHRISTMAS ni *KUSANYIKO la KRISTO.*

Kwa *WAKRISTO* wanaoamini siku hiyo, wawe makini sana na neno *X-MASS!.*

Inaaminika kuwa, baada ya siku hiyo ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO, kupata umaarufu, neno X-MASS, lilikuja baadae sana na lililetwa na wapinga KRISTO ambao waliamua kufuta neno *CHRIST* kwa kuweka alama ya *“X”* yaani hakuna KRISTO.

Hiyo ilibadili maana kwa kusomeka *X-MASS.*

X-HAKUNA na MASS-KUSANYIKO, hivyo X-MASS, maana yake ni HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO! Yaani HAKUNA CHRISTMAS!
Sasa, K**a wewe ni Mkristo hutakiwi kutumia neno X-MAS, badala yake tumia neno CHRISTMAS

MUNGU awabariki muwe na maandalizi mema ya *CHRISTMAS* na sio *“X-MASS!”*

c&p

23/04/2017

SIMULIZI FUPI YAKIJANA MMOJA..
Likizo moja kijana mmoja aliamua amchukue rafiki yake na kwenda wote kukaa nyumbani kwao kwani ilikuwa ni likizo ya muda mfupi na rafiki yake anakaa mji mmoja uliopo mbali na chuo chao hivyo ingekuwa ni gharama kwenda kwa muda mfupi na kisha kurudi.
Mama wa kijana yule alifurahi sana na kumpokea rafiki wa mwanae na kuandaa chakula kizuri na kisha kumwandalia sehemu ya kulala katika chumba cha wageni.
Baba wa familia ile yeye alikuwa ni mfanya biashara maarufu wa eneo lile na kwa habari za mitaani ilisemekana kuwa alikuwa akitumia ushirikina kwa kufanya sadaka za damu za watu ili aweze kujipatia utajiri zaidi.
Baada ya kugundua yule mgeni yupo pale akapanga na vijana wake wa kazi kuwa usiku wamchukue yule kijana na kumuua ili akamilishe sadaka ya mwaka huo kwani sadaka hiyo haikutakiwa kuangamiza wanafamilia wake bali watu wengine.
Usiku wa manane wale vijana wakaja na kwenda kwenye kile chumba na kumuua yule mtoto k**a walivyoagizwa na bosi wao na kisha kumchukua na kwenda kumweka walikoelekezwa.
Mzee akaamka asubuhi na mapema na kwenda kuangalia ile maiti na kufika kule hakuamini kuona ni mwanae aliyeuawa kwani usiku wakati wa kulala mtoto aligundua kuwa kile chumba kina tatizo la umeme na kuona sio busara kumwacha mgeni alale bila taa hivyo wakabadilishana vyumba na mgeni kulala chumba chake.
Mzee yule alianguka na kufa muda mchache akiwa anakimbizwa hospitali kwa ajili ya presha kuwa juu.
Nami nakuombea rafiki yangu usomaye ujumbe huu kuwa kila mwenye roho mbaya na ya kukudhuru wewe, familia yako, kazi zako au mafanikio yako ashindwe na kuaibika kabla ya mwaka huu haujaisha
Kila mpango mbaya dhidi yako na uwarudie mara mbili hao waliopanga kukudhuru.
Na kila shetani anayetaka kukuharibia mipango yako afe kwa sumu ya nguvu za Mungu k**a huyu Baba.
Naomba haya kwa kuamini Mwenyezi Mungu atatulinda na kututetea daima.
SHARE UJUMBE HUU NAMUNGU AKUPE BARAKA ZAKE..

25/01/2017

Habariii!

28/12/2016

HIVI KWANZA MNAJUA ASILI YA KABILA LA
WAGOGO!!!!!??
KARIBUNI,
Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila
kubwa la Tanzania ya kati, wenyeji wa mikoa ya
Dodoma na Singida. Wanakadiriwa kuwa zaidi ya
1,500,000.
Lugha yao ni Cigogo (kwa Kiswahili hutamkika
Kigogo).
Dini ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa
madhehebu ya Anglikana, halafu wa Kanisa
Katoliki.
Historia na maendeleo ya Wagogo viliathiriwa
sana na ukame na biashara ya watumwa, kiasi
kwamba hata leo ni kati ya makabila fukara zaidi
nchini Tanzania.
UTAWALA WA JADI
Wagogo walikuwa wakiongozwa na mtu aliyeitwa
Mtemi. Watemi kadhaa waliongoza kabila hilo
kabla ya mfumo wa uongozi kuvurugwa na
ukoloni.
Mtemi wa mwisho aliitwa Mazengo ambaye
alitokea katika kijiji cha Mvumi, wilaya ya
Dodoma vijijini.
NYUMBA ZA ASILI
Wagogo wamekuwa wakijenga nyumba ambazo
huitwa tembe"kwa kigogo itembe". Tangu zamani
kuta za tembe zilijengwa kwa fito (sito kwa lugha
yao) zilizosukwa kwa kupisha kuzuia mwanga na
maji. Vipande vya kuta vilivyosukwa kwa sito
vinaitwa "izizi".
Tembe huezekwa kwa udongo ambao hushikiliwa
na miti midogo midogo (walo). Walo huwa
unashikiliwa na miti mikubwa kidogo (mahapa) na
mahapa hushikiliwa na miti mikubwa (michichi).
Michichi ambayo ndiyo hubeba uzito wote
hushikiliwa na nguzo kubwa za miti imara na
migumu. Nguzo hizo hutiwa masumbili.
Kwa miaka ya karibuni kuta za tembe hujengwa
pia kwa matofali yanayotengenezwa kwa udongo.
SHUGHULI ZA UCHUMI
Wagogo ni miongoni mwa makabila ya Wakulima
na Wafugaji kwa asili na hufuga mifugo k**a
ng'ommbe, mbuzi na kondoo, kwa Kigogo
wanyama hao huitwa "ng'ombe, mhene na
ngholo" pamoja na punda "ndogowe" kwa ajili ya
ubebaji mizigo na wakati mwingine kulimia
wakitumika kukokota majembe ya kukokotwa,
k**a watumikavyo ng'ombe pia. Smbamba na
shughuli hiyo kilimo ndio shughuli kubwa na ya
wengi ijapokuwa kwa miaka mingi imekuwa
ikiathiriwa na kiwango kidogo cha mvua
zinazonyesha kutokana na jiografia ya Mikoa hiyo
miwili, yaani, Dodoma na Singida.
Mazo yanayolimwa kwa wingi ni mahindi
"mtama", mtama '[[uwele, na lugugu]. Siku za
hivi karibuni umeingia mtama unaokomaa kwa
muda mfupi k**a vile serena, lulu, tegemeo,
masia, okoa, n.k.]]', muhogo kiasi na katika
maeneo machache mpunga na zabibu, zao
ambalo ni mahususi kwa biashara.
CHAKULA KIKUU
Wagogo hula ugali wa uwele k**a chakula kikuu
na huchukulia ugali wa mahindi mtama k**a
chakula laini na chepesi kisicho na nguvu.
Miaka ya zamani mlo wa kawaida wa Mgogo
mwenye uwezo (yaani mwenye ng'ombe)
ulihusisha ugali, maziwa, mafuta ya ng'ombe,
kwa kigogo samuli na mboga k**a mlenda
"ilende", safwe, cidingulilu, nyakifwega, muhilile,
sanghala, munzimwa, cipali, ihaji, sagulasagula,
ikuwi, fwene, nghalabwajila (hasa wakati masika
inapoanza) n.k.
Kwa sasa Wagogo wamekuwa wakila chakula
cha kawaida k**a makabila mengine nchini
Tanzania.
LAFUDHI YA LUGHA
Kabila la Wagogo lina lahaja ndani yake ambazo
hutofautiana kutoka lahaja moja hadi nyingine
kwa jinsi ambavyo hutamka maneno, yaani
huongeza na kupunguza baadhi ya matamshi
kwenye neno, na pia katika msamiati. Kwa
ujumla kuna lahaja zipatazo 4, ambapo lahaja za
Cinyambwa na Cinyaugogo ndizo hujulikana zaidi.
1. Wanyambwa - Hili ni kundi linaloonekana wazi
kwenye kabila hili ambao huongea lafudhi ya
Kinyambwa. Wanyambwa hutokea vijiji vya
magharibi kwa mji wa Dodoma na sehemu ya
wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Mifano - matamshi - vipi? = ntaule?
-msamiati - panda darini = ukwine kitembe
2. Wanyaugogo - hawa huongea lafudhi iitwayo
Chinyaugogo. Wanyaugogo ambao ndio
wanaowakilisha kundi kubwa sana hutokea vijiji
vya mashariki na kusini kwa mji wa Dodoma na
pia wilaya ya Mpwapwa. Kwa sababu mtemi
Mazengo alikuwa mnyaugogo kutoka Mvumi
mahali ambapo palijengwa kijiji kinachoitwa
Mvumi Makulu (kwa maana kwamba ndipo
ilipokuwepo Ikulu ya Mtemi), inaaminika kuwa
lafudhi hii ndicho Kigogo cha asili isiyoathiriwa
na lugha za nje.
Mifano - matamshi: - vipi? = nhaule?
-msamiati - panda darini = unanuce kitembe
3. Wetumba - Hawa ni wagogo walioathiriwa
Kigogo chao na Kikaguru. Hupatikana katika
wilaya za Kongwa na Mpwapwa
Mfano - matamshi - jua limekuchwa - dizuwa
diswa. Wanyaugogo hapa husema "lizuwa laswa/
liswa"
4. Wetiliko - Hawa ni wagogo wenye asili au
mchanganyiko na wahehe, na hupatikana maeneo
ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
Mfano - matamshi - twende = tibite. Wanyaugogo
hapa husema "cibite"
A MAJINA YA UKOO YA CIGOGO
Majina hayo ni k**a Mazengo, Cidosa, Cilongani,
Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi,
Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya, Matonya,
Mtunya, Kusila, Nhonya, Mhalanyuka, Mbenaa,
Chibile, Mdoli, Lusinde, Njamasi, Majenda,
Chiwamba, Chiwaligo, Mazoya, Ufinyu,
Chilyawanhu, Mahujilo, Magaya, Ngoli,
Chiwanga,Lenjima, Lubeleje, Makupila, Fukunyi,
Mondigwa, Ndasimi, Nhukuwala, Muhembano,
Masinga, Ndahani, Chedego, Chenda, Chonya,
Chimbwi, Cibehe, Mabwe, Malejehe, Madole
(endeleza)
SEMA SASA JUU YA WAGOGO UWAJUAVYO
WEWE..!!!
# WAGOGO_OYEEEEE_LEO_NIMEWAGUSA_
HAHAHAAA!!

Photos 25/12/2016

Wapendwa tusherekee kwa Amani Krismasi na Mwaka Mpya!

Photos 14/10/2016

Neno Moja tu kwake!

07/08/2016

Usipande ngazi ya mafanikio huku mikono yako umeweka mfukoni....!

Jioni njema.

30/07/2016

Mbukwenyii wanasuk**ahela..!

31/12/2015

Heri ya Mwaka mpya 2016 ndugu zangu wooote na Mungu awabariki sana!

26/06/2015

Habariiii!!!

31/05/2015

Shida ya maji jamani SUKAMAHELA mpaka basi. ....

Want your business to be the top-listed Government Service in Manyoni?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


SINGIDA
Manyoni