๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Halmashauri ya Mji Masasi imefanikiwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na vyoo matundu sita ya elimu ya awali katika Shule ya Msingi Kitunda yaliyowavutia wazazi wengi zaidi kuwaandikisha watoto wao katika elimu ya awali.
Utekelezaji wa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi 67,300,000 kutoka katika Mradi wa Boost, ukiwa na lengo la kuboresha mazingira ya kisasa zaidi ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa elimu ya awali pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za elimu katika eneo la Kitunda.
Akizungumza Mwalimu Mkuu Shule hiyo, Mwl. Cyprian Ndaka, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia shule hiyo mradi huo bora, Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Waheshimiwa Madiwani na Mkurugenzi wa Mji kwa maelekezo mbalimbali na usimamizi wa mradi huo bora.
Amesema kuwa mradi huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia na hivyo kuvutia wazazi wengi zaidi kuwaandikisha watoto wao katika elimu ya awali.
Vilevile, mradi huo unatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu bora kwa watoto wa ngazi ya awali.
Halmashauri ya Mji - Masasi
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Halmashauri ya Mji - Masasi, Public & Government Service, P. O BOX 447 MASASI, Masasi.
25/05/2026
๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐
๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto na Wanawake (MTAKUWWA) Halmashauri ya Mji Masasi imejizatiti kuhakikisha tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani chini ya umri wa miaka 18 linakwisha kabisa hususani wanaofanya biashara za vinywaji na mayai katika sehemu za mikusanyiko k**a stendi na sokoni.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha kujadili taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto na Wanawake (MTAKUWWA) ya Robo ya Tatu (Januari-Machi 2025/2026) ambapo imebainika kuongezeka kwa watoto wanaofanya biashara za vinywaji na mayai katika sehemu za mikusanyiko k**a stendi na sokoni hasa katika kipindi cha likizo.
Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Leila Kasugulu, Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Neema Joseph amesema suala hilo limezidi kuongezeka kutokana na wazazi kuwashirikisha watoto wao katika shughuli za biashara za vinywaji na mayai sehemu za maduka, sokoni na standi za mabasi.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Andrea Kalinga amesema k**ati hiyo ifanye juhudi ya kuwatambua watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani, kutoa matangazo ya kuzuia watoto kufanya kazi hizo, kutoa elimu shuleni, kwenye nyumba za ibada na kisha kuanza kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, miongozo ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha kabisa.
Aidha imebainishwa kuwa tayari hatua mbalimbali zimefanyika ikiwemo Ustawi wa Jamii imefanikiwa kuunda vikundi vya Malezi 24 kwa kata zote 14 ikiwa na lengo la kuhakikisha familia zinakaa kwenye mazingira safi na salama ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.
23/05/2026
Kikao Cha k**ati ya Lishe kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Masasi Ndg.Andrea Kalinga kimefanyika leo tarehe 22 Mei 2026.
Ndg.Andrea Kalinga amewaasa wazidi kutekeleza majukumu yao katika kila sekta ili kuweza kuleta matokea chanya.
22/05/2026
๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐, ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Rachel Kassanda, amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu sahihi ya lishe ili kuboresha afya za familia na kuondokana na changamoto za utapiamlo katika jamii.
Akizungumza wakati anaongoza Kikao cha Tathmini ya Lishe kilichofanyika tarehe 22 Mei 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Mhe. Kassanda alisema kuwa lishe bora ni msingi wa afya, maendeleo ya watoto pamoja na ustawi wa jamii kwa ujumla.
โEndeleeni kuwasisitizia wananchi kuzingatia lishe bora hasa kwa wajawazito na watoto wadogo ili wapate virutubisho sahihi na muhimu vinavyotakiwa. Wananchi wakielewa umuhimu wa lishe wataweza kujikinga na magonjwa yanayotokana na upungufu wa virutubisho,โ alisema Mhe. Kassanda.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Andrea Kalinga aliwataka Watendaji wa Kata kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa afya pamoja na maafisa maendeleo ya jamii katika kuendesha kampeni za uhamasishaji wa matumizi ya vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika maeneo yao k**a vile mboga za majani, matunda, mayai, maziwa na vyakula vya protini.
Kwa upande wao baadhi ya Watendaji wa Kata walieleza kuwa wataendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, vikundi vya kijamii pamoja na ziara za kaya kwa kaya ili kuwapa elimu ya lishe bora.
20/05/2026
๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐, ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi imeridhishwa na kupongeza ubora wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji Masasi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.4 ikiinasibu kuwa itaenda kuchochea ukuaji wa uchumi na uboreshaji wa huduma kwa wananchi.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Masasi Bi. Mariam Kasembe akiambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wametembelea na kukagua miradi hiyo leo Mei 20, 2026.
Akizungumza katika ziara hiyo, Bi. Kasembe amesema miradi hiyo ni bora na inakwenda kuinua Uchumi wa Masasi.
โTunapongeza utekelezaji wa miradi hii, mradi wa ghala ukikamilika utaongeza mapato yetu lakini pia utapunguza adha ya utunzaji wa mazao wakati wa msimu. Hatutakua na sababu ya kuacha mazao yetu katika vyama vya msingi na kuchelewesha tena mazao kuja ghalaniโ, alisema Mhe. Kasembe na kuongeza;
โMiradi yote ni mizuri na ina tija k**a wajumbe walivyojionea, hii inadhihirisha uhalisia wa fedha za Serikali zinavyofanya kazi. Niwaombe tujitahidi kuisimamia kwa weledi ili imalizike kwa wakati na kuleta maendeleo k**a ilivyodhamiriwaโโ.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Rachel Kassanda amesema Serikali itaendelea kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inasimamiwa kwa karibu ili fedha zinazotolewa ziweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Ndg. Andrea Kalinga amesema Halmashauri itahakikisha usimamizi thabiti ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati k**a ilivyopangwa.
Kamati hiyo imetembelea miradi mitano ikiwemo mradi wa maegesho ya vyombo vya usafiri, maboresho ya Chuo cha Wanafunzi wenye Changamoto za Uoni, mradi wa shule mpya ya mkondo mmoja ya Msingi jirani na sekondari, mradi wa soko mbadala Mkuti pamoja na mradi wa ujenzi wa ghala la mazao eneo la Mtandi.
Ziara hiyo ya Kamati ya Siasa ya Wilaya imelenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi pamoja na kutoa maelekezo ya kuboresha maeneo yenye changamoto ili kuhakikisha wananchi wa Masasi wanaendelea kupata huduma bora na maendeleo endelevu kupitia miradi inayotekelezwa na Serikali.
โ๐๐ฐ๐๐ง๐ ๐ ๐ฐ๐ ๐๐ก๐ฎ๐ซ๐ฎ ๐๐๐๐ ๐ฎ๐ฆ๐๐๐ฎ๐ซ๐๐ก๐ข๐ฌ๐ก๐ฐ๐ ๐ฌ๐๐ง๐ ๐ง๐ ๐๐ฃ๐๐ง๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐จ๐๐ข ๐ก๐ข๐ข ๐ฒ๐ ๐๐๐ ๐๐จ๐ฌ๐ฉ๐ข๐ญ๐๐ฅ๐ข ๐ฒ๐ ๐๐ค๐จ๐ฆ๐๐ข๐ง๐๐จ, ๐ง๐ข ๐ฒ๐ ๐ค๐ข๐ฌ๐๐ฌ๐ ๐ฌ๐๐ง๐, ๐ง๐ข ๐ฆ๐๐๐ง๐จ ๐ฐ๐ ๐ค๐ฎ๐ข๐ง๐ ๐ฐ๐ ๐ค๐ฐ๐ ๐ค๐๐ง๐๐ ๐ฒ๐จ๐ญ๐ ๐ฒ๐ ๐ค๐ฎ๐ฌ๐ข๐ง๐ข, ๐ก๐๐ญ๐ ๐ฉ๐ซ๐ข๐ฏ๐๐ญ๐ ๐ก๐จ๐ฌ๐ฉ๐ข๐ญ๐๐ฅ ๐ก๐๐ค๐ฎ๐ง๐ ๐ฐ๐จ๐๐ข ๐ค๐๐ฆ๐ ๐ก๐ข๐ขโ ๐๐ข๐จ๐ง๐ ๐จ๐ณ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐๐ข๐จ ๐ณ๐ ๐๐ฐ๐๐ง๐ ๐ ๐ฐ๐ ๐๐ก๐ฎ๐ซ๐ฎ ๐๐๐๐.
12/05/2026
DKT. AKWILAPO AKOSHWA NA MRADI WA VIJANA UBINAKI, AAHIDI KUWALIPIA SEHEMU YA MKOPO.
Mbunge wa Jimbo la Masasi ambae pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo amewapongeza Kikundi cha Vijana wa UBINAKI kwa kuamua kuungana na kujiajiri katika soko la bidhaa za samani ili wajikwamue kiuchumi.
Mhe. Dkt. Akwilapo aliyasema hayo baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Uhuru Kitaifa 2026, Ndg. Wazo Michael Mwangโonda kukagua Mradi wa Vijana wa UBINAKI uliopo Halmashauri ya Mji Masasi ambao ni moja ya matunda ya mikopo ya asilimia 10 za mapato ya ndani.
โVijana hawa wameamua kujiunga na kujitegemea, huu ni mfano wa kuigwa kwa vijana wote nchini. Naipongeza Halmashauri ya Mji Masasi kwa kuendelea kutekeleza sera ya kuwakopesha wananchi ili wajikwamue kiuchumiโ, alisema Dkt. Akwilapo.
Katika kuonyesha dhamira ya kuwaunga mkono kwa vitendo, Mhe. Dkt. Akwilapo aliahidi kuwalipia Shilingi 400,000.00 ya marejesho ya mkopo wao kwa muda wa miezi sita mfululizo huku akinunua moja ya kitanda ambacho kimetengenezwa na wanakikundi hao.
Mhe. Dkt. Akwilapo aliahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali na makundi ya vijana ili kutatua changamoto zao k**a vile mitaji, mafunzo na vifaa vya kazi vitakavyowasaidia kuongeza kipato na kujitegemea
Kikundi cha Vijana cha UBINAKI kilianzishwa kikiwa na mtaji wa shilingi 3,380,000.00 ikijumuisha na mashine za mkono ambazo zilitokana na michango toka kwa wanakikundi. Halmashauri ya Mji Masasi iliwapatia mkopo wa Shilingi 30,972,000/=.
Mkopo huu uliwezesha kuboresha mazingira ya kiwanda, ununuzi wa malighafi, vitendea kazi ikiwemo kununua mashine za kisasa mbili (2), mashine kwa ajili ya kuranda, kuchana na urembo na mashine ya kutengeneza maumbo. Marejesho ya mkopo yatafanyika kwa miaka mitatu yaani kuanzia Disemba 2025 hadi Disemba 2028.
12/05/2026
KIONGOZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU AKOSHWA NA MRADI WA WODI MAALUM YA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOMAINDO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndg. Wazo Michael Mwangโonda amekoshwa na mradi wa ujenzi wa wodi maalum ya wagonjwa (VIP) katika Hospitali ya Mkomaindo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 170 hadi kukamilika kwake ambazo zote zimetoka katika mapato ya ndani.
โMradi huu ni wa kujivunia sana kwa sababu utatoa huduma maalum kwa wananchi wa Masasi na maeneo ya jirani. Niishukuru sana Serikali kwa mradi huu ambao ni mfano wa kuigwa kwa Ukanda wa Kusini. Wodi k**a hii, hata Hospitali za binafsi hakuna wodi ya kisasa sanaโ, alisema Ndg. Mwangโonda
Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leornard Akwilapo amesema kipaumbele cha Serikali ni kuhakikisha wananchi wa Masasi wanapata huduma bora za kijamii hususani afya kwa wote.
โAfya kwa wote ndo kauli mbiu yetu na Mhe Rais Dkt. Samia anasisitiza tutunze afya, tulinde afya zetu na mimi kwa niaba yenu nampongeza Mkurugenzi wa Mji Ndg. Reuben Jichabu, waheshimiwa madiwani na watumishi wote wa Halmashauri walioamua kujenga wodi hii ya mfano kwa kanda yote ya kusiniโ Dkt. Akwilapo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi alisema ujenzi wa wodi hiyo ni mkakati madhubuti wa Serikali kuendelea kuboresha sekta ya afya.
โNiwapongeze sana wana Masasi kwa mradi huu wa kipekee, sekta ya afya ni eneo muhimu ambalo Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutilia mkazo na uwepo wa miradi hii ni kiashiria cha muendelezo wa juhudi za kuboresha huduma za afya nchiniโ, alisema Mhe. Kanali Msengi.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Masasi Dkt. Rosemary Mushi alisema;
โMradi huu umegharimu Tsh 170,136,516.79 na unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini kwa kuwezesha uwepo wa wodi nzuri ya kisasa na yenye hadhi, kuongeza mapato ya hospitali na Halmashauri kwa ujumla na kuwaondolea adha wananchi ya kufuata huduma hiyo katika hospitali zilizo mbaliโ.
11/05/2026
MWENGE WA UHURU WAAGWA MASASI MJI, MIRADI YA KIMKAKATI YAPONGEZWA
Baada ya kukimbizwa kwa umbali wa kilomita 74 ukipita katika katika Tarafa moja (1), kata tisa (9), vijiji tisa (9) na mitaa kumi na sita (16), Mwenge wa Uhuru ulihitimisha safari yake katika viunga vya Halmashauri ya Mji Masasi.
Kiongozi wa Mbio hizo Kitaifa, Ndg. Wazo Michael Mwangโonda alipongeza juhudi zinazofanywa katika kusimamia miradi ya maendeleo ambayo inafanyika katika Mji huu.
โNawapongeza kwa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kufanyika katika Halmashauri ya Mji Masasi. Pia niwapongeze kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wakubwa kupitia mradi wa kiwanda cha kubangua korosho ambao umegharimu Shilingi Bilioni 20. Hatua hii inaenda kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia ajira na tozo zitakazolipwa wakati wa uzalishajiโ, alisema Ndg. Mwangโonda na kuongeza;
โNiwaase wanaMasasi kuendelea kudumisha amani na ushirikiano ili kuhakikisha kila Mtanzania anaishi kwa utulivu. Pia tutumie Jukwaa la Vijana kuwakutanisha vijana wenzetu kwa ajili ya kuambizana fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumiโ.
Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yalifanyika katika Kijiji cha Namatumbusi Wilayani Nanyumbu.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Website
Address
P. O BOX 447 MASASI
Masasi
65227
