The Copyright Society of Zanzibar Dealing with Registration, Protection of Artistic works & Provide
jamii
HISTORIA YA SHERIA YA HAKIMILIKI (COPYRIGHT ACT NO.14, 2003)
Dhana na ulinzi wa hakimiliki si mpya k**a jamii ya watu wa Zanzibar inavyofikira kwani Sheria ya hakimiliki (Copyright Act No. 14 of 2003) ilikuja kuifuta sheria ya Order in Council ya mwaka 1962 ambayo pia ilifatiwa na Englisha Copyright Act 1956 ambazo zote hizo kwa pamoja zilikuwepo kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wakoloni zaidi na sio wazanzibar kwa ujumla. Ndipo mnamo mwaka 2003 Serikali iliamua kuifanyia marekebisho ili kuendana na wakati uliopo. KAZI ZINAZOLINDWA NA SHERIA YA HAKIMILIKI
vitabu,vitini,makala,program za computer,maandishi ya kisayansi na
Kisanaa pamoja ma kazi nyengine za kimaandishi;
mihadhara ,hotuba ,mahubiri na kazi nyengine zenye muelekeo k**a huo. kazi za maigizo na zile za muziki wa maigizo ,maigizo bubu,na upigaji wa vinanda na kazi nyengine zinazoandzliwa kuoneshwa jukwaani. kazi za kimuziki ( wa sauti na ala) zenye kujumuisha au bila kujumuisha
Maneno. kazi za vielelzo vya kusikia na kuona
kazi za usanifu wa majengo
kazi za kuchora,kuchora kwa kutumia rangi ,usanifu wa majengo,sanaa na
uchongaji vinyago,sanaa ya utunzi nakshi ,sanaa ya litografia na mapambo
kazi za sanaa ya upigaji picha ,ikiwa ni pamoja na kazi zinazotolewa kwa
Njia zinazoambatana na upigaji picha. kazi za sanaa tumizi,ziwe za mikono au zinazotengenezwa katika viwango
Vya viwandaji. vielelzo,ramani,plani,michoro na kazi za mawanda matatu zinazohusiana
na jiografia,usanifu wa majengo au sayansi
UANZISHWAJI WA AFISI YA MSAJILI WA HAKIMILIKI NA KAZI ZAKE
Afisi ya Msajili wa Hakimiliki ilianzishwa mnamo mwaka 2005 kwa ajili ya kufanya kazi zifuatzo:-
Kusajili kazi nilizozitaja hapo juu. Kulinda na utetea maslahi ya wasanii
Kutoa leseni kwa ajili ya matumizi halali ya kazi za hakimiliki
Kukusanya mirabaha kwa matumizi halali ya kazi za hakimiliki
Kugawa mirabaha kwa wanaostahili kupipwa
Kuelimisha jamii juu ya masuala ya hakimiliki
Kutoa ushahidi mahak**ani pale inapohitajikana inapoonekana kuna uvunjwaji wa hakimiliki
Kutoa ushauri wa kisheria kuhusiana na masuala ya hakimiliki
Kutayarisha na kupitia mikataba inayohusiana na hakimiliki.