13/05/2026
WAUGUZI WA MZRH WAWAKILISHA VYEMA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI 2026
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Arusha, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC.
Wataalamu hawa(Wauguzi) wamewakilisha vyema taasisi pamoja na wenzao kutoka sehem mbalimbali Tanzania katika kilele cha maadhimisho hayo ya tarehe 12 Mei yenye kauli mbiu “Wauguzi Wetu, Mustakabali Wetu: Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha.”
13/05/2026
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge Mei 12, 2026 bungeni jijini Dodoma baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/27, hatua inayolenga kuendelea kuimarisha huduma za afya nchini
11/05/2026
MCHENGERWA KUWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA AFYA LEO BUNGENI.
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, leo tarehe 11,Mei,2026 anatarajiwa kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Afya bungeni, akieleza vipaumbele vya Serikali katika kuimarisha sekta ya afya kwa mwaka wa fedha ujao.
Katika hotuba hiyo, Serikali inatarajiwa kueleza hatua mbalimbali za kuboresha huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini.
Aidha, hatua za utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote zinapewa kupewa kipaumbele na mafanikio ya namba 199, inayotumika kuzungumza na wananchi kuhusu masuala ya afya na huduma mbalimbali na Mpango Mkakati wa Kampeni ya “Jua Namba zako”katika kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza pamoja Kampeni ya “Ubongo Hauna Spea,Vaa Helmet na mambo mengine lukuki katika uboreshaji wa Huduma za Afya.
Je, ni kiasi gani Wizara itaidhinishiwa na Bunge katika kufanikisha vipaumbele vyake muhimu ikiwemo eneo la Kinga, Tiba?
Usikose kufuatilia Mubashara kupitia TBC, Crown Media, Uhondo TV, Mzawa TV,Bunge TV na vyombo mbalimbali vya Habari.
10/05/2026
Tunajali Afya yako. Endelea kuwa nasi
01/05/2026
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAWATUNUKU VYETI NA ZAWADI WATUMISHI HODARI KATIKA MAADHIMISHO YA MEI MOSI.
Katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kwa mwaka 2026, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH) imewatunuku vyeti na zawadi wafanyakazi wake waliofanya vizuri zaidi katika nyanja mbalimbali za utoaji huduma za afya.
Hafla hiyo fupi na ya kusisimua imefanyika leo katika ukumbi wa hospitali hiyo, ikilenga kutambua mchango wa wafanyakazi hodari ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora na za haraka.
Akizungumza wakati wa kutoa vyeti hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma, amewapongeza watumishi hao na kuwataka waendelee kuwa mfano wa kuigwa kwa wenzao.
“Tuzo hizi ni chachu ya kuongeza juhudi. Tunatambua utumishi wenu uliotukuka na tunatarajia kuona mabadiliko makubwa zaidi katika utendaji kazi ili kuifikia azma ya serikali ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,” alisema Dkt. Mboma.
Hafla hiyo ilipambwa na uwepo wa viongozi waandamizi wa hospitali pamoja na wageni waalikwa kutoka Chama cha Madaktari na Wafamasia (TMDPWU), ambao walitoa neno la hamasa kwa watumishi hao, wakisisitiza umuhimu wa kulinda haki na maslahi ya mfanyakazi sambamba na kutoa huduma ya kitaalamu.
Maadhimisho haya ya Mei Mosi 2026 yanakuja wakati ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe,
yakiongozwa na kauli mbiu isemayo: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”
Watumishi waliotunukiwa vyeti hivyo wameshukuru Uongozi wa hospitali kwa kutambua mchango wao na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu ili kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2050