Morogoro District Council

Morogoro District Council

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Morogoro District Council, Government Organization, Mvuha, Morogoro.

Karibu katika Ukurasa maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, hapa utakuwa wa kwanza kupata taarifa zote muhimu kuhusu miradi ya maendeleo na shughuli zote zinazoendelea kutekelezwa na Halmashauri yetu.

03/06/2026

Wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro tunaombwa kuhudhuria kwa wingi katika kuupokea mwenge wa uhuru tarehe 15.06.2026 katika Kijiji Cha Pangawe kata ya Mkambarani na kuuga tarehe 16.06.2026.

01/06/2026

Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla mnahimizwa kuwapeleka watoto wote wenye umri wa miezi 6–59 kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya kampeni ili wapatiwe huduma za afya na lishe kwa wakati, kwa ajili ya ukuaji bora na afya njema ya mtoto.

Photos from Morogoro District Council's post 01/06/2026

‎COPRA kanda ya Mashariki Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro 1 June, 2026 imefanya kikao na Wakulima,AMCOS(Vyama vya Ushirika), Pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro iliyolenga Uhamasishaji mwongozo wa Biashara ya Mazao Jamii ya Mikunde na Ufuta.

Photos from Morogoro District Council's post 30/05/2026

‎NAIBU WAZIRI WA ARDHI AFANYA ZIARA MOROGORO DC, ASISITIZA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI KWA KUZINGATIA SHERIA

‎Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya, leo Jumamosi Mei 30, 2026, amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za ardhi zinazowakabili wananchi.

‎Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mmuya alifanya mikutano ya hadhara katika Kijiji cha Mbwade kilichopo Kata ya Bwakila Chini na Kijiji cha Msonge kilichopo Kata ya Mvuha, ambapo alipokea na kujadili changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi.

‎Naibu Waziri huyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, M***a Kilakala, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini , Zuberi Yahaya Mfaume.

‎Akizungumza na wananchi katika mikutano hiyo, Mheshimiwa Mmuya alisema Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Hata hivyo, aliwataka wawekezaji kuhakikisha wanazingatia na kuheshimu makubaliano wanayoingia na wananchi ili kuepusha migogoro inayoweza kuathiri amani na maendeleo ya maeneo husika.

‎Aidha, aliwasihi wakulima na wafugaji kutumia njia za kisheria katika kutatua migogoro yao badala ya kujichukulia sheria mkononi, akisisitiza kuwa kufuata taratibu zilizowekwa kutasaidia kudumisha amani na kuimarisha ushirikiano kati ya makundi mbalimbali ya wananchi.

‎Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Mmuya alimpongeza Mbunge wa Morogoro Kusini, Mheshimiwa Zuberi Yahaya Mfaume, kwa juhudi zake za kuwasilisha na kusimamia hoja mbalimbali zinazolenga kutatua kero za wananchi na kuharakisha maendeleo katika jimbo hilo.

‎Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za awamu ya sita kuendelea kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwa karibu, hususan katika sekta ya ardhi ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

30/05/2026

Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro inaungana na familia, ndugu, jamaa, walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisaki Kituoni katika kipindi hiki cha majonzi.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape wafiwa subira na faraja ya kweli.

Inna lillah wa inna ilaih raajiuun. 🤲

29/05/2026
26/05/2026

Tunapenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na sare ya Mwenge inayojumuisha T-shirt na Kofia k**a zinavyoonekana hapo juu.
Bei ya sare hiyo ni Tshs. 25,000/= kwa package kamili (T-shirt na Kofia).
Sare hizi zitapatikana katika maeneo mbalimbali, ikiwemo:
📍 Mvuha HQ
📍 DED ya Zamani – Mjini
📍 Ofisi za Maafisa Tarafa
Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali piga simu kupitia namba zifuatazo:
☎️ 0687 995 396
☎️ 0743 522 765
☎️ 0789 763 074
☎️ 0717 787 486

26/05/2026

Wilaya ya Morogoro inatarajiwa kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 15-06-2026
‎Katika kijiji cha Pangawe kata ya Mkambarani ukitokea Manispaa ya Morogoro na Mkesha utakuwa kijiji cha Mbwade kata ya Bwakila Chini (Duthumi) kisha tarehe 16.06.2026 utakwenda kukabidhiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.

Want your business to be the top-listed Government Service in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Mvuha
Morogoro