16/07/2019
Ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kilosa kata kwa kata katika MAANDALIZI ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo baadae
Katika Ziara hiyo Katibu Wa CCM Wilaya comrade AZIZA Aziza Isimbula amembatana na Katibu wa Siasa na Uenezi Ndg Jafari Kunambi, Katibu wa UVCCM Wilaya ndg Philbert Kipenda, Katibu wa UWT Wilaya ndg Agnes Chuma pamoja na Katibu wa WAZAZI Wilaya Bi Scholastica Salim
Katika Ziara Sekretarieti imeendelea kuhimiza umoja baina ya Wana CCM, kuvunja makundi hasa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini pamoja na kuendelea kuhimiza juu ya watu wenye sifa kujitokeza katika kuomba nafasi mbalimbali na kwamba Chama hakitambeba mgombea asiye na sifa
AIDHA Chama kimeendelea kuhimiza juu ya umuhimu wa mabalozi katika kuwaweka wanachama pamoja na kwamba kinatambua thamani ya mabalozi wake wote ndani ya Chama kwani wamekuwa wakifanya kazi kubwa mno kuhakikisha CCM inashinda
23/11/2017
Ndugu wanachama waUVCCM wilaya ya kilosa na mkoa wa morogoro napenda kuwapa taarifa kuwa uchaguzi wa viongozi was UVCCM ngazi ya mkoa utafanyika tarehe 29.11.2017 katika ukumbi wa VETA Mikumi kuanzia saa 3 asubuhi.
Aidha uvaaji wa sare za chama uzingatiwe kwa wajumbe wote wa mkutano
Pamoja tunaijenga Tanzania
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:
MOHAMED MSUYA
Mjumbe w baraza LA vijana mkoa wa Morogoro .
05/03/2017
Habari Ndugu Wana Kurasa Hii
Kwa Wiki Zipatazo Mbili Sasa Kumekuwa Na Matukio Mengi Ambayo Yameifanya Kuwa Na Taharuki Kidogo
1.Kitendo Cha RC Makonda Kuwataja Watu Wakubwa Kuhusika Na Madawa Ya Kulevya Akiwemo Gwajima,mbowe Na Manji
2.Kitendo Cha Madame Wema Sepetu Kuhamia CHADEMA Baada Ya Kutuhumiwa Na Kesi Ya Madawa Ya Kulevya
3.Kuteuliwa Kwa Mama Salma Kikwete Kuwa Mbunge
4.Godbless Lema Kuachiwa Huru Na Mahak**a Na Kuthibitika Hakuwa Na Kesi Ya Kujibu
5.Kutuhumiwa Kwa Mh Makonda Kudanganya Vyeti Vyake Vya Elimu Ya Sekondari
Jamani Sasa Nchi Imekuwa Ya Moto Hela Ngumu Tena Huipati Kirahisi Tuwe Makini Mana Tukiwasikiliza Wanasiasa Mambo Mengi Yatasimama
Piga Comment Yako Kwa Jambo Unaloona Haliendi Sawa Huko Ulipo Au Katika Hayo Hapo Juu
NB; PIGA KAZI KIJANA NJAA HAINA DINI,CHAMA WALA KABILA
BY TEAM TAIFA KWANZA
04/02/2017
IMANI ZA CCM:
Chama Cha Mapinduzi Kinaamini Kuwa;
1.Binadamu wote ni sawa
2.Kila mtu anastahili kuthaminiwa na kuheshimiwa utu wake
3.Ujamaa na kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii bora ya watu
AHADI ZA MWANACHAMA WA CCM;
1.Binadamu Wote Ni Ndugu Zangu Na Afrika Ni Moja
2.Nitaitumikia Nchi Yangu Na Watu Wake
3.Nitajitolea Nafsi Yangu Kuondosha Ujinga,umasikini,magonjwa Na Dhuluma
4.Rushwa Ni Adui Wa Haki Sitatoa Wala Kupokea Rushwa
5.Cheo Ni Dhamana Sitatumia Cheo Changu Wala Cha Mtu Mwingine Kwa Faida Yangu
6.Nitajielimisha Kwa Kadri Ya Uwezo Wangu Na Nitatumia Elimu Yangu Kwa Faida Ya Watu
7.Nitashirikiana Na Wenzangu Wote Kuijenga Nchi
8.Nitasema Kweli Daima Fitina Kwangu Mwiko
9.Nitakuwa Mwanachama Mwaminifu Wa CCM,Tanzania Na Afrika Kwa Ujumla.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!.
04/01/2017
Katika Wakati Huu Wa Hapa Kazi Tunahitaji Viongozi Imara Na Wenye Kuchapa Kazi Kwa Nguvu Zote Kwa Ajili Ya Maendeleo Ya Wananchi
Sasa Kwa Kuwa Taifa Lolote Linajengwa Na Vijana Hvyo Basi Ningeomba Vijana Tufanye Maamuzi Sahihi Wakati Wa Chaguzi Za Chama Baadae Mwaka Huu Ili Kukijenga Upya Chama Cha Mapinduzi Na Kuhakikisha Hila Ya Fedha Haitawali Chaguzi Hizi Pamoja Na Kuwaondoa Viongozi Wote Ambao Kwa Namna Moja Au Nyingine Walisababisha Makundi Ndani Ya Chama Au Walifanya Chama Kushindwa Katika Uchaguzi Mkuu 2015
Tukumbuke CCM Ndio Chama Bora,chama Dume Na Dume La Mbegu
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
28/09/2016
Kilosa yetu ndio uhuru wetu na maendeleo yetu ndio amani yetu sasa k**a vijana tuyazingatie haya
Ili ufanikiwe inabidi umtangulize mungu,uwe na mipango thabiti na endelevu na pia jaribu kupunguza maadui kwa upande wako
AHSANTENI SANA
30/06/2016
Ni Wakati Wa Kujitathmini Upya K**a Vijana Wa Kitanzania Wenye Kupenda Maendeleo Ya Taifa Letu Tumetumika Sana Na Wanasiasa Katika Kuwafanikisha Kufika Kwenye Nyadhifa Mbalimbali Lakini Tunapaswa Kujiuliza Je Wao Wametuachaje?
Kiukweli Ni Maumivu Matupu Lakini Hatupaswi Tena Kuangalia Nyuma Bali Tunapaswa Tuitayarishe Kesho Yetu
USHAURI: Wakati Wa Uchaguzi Vijana Tusishabikie Tu Watu Bali Tuangalie Wale Wenye Manufaa Na Jamii Zetu Kwa Uzuri Ama Ubaya Wa Viongozi Wa Safari Hii Tunapaswa Kusifiwa Ama Kulaumiwa Vijana Kwa Sababu Sisi Ndio Tuliokuwa Wengi Wakati Wa Upigaji Wa Kura
Your Future Is Within Your Hand Live As A Slave Today So That You May Live As A King Tomorrow
WISH YOU A NICE MOMENT