Tanzania Forestry Research Institute

Tanzania Forestry Research Institute

Share

Tanzania Forestry Research Institute (TAFORI) was established by Act No. 5 of 1980.

13/05/2026

🇹🇿

01/05/2026

Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 🇹🇿✨

Leo tunasherehekea nguvu, jitihada na mchango wa kila mfanyakazi katika kusukuma mbele maendeleo ya taifa. Kutoka Njombe, tunakumbushwa kuwa:
“Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”
TAFORI tunaamini katika ubunifu, weledi na uwajibikaji k**a msingi wa mafanikio ya pamoja.
Tuendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa heshima na kwa malengo ya kujenga Tanzania bora zaidi.

Heri ya Mei Mosi! 🙌

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 13/03/2026

TAFORI YAONGOZA HATUA ZA UANZISHWAJI WA JUKWAA LA WADAU WA UYOGA TANZANIA

Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kwa kushirikiana na Shirika la ADAP (Association for the Development of Protected Areas) imeongoza hatua za uanzishwaji wa Jukwaa la Wadau wa Uyoga nchini, hatua itakayowezesha wadau wa Sekta ya Uyoga kunufaika kiuchumi na kuongeza kipato kupitia maendeleo ya zao hilo.

Akizungumza leo Machi 13, 2026 katika Makao Makuu ya TAFORI, Morogoro, wakati wa mkutano wa Uanzishwaji wa Jukwaa la Wadau wa Uyoga Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI, Dkt. Revocatus Mushumbusi, alisema jukwaa hilo litaratibu juhudi za Wadau wa Sekta ya Uyoga nchini kwa kuwawezesha kubadilishana maarifa na uzoefu pamoja na kuendeleza sekta hiyo.

Alisema kuanzishwa kwa jukwaa hilo kunalenga kuchangia maendeleo ya ustawi wa uhifadhi wa misitu, uchumi wa wananchi na kuongeza mchango wa zao hili katika pato la Taifa.

Aidha, alisema jukwaa hili litakuwa chombo muhimu cha kutoa ushauri wa kisera, kuhamasisha uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa Kitaifa na Kimataifa.

“Ni matumaini yangu kuwa kupitia chombo hiki, Wadau wataibua mawazo mapya, kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kuendeleza Sekta ya Uyoga, usalama wa chakula, maendeleo ya uchumi yanayoweza kumgusa Mwananchi moja kwa moja na uhifadhi wa mazingira,” alisema.

Dkt. Mushumbusi alisisitiza ni muhimu kuimarisha tafiti za Kisayansi kuhusu aina na thamani ya uyoga ili zao hili liweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa Taifa. Aliongeza kuwa hatua hiyo iende sambamba na kujenga uwezo wa jamii katika kutambua uyoga unaoliwa na wenye sumu, pamoja na kuendeleza teknolojia za uongezaji thamani na kuimarisha masoko ya bidhaa za uyoga.

Alisema uyoga una mchango katika utekelezaji wa Sera mbalimbali za Taifa, ikiwemo Sera za Taifa za Kilimo na Lishe kwa kuongeza upatikanaji wa chakula chenye virutubisho muhimu.
Hatua ya kuanzishwa kwa Jukwaa la Uyoga nchini imefuata baada ya kufanyika kwa Warsha ya Wadau wa Uyoga iliyofanyika Mkoa wa Tabora mwezi Februari, 2025.

12/03/2026

TAFORI kwa kushirikiana na Shirika la ADAP (Association for the Development of Protected Areas) wanatarajia kuanzisha JUKWAA LA WADAU WA UYOGA TANZANIA, kikao kitakachofanyika Machi 13, 2026 Makao Makuu ya TAFORI, Morogoro.

11/03/2026

TAFORI YAELEZA MCHANGO WA SEKTA YA UTAFITI WA MISITU NA UFUGAJI NYUKI KATIKA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI. EP.05.

11/03/2026

TAFORI YAELEZA MCHANGO WA SEKTA YA UTAFITI WA MISITU NA UFUGAJI NYUKI KATIKA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI. EP.04.

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 08/03/2026

Wanawake TAFORI Waungana na Wengine Morogoro Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

Morogoro, Machi 08, 2026. Wanawake wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) leo wameungana na Wanawake wengine duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa bashasha na shangwe, wakisisitiza umuhimu wa haki na usawa kwa Wanawake na Wasichana katika kufikia maendeleo jumuishi.

Maadhimisho haya yamefanyika katika Viwanja vya Mikese Fulwe, Mkoani Morogoro, yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050.”

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyowakutanisha Wanawake wa TAFORI na wanawake wengine kutoka taasisi mbalimbali mkoani Morogoro, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, aliwapongeza Wanawake wa mkoa huo kwa juhudi zao katika maendeleo na uongozi.

Mhe. Malima pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake, akisema hatua hiyo inaonyesha nafasi na mchango mkubwa wa mwanamke katika Jamii na Taifa.

“Hili tunalosherehekea leo zamani hata kutajwa lilikuwa haliwezekani, lakini sasa tumepata nafasi ya kusherehekea; tuendelee kuienzi,” alisema.

Aliongeza kuwa Mkoa wa Morogoro unajivunia kuwa kinara katika kuwawezesha Wanawake na kusisitiza kuwa mchango wa Wanawake ni muhimu katika gurudumu la Maendeleo ya Taifa kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, aliwahimiza Wanawake kutambua kuwa mafanikio yao yapo mikononi mwao na kuwataka kuendelea kushirikiana.

Maadhimisho hayo yamebeba umuhimu mkubwa kutokana na mchango wa Wanawake katika Maendeleo ya Jamii na Taifa, hususan katika Sekta ya Misitu na Ufugaji Nyuki.

08/03/2026

Heri ya Siku ya Wanawake Duniani


Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 06/03/2026

📍Morogoro
Machi 05, 2026

Wanawake kutoka Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI ) wanaungana na wanawake wote nchini katika wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yanaendelea kufanyika hapa nchini kuanzia Machi 01 - 08, 2026

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mwaka huu yanaongozwa na Kauli mbiu isemayo:
”Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050”.


06/03/2026

📍Morogoro
Machi 05, 2026

Wanawake kutoka Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI ) wanaungana na wanawake wote nchini katika wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yanaendelea kufanyika hapa nchini kuanzia Machi 01 - 08, 2026

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mwaka huu yanaongozwa na Kauli mbiu isemayo:
”Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050”.


Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 19/02/2026

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. CHANDE AAGANA NA BODI YA 12 YA WAKURUGENZI YA TAFORI

*Morogoro.* Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.), ameiaga Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) iliyokuwa imemaliza muda wake kwa kipindi cha miaka Mitatu.

Akizungumza leo Februari 19, 2026 katika hafla ya kufunga kikao cha Bodi ya 12 ya Wakurugenzi kilichofanyika katika Ukumbi wa Morena, mkoani Morogoro, Mhe. Chande ameipongeza TAFORI kwa mafanikio makubwa ya utafiti, hususani kubaini sifa za asali ya Tanzania na kuwezesha utengenezaji wa alama ya chapa ya asali ya Tanzania (_Honey Trademark_) yenye ubora wa kipekee unaotambulika kimataifa.

Katika hotuba yake, Naibu Waziri ameiagiza Taasisi kuimarisha tafiti za kibunifu zitakazoongeza thamani ya rasilimali za misitu na mazao ya nyuki, pamoja na kuongeza mchango wa sekta hizo katika uchumi wa taifa.

Vilevile, amesisitiza umuhimu wa kuwajengea watafiti uwezo kitaaluma kupitia mafunzo ya juu na fursa za uzoefu ndani na nje ya nchi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika utafiti wa misitu na ufugaji nyuki.

Aidha, ameagiza TAFORI kupanua wigo wa ushirikiano kwa kushirikisha wataalam wa utafiti kutoka taasisi nyingine za kitaifa na kimataifa ili kuongeza ubora, ubunifu na ushindani wa tafiti zake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI, Dkt. Revocatus Mushumbusi, ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Wakurugenzi iliyomaliza muda wake, chini ya Mwenyekiti wake Prof. Verdiana Masanja, kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha Taasisi tangu kuanzishwa kwake.

Mkurugenzi Mkuu Dkt. Mushumbusi ameahidi kuwa TAFORI itatekeleza kwa vitendo maelekezo na maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri kwa lengo la kuendelea kuimarisha tafiti zenye tija kwa maendeleo endelevu ya rasilimali za misitu na sekta ya nyuki nchini.

Want your business to be the top-listed Government Service in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Kingolwira
Morogoro

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30