Hospitali Ya Rufaa Mkoa Katavi

Directions Website

Hospitali Ya Rufaa Mkoa Katavi Ukurasa Rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Katavi.

15/10/2026

VIDEO: "Nawapongeza sana Madaktari na Wauguzi kwa jitihada zao, Mwanangu amepona" Aeleza kwa hisia Baba aliyemleta Mtoto wake kufanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama za Pua na Tonsesi. Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi tunatoa Huduma za Kibingwa za Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Karibu tukuhudumie.

Bodi ya ushauri, Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi tunawatakia Watanzania wote maadhimish...
14/10/2026

Bodi ya ushauri, Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi tunawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya siku ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

13/10/2026

Katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Tunatoa huduma ya VIUNGO BANDIA na VIFAA TIBA SAIDIZI kwa ubora wa hali ya juu, Karibu tukuhudumie.

08/10/2026

Heri ya wiki ya Huduma Kwa wateja, Karibu tukuhudumie.

Leo, tarehe 8 Oktoba 2026, Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Afya ya Macho, siku inayoleng...
08/10/2026

Leo, tarehe 8 Oktoba 2026, Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Afya ya Macho, siku inayolenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda afya ya macho na kuchukua hatua za mapema dhidi ya changamoto mbalimbali za uoni.

Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi tunatoa huduma za matibabu ya kibingwa ya macho, Karibu tukuhudumie.

06/10/2026

"Mnatoa huduma nzuri sana, Muendelee hivyo hivyo kujali Wagonjwa", Amesema Bi. Theonistina Njunwa, mteja aliyetembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kupata huduma za kimatibabu.

Kutana na Dr. Philipo Mwita, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa mkojo na afya ya uzazi kwa wanaume kwenye kliniki ze...
29/09/2026

Kutana na Dr. Philipo Mwita, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa mkojo na afya ya uzazi kwa wanaume kwenye kliniki zetu za Kibingwa zinazofanyika kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa.

24/09/2026

VIDEO: Kliniki ya Lishekatika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi itaanza Jumatatu Septemba 28, 2026 na itafanyika kila siku za wiki, Karibu sana tukuhudumie.

23/09/2026

VIDEO: Karibu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Upate Huduma bora za vipimo vya Kisasa kutoka kwenye Maabara yetu ambavyo awali havikuwepo katika Mkoa wetu wa Katavi, K**a Vipimo ya Figo ( Renal Function Test), Vipimo vya Ini (LFT), Vipimo vya Hormone ya uzazi, Kipimo cha tenzi dume, Kipimo cha kuthibitisha Seli Mundu na Vipimo vya culture.

Mbali na vipimo hivyo, Kuna vipimo vingine zaidi ya 150, Na huduma zetu zipo masaa 24.

Karibu tukuhudumie.

Address

P. O BOX
Mpanda
449

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hospitali Ya Rufaa Mkoa Katavi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share