NACP-Tanzania

NACP-Tanzania

Share

NACP Tanzania
National AIDS Control Programme (NACP)
+255(0)262960148,[email protected]
Dodoma Tanzani

National AIDS Control Programme (NACP) under the Department of Preventive Services of the Ministry Of Health,Community Development,Gender, Elderly and Children(MOHCDGEC) is mandated to coordinate HIV and AIDS prevention, care, treatment and support response within the health sector and to respond to the needs of non-health sectors. The mission of NACP is to work in partnership with other public se

19/10/2023

NACP - Furaha YanguWizara ya Afya

31/07/2022

*Prof. Makubi akutana na Mratibu wa PEPFAR nchini Canada*

Canada

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Dkt. John Nkengasong ambaye ni Mratibu wa Serikali ya Marekani katika kupambana na UKIMWI duaniani na msimamizi wa mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti UKIMWI (PEPFAR).

Prof. Makubi na Mhe. Dkt. Nkengasong wamekutana wakati wa Kongamano la UKIMWI duniani linalofanyika mjini Montreal, Canada ambako walijadiliana kuhusu jinsi ya kuboresha ushirikiano kati ya PEPFAR na Serikali ya Tanzania katika kudhibiti UKIMWI.

Prof. Makubi amempongeza Dkt. Nkengasong kwa uteuzi wake wa kihistoria na kumuomba kushirikiana zaidi na PEPFAR katika kuwekeza Tanzania kwenye viwanda vya bidhaa za huduma za afya.

Vile vile umuhimu wa kuboresha utoaji wa huduma za afya na kutumia watoa huduma za afya ngazi ya jamii kwa kuwa kuna upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali za afya.

Aidha, Prof. Makubi aliongelea umuhimu wa kutambua ongezeko la kasi la magonjwa yasiyoambukizwa k**a Kisukari, Shinikizo la damu na unene uliopitiliza.

Prof Makubi aliishukuru PEPFAR kwa kuijuimisha Tanzania kuwa kati ya nchi chache zitakazo tekeleza mkakati maalumu wa kutokomeza UKIMWI kwa Watoto. Mwisho Prof. Makubi alimkaribisha Mhe. Dkt. Nkengasong kutembelea Tanzania.

Balozi Nkengasong alisisitiza umuhimu wa nchi kujipanga na kuhakikisha uendelevu wa mwitikio wa mapambano dhidi ya UKIMWI. Katika kuendeleza ushirikiano kati ya serikali hizi mbili Balozi Nkengasong ameahidi kuja kutembelea Tanzania

Photos from NACP-Tanzania's post 31/07/2022

*Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na Global Fund*

Montreal , Canada, 30 Julai 2022.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi leo tarehe 30 Julai,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Global Fund Bw. Peter Sand katika Mkutano wa Kimataifa wa UKIMWI unaofanyika Montreal nchini Canada.

Katika mazungumzo hayo Prof. Makubi amemuhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Wizara ya Afya itaendelea kudumisha mahusiano ya karibu na mfuko huo pamoja na kusimamia kwa makini miradi pamoja na kuboresha zaidi huduma za afya kwa wananchi.

Katika Mkutano huo Tanzania imewasilisha 360 video ya mafanikio ya mfuko wa Serikali na Global Fund katika kudhibiti magonjwa ikiwemo UKIMWI, Malaria, TB na kuimarisha mifumo ya Afya.

Mkurugenzi Mkuu wa Global Fund ameahidi kutembelea Tanzania mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Photos from NACP-Tanzania's post 30/06/2022

Makakati Mpya wa kudhibiti UKIMWI Waandaliwa

Wizara ya Afya kupitia NACP kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeanza kikao kazi cha kuandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Afua za VVU na UKIMWI nchini. Kikao hicho cha siku tano kinafanyika mkoani Singida kikihusisha wadau kutoka OR-TAMISEMI, taasisi za Umma na Binafsi, wawakilishi wa Waratibu wa UKIMWI wa Mkoa na Wilaya, Wadau wa Utekelezaji na Wamaendeleo.

Akifungua mkutano huo, Dkt.Victorina Ludovick, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida amewataka wadau kubaini mbinu mpya za kuhakikisha walioambukizwa VVU wanahudumiwa k**a wanavyostaili. “Kipindi hiki ambacho tumeanzisha tiba na matunzo ya dawa za ARV kwa watu wote wanaogundulika na maambukizo ya VVU, wadau tuhakikishe kuwa Mpango kazi unabainisha mbinu mbalimbali za kutatua changamotozinazoweza kujitokeza katika utekelezaji huu”

NACP inaratibu mwitikio wa Sekta ya Afya katika kudhibiti UKIMWI nchini kwa kuandaa Mpango Mkakati, Mpango wa utekelezaji, miongozi ya mafunzo na uelimishaji wa umma

30/11/2021

TOENI JIBU LA KUMALIZA MAAMBUKIZI YA VVU NCHINI.

Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii. Jinsia wazee na Watoto Dkt.Beatrice Mutayoba amewataka Waganga wakuu wa Wilaya,Waratibu wa UKIMWI wa Mikoa na Waratibu wa UKIMWI wa Wilaya Nchini kutoa suluhisho la kumaliza maambukizi ya UKIMWI nchini kwa kufikia Malengo ya kidunia ya mwitikio wa UKIMWI ifikapo 2030.

Dkt.Mutayoba, aliyemuwakilisha Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Wedson Sichwale katika ufunguzi wa mkutano wa kitaalamu wa waganga wa wakuu wa wilaya na waratibu wa UKIMWI wa mikoa na wilaya nchini kutoka nchi nzima Jijijini Mbeya, uliandaliwa sambamba na maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani amesema Tanzania imepiga hatua katika kufikia malengo ya 95 95 95 ya kidunia lakini bado takwimu zionyesha bado nchi ipo chini ya malengo hayo.

Angalau kutoka mwaka 2010 hadi 2020 tumepunguza vifo kwa asilimia 50 lakini changamoto bado ni nyingi kwenye maeneo mengi k**a maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, unyanyapaa, huduma za upimaji, huduma za kufubaza VVU, na huduma nyingine za kinga, alisema Dkt . Mutayoba na kusisitiza kikao hicho kijadili masuala ya UKIMWI nchini na kubuni mkakati unaoshabihiana na yale ya tamko la makubaliano ya kisiasa unaolenga kutokomeza maambukizi ifikapo mwaka 2025.

30/11/2021

KUMALIZA MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO-BADO VITA IPO.

Mkurugenzi na Mwakilishi mkazi wa UNAIDS nchini Dr Leo Zekeng amewataka wataalamu wa Afya na Taasisi zinazotekeleza afua za kudhiti UKIMWI nchini kusaidia jamii kuwa ulelewa wa kutosha kuhusu udhiti wa maambuki ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambao bado ni chanagamoto kwa jamii na linaendelea kukwamisha kufikia malengo ya kidunia ya kutokomeza maambuki ya VVU ifikapo 2030.

Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa kikao cha kitaalamu cha waganga wakuu wa wilaya na waratibu wa UKIMWI wa Mikoa na Wilaya jijini Mbeya uliandaliwa kuelekea madhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, Dkt. Zekeng amewahasa wataalamu kuongozea jitihada za uelimishaji na huduma za kinga kudhibiti maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili kufikia ya kidunia na kitaifa kuhusu VVU na UKIMWI.

30/11/2021

MADAKTARI NCHINI WAHIMIZWA KUFIKISHA HUDUMA ZA UKIMWI KWA KILA MUHITAJI.

Mratibu wa Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Masuala ya UKIMWI (PEPFAR) nchini Jesca Greene amewahasa wataalamu wa Afya na waratibu wa afua za kudhibiti UKIMWI nchini kutekeleza afua hizo kwa mapana yake na kufikia makundi yote ya jamii.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa waganga wakuu wa Wilaya na Waratibu wa UKIMWI wa Mikoa na Wuilaya, ulioandaliwa sambamba na maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Jijini Mbeya leo Tarehe 29/11/2o21 Bi. Jesca amesema PEPFER itaendelea kusaidia utekelezaji wa afua hizo kifedha ili kuwezesha serikali na wadau wanatekeleza afua hizo muhimu kufikia malengo ya kidunia kwa unora unaotakiwa.

Bi Jesca ameeleza umihimu wa kuimarisha huduma kwa kundi la Watoto na kundi la watuy wanaoshi na VVU, akisisitiza pia jamii kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa kuwa ulimwengu upo katika zama za kugubikwa na Magonjwa ya milipuko.

Photos from NACP-Tanzania's post 30/11/2021
Photos from NACP-Tanzania's post 29/11/2021

ULEVI, DAWA ZA KULEVYA SIYO KIKI, JITAMBUE.

Vijana nchini Tanzania wametakiwa kutambua nafasi yao katika jamii na kuishi kwa malengo, kujithamini na kuamini kuwa wao ni wazazi na viongozi wa Taifa watumainiwa.
Wito huo umetolewa na Naibu katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Uratibu na Bunge Mh. Casper Muya akizindua Mdahalo wa vijana kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Jiijini Mbeya Tarehe 28/11/2021.

Mh. Muya amesema vijana ni asilimia 68 ya watanzania wote jambo la kujivunia kuwa Taifa lina nguvu kazi ya kutosha lakini k**a vijana hao watajiinginza kwenye dhahama ya ulevi wa kupindikia, matumizi ya dawa za kulevya, bangi, mirungi,na tabia hatarishi k**a kujiingiza katika tabia ya ngono isiyo salama wataangamia na taifa itapoteza rasilimali hiyo muhimu .

Mh. Muya amewahasa vijana wanaoshiriki mdahalo huo kupitia programu za NYP+, BEILA,TIMIZA MALENGO na DREAMS ambazo zote zinashugulika na masuala ya vijana nchini na kuwataka kuwekeza katika stadi za maisha na kujielimsha zaidi kuhusu afua za kinga, tiba na matunzo ya VVU na UKIMWI zinazoratibiwa na Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto kupitia NACP kulisaidia taifa kufikia malengo ya kutokomeza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030.

Naibu Katibu Mkuu, aliwataka vijana kuwa mabalozi wa afua za tohara, kutumia kondomu, kuwa waaminifu katika mahusiano, kusikiliza na kujifunza kupitia mawaidha ya viongozi wa dini, na Kuamini katika matumizi sahihi ya ARV kwa wale wanaoishi na VVU.

Photos from NACP-Tanzania's post 29/11/2021

K**A HAVIONEKANI HAIMAANISHI VIRUSI HAVIMO - DKT ANATH RWEBEMBERA.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mdahalo wa Vijana Jijini Mbeya, Dkt. Anath Rwebembera amewapongeza watoa huduma za VVU na UKIMWI ngazi ya vituo vya huduma za afya na jamii, wadau na vijana wanaotumia ARV kwa kuzingatia taratibu za huduma na afya za walengwa kuimarika.

Dkt. Anath, ameyasema hayo alipokuwa akitoa elimu kuhusu dhana ya kutumia ARV kwa usahihi na kupungua kwa kiwango cha VVU mwilini. Dkt. Anath alisisitiza kuwa elimu sahihi kuhusu njia za uhakika za kudhibiti UKIMWI ni silaha sahihi ya kulikoa Taifa la leo na la kesho. Mfano: elimu kuhusu tabia ya vimelea vya VVU kwa watu wanaotumia ARV ni muhimu sana, maana wakati mwingine watu wanachanganya kati ya kupungua kwa wingi wa VVU mwilini na kwisha kwa VVU mwilini. Alisema jamii inapaswa kuelewa kuwa mtu anaetumia ARV kwa usahihi vimelea vinaweza kufubaa kiasi cha kutoonekana kwenye vipimo, hali hii inaweza kusababisha muhusika kudhani VVU vimekwisha mwilini na kuacha ARV au akarudia tabia hatarishi, hii ni hatari kwani kiwango cha VVU mwilini kitapanda, magonjwa nyemelezi yatajitokeza na hata kuongeza hatari ya kumuambukiza VVU mwenzi na hata kusababisha kifo.

26/11/2021
Want your business to be the top-listed Government Service in ruvuma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Ruvuma
255