Ntenga Secondary School

Directions

Ntenga Secondary School A page for Ntenga Secondary Students

🎓ALUMNI SPOTLIGHT🎓Leo tunamwangazia na kumpongeza mhitimu wetu aliyepiga hatua kubwa, aliyeacha alama, na kuendelea kuwa...
28/09/2026

🎓ALUMNI SPOTLIGHT🎓
Leo tunamwangazia na kumpongeza mhitimu wetu aliyepiga hatua kubwa, aliyeacha alama, na kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika jamii!

👤 Jina:Adv. Rahim Mjema
📜 Wadhifa/Taaluma: Mwanasheria na Wakili wa Mahak**a Kuu (Advocate)
🏫 Shule: Ntenga Secondary School
🎓 Mwaka: Form Four (Class of 2010)
Tunajivunia sana nidhamu, juhudi na mafanikio yake makubwa katika taaluma ya sheria. Hatua zake ni mfano hai wa msingi bora na thabiti tuliouweka Ntenga Secondary School!

Tunamtakia kila la kheri na mafanikio tele katika kusimamia haki na sheria:
⚖️ “Fiat justitia ruat caelum”
(Haki itendeke hata k**a mbingu zitaanguka)
⚖️ “Audatur et altera pars”
(Sikiliza na upande wa pili)
⚖️ “Ignorantia juris non excusat”
(Kutokujua sheria si kisingizio)

Hongera sana Wakili Msomi Rahim Mjema! Endelea kuangaza na kuwa njozi njema kwa wengi! 🏛️✨

👏⚖️✨

🎓 ALUMNI SPOTLIGHTLeo tunamwangazia mhitimu wetu aliyeacha alama na kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.👤 Jina: ...
28/08/2026

🎓 ALUMNI SPOTLIGHT
Leo tunamwangazia mhitimu wetu aliyeacha alama na kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
👤 Jina: Samwel Samwel (Askof)
🏫 Shule: Ntenga Secondary School
🎓 Mwaka: Form Four (Class of 2010)
Tunajivunia sana mchango, juhudi na hatua zake kubwa katika jamii! Mafanikio yake ni mfano hai wa msingi bora tuliouweka.

👏✨

🎓 ALUMNI SPOTLIGHTJina: Sajo MngaraShule: Ntenga Secondary SchoolMwaka: Form Four, Class of 2009  – Tunatekeleza Ndoto, ...
10/08/2026

🎓 ALUMNI SPOTLIGHT
Jina: Sajo Mngara
Shule: Ntenga Secondary School
Mwaka: Form Four, Class of 2009
– Tunatekeleza Ndoto, Tunaandaa Viongozi.
“Tunajivunia mchango na hatua zake katika jamii! “👏✨

07/03/2026
03/03/2026
21/02/2026

Habari za mfungo wa Ramadhani, Kwaresma, Sabato na Weekend njema kwa wote.

Gonja Vuje tunawatakia kila la kheri katika nyakati hizi za ibada, tafakari na mapumziko.

Pia, tunaomba kwa yeyote mwenye maudhui yanayohusiana na jamii yetu ya Gonja vuje iwe ni picha, makala, taarifa au jambo lolote lenye manufaa kwa jamii asisite kuwasiliana nasi kupitia barua pepe yetu rasmi: đź“§ [email protected]

Credit itatolewa kwa kila atakayewasilisha maudhui, makala au taarifa yoyote itakayochapishwa inayohusu Gonja Vuje.

Asanteni sana. Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu.

-AK

02/01/2026
02/08/2025

Ndugu Nickson Eliud MJEMA: Mzalendo Kutoka Vuje Anayeleta Tumaini Jipya kwa Same MasharikiKatika mchakato wa kumpata mgombea bora wa ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Jimbo la Same Mashariki, jina la Ndugu Nickson Eliud MJEMA limeendelea kuibua matumaini miongoni mwa wananchi — hasa wale wanaotoka Vuje, alikozaliwa na kulelewa.Ndugu Nickson ni kielelezo cha uzalendo wa kweli. Ni mzawa wa Vuje, kijiji chenye historia ya maadili, mshik**ano, na utu. Amelelewa katika mazingira yanayomjenga kiongozi anayejua kwa undani changamoto halisi za wananchi wa Same Mashariki — si kwa kusimuliwa, bali kwa kuishi nazo.Kwa sasa, ananadi sera zenye lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, yanayozingatia elimu bora, afya kwa wote, miundombinu ya kisasa, na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja.“Uongozi bora unaanzia nyumbani.”Leo tuna nafasi ya kumchagua kiongozi wetu – wa damu na roho, anayejua maumivu ya jamii yake na aliye tayari kuyapigania bungeni.Wajumbe wa CCM na wananchi wa Same Mashariki, huu si wakati wa majaribio — ni muda wa kumpa nafasi kijana wetu, mzalendo wetu, Ndugu Nickson Eliud MJEMA – sauti ya Vuje, sauti ya maendeleo.

02/08/2025

Ndugu Adrea Godfrey CHEZUE, mzaliwa halisi wa kata ya Vuje, ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Same Mashariki kupitia chama tawala cha CCM. Akiwa mzalendo, mwenye historia ya kushiriki katika maendeleo ya jamii yake, amejitokeza kuomba ridhaa ya wananchi kwa dhati kabisa.Ananadi sera zinazolenga kuimarisha huduma za kijamii, kuinua uchumi wa wananchi wa kawaida, na kuhakikisha kuwa vijana na wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo ya jimbo. Uzoefu wake katika masuala ya kijamii na uongozi, pamoja na maono yake ya kulijenga Same Mashariki kwa misingi ya haki, uwazi na maendeleo jumuishi, vinamweka katika nafasi nzuri ya kuwa mwakilishi wa kweli wa wananchi wa Vuje. Ni muda sasa kuchagua Mzalendo wa kweli, mwenye mizizi, maono na mapenzi ya dhati kwa jamii same mashariki

Address

Ntenga
Same
BOX263

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ntenga Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category