Singida Manispaa

Directions Website Contact the organization

Singida Manispaa Karibu Katika Ukurasa Rasmi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Karibu katika Ukurasa wa Halmashauri ya Manispaa Singida
Lengo la Ukurasa huu ni kuwaleta watumishi na wakazi wote wa Singida Manispaa Kwa pamoja na kupeana taarifa mbali mbali za kiutendaji ndani ya Manispaa Singida, Pia kupeana matangazo mbali mbali

TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO
07/10/2026

TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO












06/10/2026
TAHADHARI DHIDI YA MVUA ZA EL NINONi wajibu kwa kila Mwananchi kujilinda na ni vyema kuchukua tahadhari mapema.  mhando
05/10/2026

TAHADHARI DHIDI YA MVUA ZA EL NINO

Ni wajibu kwa kila Mwananchi kujilinda na ni vyema kuchukua tahadhari mapema.













mhando

KAMATI YA SIASA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI MANISPAA YA SINGIDAKamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wila...
29/09/2026

KAMATI YA SIASA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI MANISPAA YA SINGIDA

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Manispaa ya Singida.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 29, 2026 na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Bi. Lucia Mwiru wakati wa majumuisho ya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Manispaa ya Singida.

Ameongeza kuwa Manispaa imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo, hasa katika sekta za elimu, afya na uwezeshaji wa vikundi vya uzalishaji vya mikopo ya asilimia 10.

Katika ziara hiyo Kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi Mwachichi iliyopo Kata ya Mwankoko, ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Unyamikumbi B Kata ya Kisaki, ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Mungumaji Kata ya Mungumaji, kikundi cha Fighters cha Madereva Bajaji kilichopo Kata ya Misuna na ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Kindai.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imeipongeza Manispaa ya Singida kwa kuwaondoa wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa kwa hiari
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe ameipongeza Manispaa kwa ushirikiano mzuri na taasisi za Chama na kuahidi kuendelea kuisimamia ili miradi yote ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

 ——MITIHANI YA TAIFA YASOGEZWA KUEPUKA ATHARI ZA EL NINOWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya marekebisho ya r...
25/09/2026


——
MITIHANI YA TAIFA YASOGEZWA KUEPUKA ATHARI ZA EL NINO

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026, kwa lengo la kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uwezekano wa mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Serikali kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa na kutathmini athari zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa upimaji na mitihani ya Taifa.

Amesema kwa mujibu wa utabiri rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, kuna uwezekano wa kutokea kwa El Nino yenye nguvu, huku mvua zikitarajiwa kuanza katika baadhi ya maeneo mwezi Oktoba 2026 na kuwa nyingi zaidi mwezi Novemba 2026, hali ambayo inaweza kuathiri usafiri na kufikika kwa baadhi ya vituo vya mitihani.

Ameeleza kuwa kwa kuzingatia jiografia ya nchi na uwezekano wa baadhi ya maeneo kukumbwa na mafuriko, changamoto za usafiri na athari nyingine zinazoweza kusababishwa na hali ya hewa, Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyorekebishwa, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili Ngazi ya Shule utafanyika Oktoba 7 hadi 8, 2026, wakati Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 hadi 6, 2026.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili utafanyika Oktoba 12 hadi 23, 2026, huku Mitihani ya Kidato cha Nne ikifanyika kuanzia Oktoba 19 hadi Novemba 6, 2026.

Amesema marekebisho hayo yanalenga kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi, maafisa na wadau wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka muhimu.

Wizara imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali ya hewa na kuchukua hatua stahiki kwa kushirikiana na mamlaka na taasisi husika, ili kuhakikisha upimaji na mitihani ya Taifa inafanyika kwa utaratibu unaofaa, huku usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na wadau wengine ukipewa kipaumbele.

MKURUGENZI MANISPAA YA SINGIDA ASHIRIKI AMSHA ARI YA SEPTEMBA YA MAENDELEO YA JAMII.Na, Johnson SoahMkurugenzi wa Manisp...
22/09/2026

MKURUGENZI MANISPAA YA SINGIDA ASHIRIKI AMSHA ARI YA SEPTEMBA YA MAENDELEO YA JAMII.

Na, Johnson Soah

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia, ameongoza shughuli za Amsha Ari ya Septemba ya Maendeleo ya Jamii kwa kushiriki ujenzi wa Shule ya Sekondari Manguanjuki iliyopo Kata ya Mandewa.

Shughuli hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Manispaa ya Singida imefanyika leo Septemba 22, 2026 ambapo Bi. Kataraia alijumuika na mamia ya wananchi wa Kata ya Mandewa katika kazi za kubeba matofali, kuchanganya zege na upandaji wa kuta za madarasa.

Akizungumza mara baada ya shughuli hizo, Bi. Kataraia amewapongeza wananchi kwa moyo wa kujitolea na kuwataka kuendelea na ushirikiano huo ili mradi ukamilike kwa wakati.

Aidha, amewataka wananchi wote wa Manispaa ya Singida kujiandaa na mvua za El-Nino zinazotarajiwa kwa kufanya usafi na kufukua mitaro katika makazi yao.

"Tumekuja kujenga shule, lakini tujikumbushe El-Nino inakuja. Kila kaya safisha mazingira yako, fukua mtaro, usitupie taka mtaroni. Tukijikinga mapema hatutaathirika," alisisitiza Bi. Kataraia.

Kwa upande wake Mhandisi wa Manispaa, Mhandisi Edna Mhando, amesema mradi wa Shule ya Sekondari Manguanjuki una thamani ya Shilingi Milioni 544 na hadi sasa umefikia asilimia 35% ya utekelezaji, na unatarajiwa kukamilika Novemba, 2026.

Naye Diwani wa Kata ya Mandewa, Mhe. Yusufu Mpaki amemshukuru Mkurugenzi na Halmashauri kwa kuileta shule hiyo kimkakati katika kata yake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa Mandewa wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule hiyo kwani watoto wao hawatatembea umbali wa muda mrefu tena kufuata elimu.

WANANCHI WA MANISPAA YA SINGIDA KUNUFAIKA NA MFUMO WA e-ARDHINa, Johnson Soah Wananchi wa Manispaa ya Singida wameanza k...
21/09/2026

WANANCHI WA MANISPAA YA SINGIDA KUNUFAIKA NA MFUMO WA e-ARDHI
Na, Johnson Soah
Wananchi wa Manispaa ya Singida wameanza kunufaika na mfumo mpya wa kielektroniki wa maombi ya viwanja ujulikanao k**a e-Ardhi, baada ya baadhi yao kuanza kupata hati zao kupitia mfumo huo.

Hayo yamebanishwa leo Septemba 21, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe Halima Dendego wakati akifunga mafunzo ya siku nane kwa Maafisa Ardhi wa mkoa huo yaliyofanya katika ukumbi wa Samaki Samaki, Manispaa ya Singida.

Akizungumzia mfumo huo, Mhe. Dendego amesema utawaondolea wananchi adha ya kufuata huduma za ardhi, kwani sasa wanaweza kuomba viwanja wakiwa mahali popote kwa kutumia simu janja.

"Kwa kweli nitumie nafasi hii kuishukuru Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kubuni mfumo huu, sasa wananchi hawatapata adha tena ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya hati za viwanja vyao," alisema Dendego.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha wananchi kupitia majukwaa mbalimbali ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu mfumo huo.

Kwa upande wake, mmoja wananchi waliopata hati kupitia mfumo huo, Bi. Regina Mollel, amesema mfumo huo umekuwa mkombozi kwake kwa kuwa ni rahisi kutumia na anaweza kuhudumiwa hata akiwa nyumbani.

Naye Afisa Ardhi Mteule Manispaa ya Singida, Bw. Nyambega Kichele, amesema baada ya mafunzo hayo wataenda kutoa elimu kwa wakazi wa Manispaa hiyo ili kuwaondolea changamoto za masuala ya ardhi zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA HUDUMA KITUO CHA AFYA SOKOINENa, Johnson SoahKamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida imeridhis...
19/09/2026

KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA HUDUMA KITUO CHA AFYA SOKOINE

Na, Johnson Soah

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida imeridhishwa na kupongeza huduma zinazotolewa katika Kituo cha Afya Sokoine kilichopo Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida kwa kutoa huduma za viwango vya ubora kwa wagonjwa wanaofika kupata matibabu.

Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 19, 2026 na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, Bi. Martha Mlata wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Mlata amesema huduma za Kituo cha Afya Sokoine zinasifika kwa kutoa huduma bora ambayo imekuwa kimbilio kwa wananchi wengi hata kutoka nje ya Manispaa ya Singida.

"Wakati natembelea hapa nimeingia ndani ya jengo la wazazi katika Kituo, nimekuta akina mama wanaosubiri kujifungua wana furaha sana, hii inatokana na huduma bora wanaopata hapa. Niwapongeze wafanyakazi wa hiki Kituo cha Afya, hongereni sana kwa kufanya kazi kwa bidii," alibainisha.

Aidha, kabla ya kutembelea Kituo cha Afya Sokoine, Kamati ya Siasa ilitembelea na kujionea maendeleo mazuri ya ujenzi wa Soko la Vitunguu lenye thamani ya shilingi Bilioni 3.8 ambao umefikia 37 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2027

Katika hatua nyingine, Bi. Mlata ameelekeza kujengwa kwa uzio katika Kituo cha Afya Sokoine ili kuepuka mwingiliano na kwa ajili ya ulinzi wa wagonjwa, wafanyakazi na mali za kituo hicho, huku akishauri kujenga majengo mengine zaidi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wengi zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego ameagiza wataalamu kufanya tathmini ya ujenzi wa uzio huo ili uanze mara moja.

Address

Ipembe
Singida
236

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:29 - 17:00
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Singida Manispaa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Singida Manispaa:

Shortcuts

Share