Ikulu habari Zanzibar

Call Directions Website

Ikulu habari Zanzibar Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

RAIS DKT. MWINYI: ZANZIBAR KUIMARISHA USHIRIKIANO NA KOREA KUSINI KATIKA UTALII, UCHUMI WA BULUU NA TEKNOLOJIARais wa Za...
27/10/2026

RAIS DKT. MWINYI: ZANZIBAR KUIMARISHA USHIRIKIANO NA KOREA KUSINI KATIKA UTALII, UCHUMI WA BULUU NA TEKNOLOJIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar inalenga kuimarisha ushirikiano na Korea Kusini katika utalii, uchumi wa buluu, nishati mbadala, viwanda, teknolojia na elimu.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 27 Oktoba 2026, jijini Yeosu, alipokutana na Meya wa Jiji la Yeosu, Mhe. Seo Young-hak, na kujadili fursa za ushirikiano na uwekezaji.

Katika ziara hiyo, ametembelea kampuni za POSCO na K-Food, pamoja na Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026, kujifunza teknolojia za uzalishaji viwandani na uchakataji wa mwani kwa lengo la kuongeza thamani ya bidhaa na kukuza uchumi wa Zanzibar.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
27/10/2026

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

RAIS DKT. MWINYI AWASILI KOREA KUSINIRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi...
27/10/2026

RAIS DKT. MWINYI AWASILI KOREA KUSINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa ameambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake, amewasili nchini Jamhuri ya Korea (Korea Kusini) kwa ziara ya kikazi itakayoanza tarehe 27 Oktoba, 2026.

Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Noel Emmanuel Kaganda, pamoja na maafisa wengine wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Akiwa Korea Kusini, Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kushiriki Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026 jijini Yeosu pamoja na Jukwaa la 27 la Sera za Utalii kwa Visiwa (ITOP Forum 2026) katika Kisiwa cha Jeju.

RAIS DKT. MWINYI KUELEKEA KOREA KUSINI KUSHIRIKI MAJUKWAA YA UTALIIRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi...
25/10/2026

RAIS DKT. MWINYI KUELEKEA KOREA KUSINI KUSHIRIKI MAJUKWAA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuondoka nchini leo, tarehe 25 Oktoba 2026, kuelekea Korea Kusini kushiriki Jukwaa la 27 la Sera za Utalii kwa Visiwa na kutembelea Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026, yatakayofanyika Jijini Yeosu, katika Kisiwa cha Jeju.

Ushiriki huo unalenga kuitangaza Zanzibar kimataifa, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya utalii, kuvutia uwekezaji na kuongeza idadi ya watalii, hatua zitakazochangia kukuza uchumi na fursa za ajira kwa wananchi.

Jummah Mubarak.
23/10/2026

Jummah Mubarak.

22/10/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha wajumbe wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Tume hiyo ina jukumu la kuratibu mipango ya maendeleo, kuweka vipaumbele na kufuatilia utekelezaji wake.

Hafla ya uapisho imefanyika leo, tarehe 22 Oktoba 2026, Ikulu Zanzibar, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Wajumbe walioapishwa ni:
1. Mhe. Mansura Mosi Kassim
2. Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji
3. Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed
4. Mhe. Omar Said Shaaban
5. Mhe. Rahma Kassim Ali
6. Mhe. Shaaban Ali Othman
7. Mhe. Dkt. Juma Malik Akil
8. Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar
9. Mhe. Amina Khamis Shaaban
10. Mhe. Joseph J. Semboja
11. Mhe. Dkt. Twahir Mohammed Khalfan

RAIS DKT. MWINYI AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA MIPANGO ZANZIBARRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe...
22/10/2026

RAIS DKT. MWINYI AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA MIPANGO ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha wajumbe wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Tume hiyo ina jukumu la kuratibu mipango ya maendeleo, kuweka vipaumbele na kufuatilia utekelezaji wake.

Hafla ya uapisho imefanyika leo, tarehe 22 Oktoba 2026, Ikulu Zanzibar, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Wajumbe walioapishwa ni:
1. Mhe. Mansura Mosi Kassim
2. Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji
3. Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed
4. Mhe. Omar Said Shaaban
5. Mhe. Rahma Kassim Ali
6. Mhe. Shaaban Ali Othman
7. Mhe. Dkt. Juma Malik Akil
8. Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar
9. Mhe. Amina Khamis Shaaban
10. Mhe. Joseph J. Semboja
11. Mhe. Dkt. Twahir Mohammed Khalfan

21/10/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza leo, Oktoba 21, 2026, alipokutana na Mhasham Baba Askofu Lameck Paul Ndomba, Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar.

Address

Zanzibar
Stone Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ikulu habari Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share