05/10/2026
_AL AMAL YAKABIDHI VITI MWENDO VITATU - CHUNGURIRA, TANGA_
Ndugu wadau wa Al Amal Charitable Foundation,
Siku ya jana tarehe _04/10/2026_, Taasisi ya Al Amal Charitable Foundation imefanikiwa kufika Kata ya Tangasisi, Mtaa wa Chungurira kwa ajili ya kukabidhi _Viti Mwendo vitatu_ kwa watoto wenye ulemavu.
Zoezi hilo liliongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo, _Ndugu M***a Lumwe Jumaa_, ambaye alisimamia zoezi zima la ugawaji wa viti hivyo.
Mwenyekiti ametoa shukrani za dhati kwa Taasisi ya Al Amal Charitable Foundation kwa kutimiza ahadi yake ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu.
Aidha, Katibu wa Taasisi ya Al Amal Charitable Foundation, Ndugu Salmin Ganga, kwa niaba ya Taasisi ametoa shukrani za dhati na kumpongeza _Ndugu Mohamed Hilali (Ba Magongo)_ pamoja na Asasi ya SEMA na Tanga kwa kushirikiana na Taasisi kuhakikisha viti hivyo vinapatikana na watoto wenye uhitaji wanapata msaada.
Taasisi inatoa wito kwa wazazi kutunza viti hivyo walivyokabidhiwa watoto wao, pamoja na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana katika kutatua changamoto za kijamii.
Jazakumullahu Khairan.
_Imetayarishwa na:_
_Katibu - Salmin Ganga_
_0674435000_
_Al Amal Charitable Foundation_
_05/10/2026_