ULEMO MPYA

Directions

ULEMO MPYA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ULEMO MPYA, Political organisation, Ulemo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (MB), Iramba MagharibiAmetuma salamu za rambi ...
22/09/2026

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (MB), Iramba Magharibi

Ametuma salamu za rambi rambi na za pole kufuatia taarifa ya ajali iliyotokea leo Wilayani Iramba, Mkoa wa Singida, na kusababisha vifo vya watu 12, wakiwemo mahabusu saba na Askari Polisi watano.

"Ninaungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa pole kwa familia za marehemu, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na awape wafiwa subira na faraja. Amina."

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia  kifo cha Mama ...
22/09/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia

kifo cha Mama yetu, Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kilichotokeo leo tarehe 21 Septemba, 2026.

​Kifo chake ni pengo kwa familia na Taifa kwa ujumla, kwani alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu.

​Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

​Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 1...
22/09/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12, wakiwemo mahabusu saba na askari polisi watano, vilivyotokea leo katika Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, baada ya ajali iliyohusisha gari la Jeshi la Polisi na lori.

Rais Samia ametoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Omary Dendego, familia za marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania wote kufuatia msiba huo.

Aidha, amewasisitiza madereva wote kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani na kuhakikisha vyombo vya moto vinakuwa katika hali nzuri na salama kabla ya kutumika, ili kulinda maisha ya wananchi na watumiaji wengine wa barabara.

Rais Samia amewaombea marehemu wapumzike mahali pema peponi.

21/09/2026

Fatma Karume, mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume,

amefariki dunia Septemba 21, 2026 akiwa na umri wa miaka 97. Kifo chake kimethibitishwa na Makamu wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, kikiwa kimetokea Mbweni usiku huo

Alizaliwa Februari 2, 1929 Bumbwini Misufini, Kaskazini Unguja, na baadaye kuolewa na Sheikh Abeid Amani Karume. Alijulikana kwa harakati za kisiasa, hususan kutetea haki za wanawake na ushiriki wao katika uchaguzi.

Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 1964, alihudumu k**a Mama wa Kwanza wa Taifa hadi mwaka 1972 alipofariki mume wake. Pia alikuwa mama wa Rais wa zamani wa Zanzibar Amani Abeid Karume (2000–2010).”

21/09/2026

AJALI IRAMBA: WATU 12 WAPOTEZA MAISHA MLIMA SEKENKE

Watu 12 wamefariki dunia, wakiwemo askari 5 wa Polisi na mahabusu 7, katika ajali iliyotokea eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.

Ajali hiyo imehusisha gari la tanki la mafuta na gari la Jeshi la Polisi lililokuwa limewabeba mahabusu pamoja na askari kuelekea Mahak**a ya Kiomboi.

Watu wawili wamejeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu.

Taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa.

21/09/2026
ASKARI, MAHABUSU 12 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE, WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDAAskari na ma...
21/09/2026

ASKARI, MAHABUSU 12 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE, WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDA

Askari na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la polisi walilokuwa wakisafiria kugongwa na lori la mizigo katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa.

21/09/2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi ameungana na wananchi mbalimbali kufanya mazoezi ...
19/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi ameungana na wananchi mbalimbali kufanya mazoezi ya asubuhi katika barabara ya fukwe za Coco beach kuelekea Daraja la Tanzanite, Jijini Dar es Salaam, Septemba 19, 2026.

Address

Ulemo

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ULEMO MPYA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share